2026.04.27 Papa atembelea Chuo cha Kipapa cha Kanisa katika fursa ya miaka 325 ya chuo hicho. 2026.04.27 Papa atembelea Chuo cha Kipapa cha Kanisa katika fursa ya miaka 325 ya chuo hicho.  (@VATICAN MEDIA)

Papa Leo XIV:Diplomasia ya Kipapa ni kukuza na kulinda heshima ya wote

Akitembelea Chuo cha Kipapa cha Kanisa katika hafla ya maadhimisho ya miaka 325,Papa Leo XIV alielezea juu ya diplomasia ya Kipapa na kwamba mjumbe wake ni wa amani,ni mtetezi wa familia ya wanadamu na sio Jumuiya ya Wakatoliki tu.Kwa hiyo ni ya"huduma ya amani,ukweli na haki kwa wote waliumbwa kwa mfano na sura ya Mungu na kukuza wema wa pamoja."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV, Jumatatu tarehe 27 Aprili 2026 alitembelea Chuo cha Kipapa cha Kanisa jijini  Roma, ambapo katika hotuba yake alifafanua juu ya  wito maalum kwa  Padre wa kidiplomasia ya kipapa ambaye anaitwa kujikita na Diplomasia ya  huduma ya amani, ukweli na haki. Mkutano huo ulifanyika ndani ya muktadha wa maadhimisho ya miaka 325 ya kuanzishwa kwa taasisi hiyo, ambayo Papa alikuwa tayari ameitembelea kabla ya kuchaguliwa kuwa Kharifa wa Mtume  Petro, alipokuwa Mwenyekiti wa  Baraza la Kipapa la Maaskofu.

Papa akitia saini katika Chuo cha Kipapa cha Kanisa
Papa akitia saini katika Chuo cha Kipapa cha Kanisa   (@VATICAN MEDIA)

Kujenga umoja kati ya tofauti

Baba Mtakatifu Leo XIV katika hotuba yake alionesha shukrani kubwa kwa historia ya kujitolea na huduma iliyoadhimishwa na maadhimisho haya ya furaha. Ni historia muhimu, iliyowezeshwa na mapadre  kutoka ulimwenguni kote ambao wamechangia kwa juhudi zao za unyenyekevu za kujenga umoja huo katika Kristo ambao, kati ya utofauti wa asili, hufanya ushirika kuwa sifa inayofafanua Kikosi cha Kidiplomasia ya Vatican.

Papa akitia saini yake katika Chuo cha Kipapa cha Kanisa
Papa akitia saini yake katika Chuo cha Kipapa cha Kanisa   (@VATICAN MEDIA)

Mageuzi ya kufufua muundo wa mafunzo

Papa Leo XIV kadhalika  alitafakari kuhusu mageuzi ambayo yameipatia taasisi hiyo uhuru unaohitajika ili kufufua muundo wa mafunzo ya sheria, historia, sayansi ya siasa na uchumi, pamoja na utafiti wa lugha zinazotumika katika mahusiano ya kimataifa. Hata hivyo kuna mageuzi muhimu zaidi, alisisitiza kwamba ni ya zoezi la uongofu la mara kwa mara, linalolenga kukuza ukaribu, kusikiliza kwa makini, ushuhuda, mbinu ya kidugu na mazungumzo,  pamoja na unyenyekevu na upole, fadhila zote ambazo lazima zienee katika huduma yao yote ya ukuhani, Papa alisisitiza.

Ramani ya Chuo cha Kipapa cha Kanisa
Ramani ya Chuo cha Kipapa cha Kanisa   (@VATICAN MEDIA)

Amani iwe nanyi:utume unakuwa madaraja na njia

Akiwakumbuka watakatifu, wenyeheri na Mapapa ambao wameunda historia ya Chuo hicho, Baba Mtakatifu aliakisi jukumu la kipekee la Padre  wa kidiplomasia wa kipapa kwamba ni mjumbe wa tangazo la Pasaka lile la, “Amani iwe nanyi!” Hata wakati matumaini ya mazungumzo na upatanisho yanaonekana kufifia, bado ni muhimu kupeleka maneno yote ya Kristo Mfufuka asemaye:  "Ninawaachieni amani, nawapeni  amani yangu," Papa alisisitiza. Kwa kusisitiza zaidi, Papa alisema “Utume wenu unawataka kuwa madaraja na njia ili neema itokayo mbinguni iweze kuingia katika historia.

Muda wa kuzungumza na wanachuo
Muda wa kuzungumza na wanachuo   (@VATICAN MEDIA)

Diplomasia ya Papa ni kupeleka ukweli

Katika kudadavua aidha Baba Mtakatifu alibainisha kuwa Kazi nyingine ya mwanadiplomasia wa kipapa ni kupeleka Ukweli  ambao ni Kristo, katika mkutano wa mataifa, kuwa ishara ya upendo Wake kwa sehemu hiyo ya ubinadamu iliyokabidhiwa kwa uangalizi, awali  kama mchungaji, na kisha tu kama mwanadiplomasia. Kwa njia hiyo Papa Leo XIV alirudia, kama alivyofanya katika hotuba yake ya Kikundi cha Kidiplomasia kilichoidhinishwa na Vatican , mwanzoni mwa mwaka 2026, kwamba maneno yale yana uzito na lazima tena "yaeleze ukweli waziwazi na bila utata, ili kukuza mazungumzo halisi bila kutoelewana, kwa kushuhudia kile ambacho kimekuwa mwili."

Kupokea zawadi
Kupokea zawadi   (@VATICAN MEDIA)

Huduma ya mwanadiplomasia si kwa jumuiya ya wakatoliki

Kwa kupanua mtazamo wake lazima kukumbatia familia nzima ya wanadamu, “kwani huduma ya mwanadiplomasia huyo haishii na Jumuiya ya Wakatoliki tu. Kwa hiyo Papa alisema inawataka kuwa watetezi wa kila aina ya haki inayosaidia kutambua, kurejesha na kulinda taswira ya Mungu iliyochorwa ndani ya kila mtu. Katika ulimwengu uliojaa mvutano, ambao unaonekana kufanya migogoro kuwa njia pekee ya kushughulikia mahitaji, juhudi zetu za kujitolea kwa mazungumzo, kusikiliza na upatanisho zinaweza kuonekana kuwa hazitoshi, wakati mwingine hata hazina maana, Papa alisema."

Watawa wanahudumia katika Chuo cha Kipapa cha Kanisa
Watawa wanahudumia katika Chuo cha Kipapa cha Kanisa   (@VATICAN MEDIA)

Wakati huo huo katika salamu zake, Askofu Mkuu Salvatore Pennacchio, Rais wa Chuo cha Kipapa cha Kanisa, alisisitiza kwamba ziara ya Papa ni chanzo cha kutia moyo katika njia ya maandalizi ya huduma katika diplomasia ya Vatican. Pia alitoa matashi mema  yake kwa Kardinali Pietro Parolin katika maadhimisho ya miaka 46 ya kuwekwa wakfu kwake kwa ukuhani, ambayo ilifanyika tarehe 27 Aprili 1980.

Papa akiondoka kutoka ndani ya chuo cha Kipapa cha Kanisa
Papa akiondoka kutoka ndani ya chuo cha Kipapa cha Kanisa   (@VATICAN MEDIA)
CHUO CHA KIPAPA CHA KIKANISA

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here

27 Aprili 2026, 19:55