Misa ya kumuombea Papa Francisko baada ya mwaka mmoja wa kifo chake ilifanyika tarehe 21 Aprili 2026. Misa ya kumuombea Papa Francisko baada ya mwaka mmoja wa kifo chake ilifanyika tarehe 21 Aprili 2026.  (ANSA)

Papa Bergoglio,“Mtawa wa Fumbo”na urithi wa neema na utume!

Kumbukumbu ya kwanza ya kifo cha Papa Francisko inaalika kutafakari urithi wake kupitia lenzi ya "Mtawa wa Fumbo,"utegemezi wa Kanisa kwenye nuru ya Kristo.Upapa wake ulisisitiza uongofu wa kimisionari,unyenyekevu na ukuu wa neema katika maisha ya Kanisa.Maono haya yanaendelea leo hii katika mwendelezo wa huduma ya Papa Leo XIV.

Na Sr. Christine Masivo – CPS – Vatican.

Mwaka mmoja baada ya kifo cha Papa Francisko kilichotokea mnamo tarehe 21 Aprili 2025 katika Jumatatu ya Pasaka, kwa Kanisa linatafakari kwa shukrani juu ya upapa uliooneshwa kwa urahisi, kina na bidii ya kiinjili. Ishara yake ya mwisho ya hadharani, ilikuwa baraka ya Pasaka kutokea Dirisha la Basilika ya Mtakatifu Petro, ambayo ilibaki kuwa taswira yenye nguvu ya mchungaji aliyejitoa kikamilifu kwa watu wa Mungu.

Kumkumbuka Padre aliyejikita katika neema

Papa Leo XIV akiendelea na Ziara yake ya Kitume, hata katika nchi za mbali, kumbukumbu hii ilitoa fursa ya kutafakari urithi wa kiroho wa kudumu wa Jorge Mario Bergoglio. Kadri muda unavyopita, mijadala na migawanyiko ambayo mara nyingi iliambatana na huduma yake ilifungua njia ya utambuzi wazi wa ujumbe wake muhimu kwamba, Kanisa haliishi kwa nguvu zake, bali kwa neema ya Kristo.

"Mtawa wa Fumbo" na utambulisho wa Kanisa"

Kitu muhimu katika maono ya Papa Francisko kilikuwa dhana ya kale ya Mtawa wa Fumbo, iliyothaminiwa na Mababa wa Kanisa na mara nyingi aliikumbuka. Picha hii inaelezea Kanisa kama mwezi, ambao hauangazi kwa nuru yake wenyewe bali huakisi nuru ya Kristo, jua. Bila hilo, Kanisa lingebaki gizani. Tangu mwanzo wa upapa wake, Papa Francisko alisisitiza kwamba imani si ya kujizalilisha bali ni zawadi iliyotolewa bure na Kristo. Alionya dhidi ya kujirejea kikanisa, akielezea kama ugonjwa wa kiroho unaotenganisha Kanisa na chanzo chake cha kweli cha uzima. Badala yake, alitoa wito wa kurudi kwa Kristo mara kwa mara, ambaye huifanya upya na kuitegemeza Kanisa kupitia huruma na msamaha. Maono haya ya Taalimungu yaliunda mafundisho yake, mahubiri, na Wosia wake wa Evangelii Gaudium, ambapo alielezea hitaji la mabadiliko ya kimisionari ya Kanisa.

Kanisa zaidi ya kimisionari

Kwa Papa Francisko, utambulisho wa Kanisa kama kielelezo cha Kristo lazima uhusishe wito wa kimisionari. Kwa sababu ni wa Kristo, haliwezi kujitangaza au kujifunga katika miundo yake. Badala yake, lazima liende mbele, likielekeza kwa Bwana Mfufuka kila wakati. Wito huu wa "uongofu wa kimisionari" ukawa uzi unaofafanua huduma yake ya Petro. Ni maono yanayoendelea chini ya Papa Leo XIV, ambaye anahimiza mapokezi mapya ya Evangelii Gaudium kama mwongozo wa utume wa Kanisa wa sasa na ujao. Licha ya tofauti katika mtindo au msisitizo, mwendelezo kati ya mapapa hao wawili ulisisitiza kujitolea kwa pamoja kwa uinjilishaji unaotokana na neema.

Zaidi ya mtu ni shahidi anayemlenga Kristo

Katika maisha yake yote, Papa Francisko alijitenga na umakini wake mwenyewe. Alijielezea kama "mwenye dhambi anayetazamwa na Kristo," alisisitiza kwamba Kanisa hukua si kupitia mikakati ya kibinadamu bali kupitia mvuto wa wazo ambalo mara nyingi alilihusisha na Mtakatifu Agustino na kulirudia kutoka kwa Papa Benedikto XVI. Hata hivyo, hotuba za hadharani mara nyingi zilimfanya awe mtu wa kutengana, akizingatia utu wake badala ya ujumbe wake. Kinyume chake, waaminifu, wakiongozwa na imani yao ya hisia, walitambua kwamba huduma yake ilielekeza zaidi ya yeye mwenyewe kwa Kristo. Mwenendo huu unaonekana hata leo kwenye kaburi lake katika Basilika ya Mtakatifu Maria Mkuu. Mahujaji husimama katika sala, lakini baadaye wao huenda kwenye sanamu ya Bikira Maria, Salus Populi Romani, mpendwa wake sana. Katika ishara hii, urithi wake hupata maana yake ya kweli,  haukujikita kwake mwenyewe, bali unawaongoza wengine kwa Kristo kupitia Maria, katikati ya Kanisa.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.

23 Aprili 2026, 10:17