Papa Leo XIV wakati alipokwenda kwenye Karubu la Papa Francisko Papa Leo XIV wakati alipokwenda kwenye Karubu la Papa Francisko   (@Vatican Media)

Papa Leo XIV amkumbuka Papa Francisko:Alitoa mengi na alikuwa zawadi kwa Kanisa na Ulimwengu

Katika safari ya ndege kutoka Angola hadi Guinea ya Ikweta,kituo cha mwisho cha Ziara yake ya Kitume, barani Afrika,Papa Leo XIV alimkumbuka kwa furaha mtangulizi wake katika kumbukumbu ya mwaka wa kwanza wa kifo chake:"Alitoa mengi kwa maisha yake na ukaribu wake na maskini."

Na Salvatore Cernuzio- Luanda/Malabo

"Katika kumbukumbu hii ya kwanza ya kifo chake, ningependa kumkumbuka Papa Francisko, ambaye aliacha nyuma na kutoa mengi kwa Kanisa, kwa maisha yake, ushuhuda wake, maneno yake, na matendo yake. Kwa kile alichofanya, kuishi karibu na maskini zaidi, wadogo zaidi, wagonjwa, watoto, na wazee." Ni siku ya kutoka kwake Angola kuelekea Guinea ya Ikweta, kituo cha mwisho katika Ziara  yake ya Kitume barani Afrika, lakini pia ilikuwa ni siku maalum: ya kumbukizi ya mwaka wa kwanza tangu kifo cha Papa Francisko, ambaye alifariki alfajiri ya tarehe 21 Aprili 2025.

Ukumbusho ukikumbukwa kwa ushiriki mkubwa ulimwenguni kote na wakati wa safari ya ndege ya kwenda Malabo, Papa mwenyewe alitoa hata wazo la kibinafsi kwa mtangulizi wake, ambalo alishirikisha waandishi wa habari wapatao 70 katika msafara wake.

Kukuza Udugu

Kumbukumbu iliyojaa upendo na shukrani kwa Papa ambaye, alisema, "aliacha mengi nyuma ya Kanisa kwa ushuhuda wake na maneno yake." "Mambo mengi" yanaweza kukumbukwa kuhusu Jorge Mario Bergoglio, lakini Papa Leo XIV alikumbuka kwanza kabisa agizo lake lisilokoma la "udugu wa ulimwengu wote:" Papa Francisko alijitahidi kweli "kukuza heshima ya kweli kwa wanaume wote, wanawake wote, kukuza roho ya udugu, ya kuwa kaka na dada, sisi sote, ya kutafuta jinsi ya kuishi ujumbe tunaoupata katika Injili."

Papa akizungumza na waandishi wa habari wakati anaelekea Guinea ya Ikweta
Papa akizungumza na waandishi wa habari wakati anaelekea Guinea ya Ikweta   (@Vatican Media)

Ujumbe wa huruma

"Ujumbe"mwingine wa Papa Francisko ambao Papa Leo XIV alikumbuka ni ule wa "huruma” uliotolewa wakati wa Sala ya  Malaika wa Bwana,  baada ya kuchaguliwa kwake mnamo tarehe 13 Machi 2013. "Mara hiyo ya kwanza katika Sala ya Malaika wa Bwana, lakini pia katika Misa Takatifu alioadhimisha hata kabla ya kuapishwa kwa upapa wake mnamo tarehe 17 Machi 2013," katika Parokia ya Mtakatifu Anna mjini Vatican, "alihubiri kuhusu mwanamke mzinzi" na "alizungumza kutoka moyoni mwa huruma ya Mungu, kutoka moyoni mwa upendo huu mkuu, wa msamaha na wa usemi wa ukarimu wa Bwana wa huruma." Papa Francisko alitaka kushiriki "roho" hii "na Kanisa lote," Papa Leo XIV alirudia, pia huku akikumbuka "sherehe nzuri ya Jubilei Maalumu ya Huruma."

Zawadi kwa Wote

"Tumwombe kwamba,  tayari anafurahia huruma ya Bwana. Tumshukuru Bwana kwa zawadi kubwa ya maisha ya Papa Francisko kwa Kanisa lote na kwa ulimwengu wote."

Papa Leo XIV akumbuka Papa Francisko

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.

21 Aprili 2026, 13:11