Papa akutana na wakuu wa Mashirika ya Kitawa nchini Cameroon

Katika Ukumbi wa Ubalozi wa Vatican huko Yaoundé,PapaLeo XIV alizungumza na Watawa wa kike na kiume 9,Wakuu wa Mashirika ya Kitaifa na Kimataifa na Taasisi na vyama vya Kitume zaidi ya 250 wakitoa huduma nchini.Walishirikisha changamoto wanazokabiliana na huduma ya kichungaji kwa vijana,waliokimbia makazi yao,waathiriwa wa vurugu na biashara haramu ya binadamu.Papa aliwakumbusha,"maisha yaliyowekwa wakfu ni sehemu muhimu ya maisha ya Kanisa."

Vatican News

Baada ya siku ya tatu ya safari ndefu nchini Cameroon, kati ya asubuhi huko Douala na alasiri huko Yaoundé, Baba Mtakatifu  Leo XIV, aliporudi kwenye Ubalozi wa Vatican, alikutana na kundi la watawa tisa wanaowakilisha Mashirika ya Kitawa ya Kitaifa na ya Kimataifa na taasisi za Kitume, za mashirika zaidi ya 250 yanayohudumu nchini Cameroon.

Papa Leo akisikiliza historia za watawa
Papa Leo akisikiliza historia za watawa   (@Vatican Media)

Haya yalielezwa na Ofisi ya Habari ya Vatican kupitia chaneli yake ya Telegram, ikielezea kwamba "Papa alisikiliza maneno waliyomwambia, shukrani zao kwa ziara yake nchini na kwa maneno yake katika siku za hivi karibuni. Simulizi ya kujitolea kwao na ushuhuda wao katika hali nyingi za mateso nchini humo, na ile ya vijana, watu waliohamishwa makazi yao, waathiriwa wa vurugu na biashara haramu ya binadamu, hitaji la waamini kushirikiana kwa karibu zaidi na Maaskofu na Mapadre wa Majimbo, na maswali kuhusu utambulisho wao wa kitawa unaojitokeza ndani ya Mashirika.

Katika usikivu wa historia za watawa
Katika usikivu wa historia za watawa   (@Vatican Media)

Kuhamasisha Karama

Kwa upande wake Papa aliwahutubia kwa ufupi, kwanza akiwashukuru kwa fursa iliyotolewa na mkutano na kwamba: "Maisha yaliyowekwa wakfu ni sehemu muhimu ya maisha ya Kanisa!" Papa Leo XIV alizungumzia suala halisi la uhusiano kati ya maisha yaliyowekwa wakfu na Maaskofu na Mapadre wa Majimbo, akikumbuka kwamba miongoni mwa hitimisho la Sinodi iliyopita lilikuwa pendekezo la kikundi cha utafiti kusasisha hati ya Mutuae Relationes, na jinsi, kwa maana hiyo, ni muhimu kutambua na kuhamasisha karama mbalimbali za mashirikia yaliyopo katika kila Jimbo.

Sala ya Baba Yetu pamoja
Sala ya Baba Yetu pamoja   (@Vatican Media)

Papa pia alizungumzia kuhusu malezi katika maisha yaliyowekwa wakfu, kila shirika  kulingana na sifa zake maalum, na jinsi ya kusikiliza kwa pamoja kunavyohitajika ili kuwaandaa watahiniwa kukumbatia maisha ya sadaka, kujitolea,na huduma katika jumuiya. Pia alielezea jinsi ambavyo changamoto fulani, kama vile kuishi pamoja kati ya watu wa imani na dini tofauti, na huduma ya vijana, zinavyohitaji kutafakari ndani ya kila taasisi au jumuiya, kwa kushirikiana na majimbo, ambapo karama huwekwa katika huduma ya Kanisa katika kila ngazi.

Papa alitoa Baraka
Papa alitoa Baraka   (@Vatican Media)

Alijibu changamoto ngumu za leo hii

"Mmetaja hotuba za siku hizi: Papa amewasili, Papaanaondoka," lakini ninyi mnayo yale ambayo yamesemwa," Papa aliongeza, akikumbuka jukumu la kuchukua kile kilichosemwa na kutafakari na kushirikisha ujumbe wa ziara hiyo ili kukabiliana na changamoto ngumu za wakati huu. Na "maisha yaliyowekwa wakfu," Papa Leo XIV alihitimisha, "yanatuhitaji kuwa jasiri, wakati mwingine wenye msimamo mkali, katika uchaguzi wetu wa kutangaza bila woga kile ambacho Yesu anatufundisha katika Injili, wanafunzi wanaofikia matatizo magumu zaidi, ncha za mbali zaidi za dunia, wadogo zaidi, wafungwa, wale wanaohitaji zaidi tumaini la upendo wa Mungu." Hatimaye, Papa aliwabariki wale wote waliokuwepo, na pamoja nao akasali sala ya  Baba Yetu, kabla ya kuwasalimia kila mmoja wao.

Papa akutana na wawakilishi wa watawa
Papa akutana na wawakilishi wa watawa   (@Vatican Media)

Asante kwa kusoma makala haya. Ikiwa unataka kuendelea kupata taarifa mpya, tunakualika ujiandikishe kwa jarida. cliccando qui

Picha za Mkutano

Picha ya Papa na mtawa
Picha ya Papa na mtawa   (@Vatican Media)

 

Salamu
Salamu   (@Vatican Media)

 

Salamu
Salamu   (@Vatican Media)
PAPA KWA WAKUU WA WATAWA

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here

 

 

17 Aprili 2026, 20:40