Papa Leo XIV,huko Bamenda:"Ole anayetumia dini kwa malengo ya kiuchumi na kijeshi"
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV tarehe 16 Aprili 2026 aliendelea na Ziara yake nchini Cameroon, na kusafiri kwa Ndege hadi Bamenda eneo linalojulikana na mateso ya watu ambapo alifanya Mkutano wa amani na Jumuiya ya Bamenda kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu. Katika Hotuba yake ya Tatu kwenyeTaifa hilo alianza kuonesha furaha kuwa katikati yao katika Mkoa wa Mateso. Kulingana na ushuhuda wa waliotangulia, Papa alipenda kuwa kama shuhuda zilivyojionesha, uchungu wote ulioikumba Jumuiya yao, unafanya leo hii kuwa na utambuzi wa usumbufu usio isha kwamba “Mungu hatuachi kamwe! Katika Yeye, katika amani yake, tunaweza kiurahisi kutanza upya! Akigusia ushuhuda wa Askofu Mkuu, Papa alisema kuwa Askofu Mkuu alikumbusha unabii unaotangazwa: “Jinsi gani ilivyo mizuri miguu yake juu ya milima kwa yule aletaye habari njema ya amani!" (Is 52,7).
Papa alisema hivyo kwamba kufika kwake katikati yao na sasa, Papa alitaka kujibu, kuwa: "Miguu yenu pia ni mizuri sana, imechafuka kutokana na udongo huu uliojaa damu lakini wenye rutuba, kutokana na udongo huu uliojaa hasira, lakini pia ina mimea mingi na matunda mengi." Ni miguu ambayo imewaleta hadi hapa na licha ya kukutana na majaribu na vizingiti, viliwasindikiza katika njia ya wema. “ Sote tunaendelea katika hatua hizo za wema na amani.” Papa Leo XIV aliwashukuru kwa sababu, ni kweli! “Niko hapa ili kuwatangazia amani, lakini kwa haraka ninakutana nanyi ambao mnanitangazia mimi na ulimwengu wote.”
Mgogoro uliokumba Cameroon
Kiukweli, Papa alisema, kama mmoja wao alivyokumbusha, mgogoro ambao umeikumba Mikoa ya Cameroon, iliwakaribia zaidi kuliko hapo awali Jumuiya nzima za Kikristo na za kiislamu, kiasi kwamba viongozi wenu wa kidini waliungana na kuanzisha Harakati kwa ajili ya amani, ambayo inatafuta kuweka maridhiano kati ya sehemu zinazokinzana. Katika maeneo haya, ninataka kuwa iweze kuwa hivi! Heri wahudumu wa amani! Kinyume chake, Ole anayetumia dini na kwa jina lenyewe na kwa kutumia malengo yake binafsi kijeshi, kiuchumi na kisiasa, kwa kupuuza kile ambacho ni kitakatifu kwenye kile kilicho kichafu zaidi na cha giza.”
Ninyi ni wenye njaa na kiu ya haki
Baba Mtakatitu Leo XIV aliendelea kusema kuwa “ninyi ni wenye njaa na kiu ya haki, ninyi masikini, wa huruma, wapole na wanyofu wa moyo, ninyi mliolia, ni mwanga wa dunia (Mt 5,3-4) Bamenda leo hii, wewe ni mji juu ya mlima, unaong’aa machoni pa wote! Baba Mtakatifu aliewaeleza kwamba wao ni chumvi kwa muda mrefu inayotoa ladha, katika ardhi hiyo, “msipoteza ladha yenu hata kwa miaka ijayo! Thamini kile ambacho kinawakaribia na kushirikishana katika saa ya kulia. Ninyi ni mafuta ambayo yanapakwa kwenye majeraha ya ubidamu. Kwa mtazamo huo, Papa alitoa shukrani kwa wote ambao kwa namna ya pekee wanawake, walei, na watawa ambao wanatoa utunzaji wa watu waliopata viwewe vya vurugu. Ni kazi kubwa sana, isiyooonekana yenye hatari, kila siku na kama alivyokumbusha Sr Carine, Mabwana wa vita wanajifanya kutoelewa kwamba, inashosha kidogo kuharibu, lakini mara nyingi siyo rahisi kuweza kujenga maisha.
Wanajifanya kutoona kuwa, inahitajika mabilioni ya dola ili kuua na kuharibu, lakini hawapati rasilimali muhimu kuponesha wagonjwa, kuelimisha na kuinuka tena. Anayeiba ardhi yenu kutoka kwenye rasilimali zake, kwa kawaida anawekeza kwenye silaha nzuri , ambazo kwa sehemu kubwa ya faida ni katika mzunguko wa uthabiti na kifo kisicho na mwisho.” Ni ulimwengu uliopinduliwa, upotoshaji wa uumbaji wa Mungu ambao kila dhamiri nyofu lazima iulaani na kuukataa, ikichagua mabadiliko hayo, uongofu, unaoongoza upande mwingine, kwenye njia endelevu na tajiri ya udugu wa kibinadamu. Dunia inaangamizwa na watawala wachache na inaunganishwa pamoja na maelfu ya kaka na dada kwa mshikamano! Wao ni wazao wa Ibrahimu, wasiohesabika kama nyota za angani na chembe za mchanga kwenye ufukwe wa bahari.
Tutazamane machoni tayari sisi ni watu wakubwa
Papa alisema kuwa “Tutazamane machoni: tayari sisi ni watu wakubwa sana! Amani si kitu cha kubuniwa: ni kitu cha kukumbatiwa, kuwakaribisha wengine kama kaka na dada. Hakuna anayechagua kaka na dada zao: tunapaswa tu kukaribishana! Sisi ni familia moja na tunaishi katika nyumba moja, sayari hii nzuri ambayo tamaduni za kale zimeitunza kwa milenia.” Papa Francisko aliandika katika Wosia wake wa Kitume wa Evangelii Gaudium, kitu ambacho kilirudikwenye akili ya Papa kwa kusikiliza maneno ya mashuhuda yake: “Utume wangu kwa mioyo ya watu si sehemu ya maisha yangu, au pambo ninaloweza kuondoa, si kiambatisho, au wakati mmoja kati ya mingi katika maisha yangu. Ni kitu ambacho siwezi kukiondoa kutoka kwangu isipokuwa ninataka kujiangamiza. Mimi ni utume hapa duniani, na ndiyo maana niko katika ulimwengu huu,”(EG 273).
Papa aliwaeleza watu wa Bamenda kuwa hizo ndizo hisia zake ambao alikuwa katikati yao. “Tuhudumie pamoja amani.” Lazima kujitambua sisi wenyewe kama waliowashwa moto wa utume huo wa kuangazia, kubariki, kuhuisha, kuinua tena, kubariki na kukomboa. Hapo anajionesha muuguzi katika nafsi, mwalimu katika nafsi, mwanasiasa katika nafsi na wanafunuliwa, wale ambao wameamua ndani kabisa kuwa pamoja na wengine na kwa ajili ya wengine.” Papa tena alikumbuka Mtangulizi wake: “mtangulizi wangu alitushauri kutembea pamoja, kila mmoja kwa wito wake binafsi, kwa kupanua mipaka ya Jumuiya zetu, kwa uhalisia wa kuanza tena kuanzia na kazi mahalia ili kufikia katika upendo wa jirani, kila mtu mahali popote pale.
Ni mapinduzi ya kimya ambayo ninyi ni mashuhuda! Kama alivyosema Imam, Tumshukuru Mungu ambaye katika mgogoro huu hapakuzaliwa vita vya kidini, na ambapo tunaishi bado tukitafuta kupendana mmoja na mwingine. Kwa njia hiyo Papa Leo XIV alihimiza waendelee mbele bila kuchoka kwa ujasiri na hasa pamoja na daima kwa pamoja. Tutembee pamoja katika upendo, tukitafuta amani siku zote.”
Kurusha Njia ishara ya Amani
Mwishoni mwa hotuba yake, Papa alitoka Nje ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu na kueleza walikuwa umati ulikuwa kwenye Uwanja huo kuwa: “kaka na dada zangu wapendwa, leo Bwana ametuchagua sisi sote kwa wafanyakazi wanaoleta amani katika nchi hii! Sote tumwombe Bwana, kwamba amani itawale kweli miongoni mwetu, kwamba tunapowaachilia hawa njiwa weupe, ishara ya amani, kwamba amani ya Mungu iwe juu yetu sote, juu ya nchi hii, na kutuweka sote katika umoja katika amani Yake.”
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here
