2026.04.17 Papa atembelea Hospitali ya Mtakatifu Paulo ya Douala. 2026.04.17 Papa atembelea Hospitali ya Mtakatifu Paulo ya Douala.  (@Vatican Media)

Papa atembelea Kituo cha Afya na kutoa faraja kwa wagonjwa

Baada ya Misa,muda wa faragha ulitumika katika baadhi ya wodi za kituo kinachosimamiwa na Jimbo Kuu la Douala na kilichopo wilayani Bassa ambapo Papa alitoa faraja kwa watoto,wanawake na wafanyakazi wanaowatunza wagonjwa katika hali ngumu sana.

Vatican News

Baada ya umati wa watu katika Misa kwenye Uwanja wa Japoma wa Douala, Ijumaa tarehe 17 Aprili 2026, Baba Mtakatifu Leo XIV aliwatembelea wagonjwa katika Hospitali Katoliki ya Mtakatifu Paulo, ambapo aliwapa mabembelezo na faraja. Akifuatana na mkurugenzi wa Hospitali hiyo, alitembelea Wodi kadhaa. Kituo hicho, kinachosimamiwa na Jimbo Kuu la Douala, kiko katika wilaya ya Bassa. Kulikuwa na muda wa kutafakari katika Kikanisa, na Papa Leo XIV, alisimama katika uwanja wa ndani na  kuwasalimia wafanyakazi na baadhi ya wagonjwa kwa ufupi.

Papa alitembelea Kituo cha Wagonjwa
Papa alitembelea Kituo cha Wagonjwa   (@Vatican Media)

Ishara ya Faraja

“Kila siku, bila usumbufu, tunajitahidi kutoa huduma ya afya inayopatikana kwa urahisi na ubora. Uangalifu maalum hutolewa kwa wanawake,” alisema Mkurugenzi wa Kituo hicho. Baadhi ya wagonjwa hao  waliweza kumpatia  mkono Baba Mtakatifu, ambaye, kwa huruma isiyo na kikomo, alikubali mateso ya watoto na watu wazima. Baraka zake zilitolewa kwa kila mtu, ikiwa ni pamoja na wanafamilia waliokuwepo, kabla ya kumsalimia kila mgonjwa mmoja mmoja.

Wakati wa sala ya Malkia wa Mbingu
Wakati wa sala ya Malkia wa Mbingu   (@Vatican Media)

Majeraha ya Nafsi na Mwili

Baada ya Sala ya Malkia wa Mbingu, Baba Mtakatifu  Leo XIV aliweza kuingia vyumba ambavyo baadhi ya wagonjwa wanatunzwa. Alikaribia watoto na wazee. Mwishoni mwa ziara hiyo, muda mfupi kabla ya saa 8 alasiri  saa  zahuko, Papa Leo XIV aliondoka kwenda uwanja wa ndege kwa ajili ya kurudi kwake Yaounde, ambapo alitakiwa kukutana na wanafunzi na wasomi wa  Chuo Kikuu Katoliki cha Afrika ya Kati. Kwa hivyo “uwepo wa Mrithi unagusa majeraha ya vita na yale ya mwili, ukificha majeraha makubwa, ukiomba uponyaji kwa roho na mwili.”

Hata watoto wachanga na wazazi wao
Hata watoto wachanga na wazazi wao   (@Vatican Media)
Hospitali ya Douala

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.

17 Aprili 2026, 16:48