Patriaki wa i Baghdad ya Wakaladayo Polis III Nona. Patriaki wa i Baghdad ya Wakaladayo Polis III Nona. 

Papa ampatia Ushirika wa Kikanisa Patriaki wa Baghdad ya Wakaldayo

Baada ya ombi kutoka kwa Mkuu wa Kanisa la Kikaldayo Polis III Nona,Papa Leo XIV,katika barua, alikubali kumpatia Ushirika wa Kikanisa,"usemi na kifungo cha ushirika kamili na Kiti cha Kitume, katika huduma ya pamoja ya umoja katika Kanisa na ujenzi wa Mwili wa Kristo."

Vatican News

Baba Mtakatifu Leo XIV  aliandika katika barua ya majibu iliyotolewa Jumanne tarehe 28  Aprili 2026 , na Ofisi ya Vyombo vya Habari ya Vatican akibainisha kuwa "Ni kwa moyo uliojaa furaha kwamba ninawapatia Ushirika wa  Kikanisa." Barua iliyoelekezwa kwa Patriaki wa Baghdad wa Wakaldayo, Polis III Nona, aliyechaguliwa kisheria mnamo tarehe 12 Aprili  2026, mjini Roma na Sinodi ya Maaskofu wa Kanisa lake la kisheria( sui iuris). Patriaki mpya alikuwa amendika  hapo awali kuomba, kwa mujibu wa Kanuni ya  76 § 2 ya Gombo la Kanoni ya Kikanisa ya Mashariki , kuidhinishwa kwa Ushirika wa Kikanisa.

"Kifungo cha ushirika kamili na Kiti cha Kitume"

Papa Leo XIV kwa hiyo katika barua yake anabainisha kuwa “ni usemi na kifungo cha ushirika kamili na Kiti cha Kitume, katika huduma ya pamoja ya umoja katika Kanisa na ujenzi wa Mwili wa Kristo. Ninafurahi kuinua sala za dhati ili wewe mkuu, kama Baba na Kichwa cha Kanisa hili pendwa, uwe na  uangalifu wa kichungaji,” Papa Leo XIV aliongeza wa, “huduma uliyokabidhiwa, kuwaongoza Watu wa Mungu kulingana na Moyo wa Kristo na kuwathibitisha katika imani, matumaini, na upendo.” Papa alimwomba Roho Mtakatifu ili kudumisha utume ambao Patriaki ameitwa kutimiza “ili Kanisa la Wakaldayo, lenye utajiri wa mapokeo yake ya kale ya kitume na liwe na ushuhuda unaong’aa wa mashuhuda wengi na waungamaji, aendelee kufanya tangazo la Injili liwe na matunda,” Papa aliongeza, “akiimarisha ushirika wa kikanisa katika eneo lake na katika wale walio nje ya nchi wanaozidi kukua.”

Salamu kwa Sinodi ya Kanisa la Wakaldayo

Kwa hiyo Papa Leo XIV aliwasalimu Maaskofu ambao ni wajumbe  wa Sinodi, mapadre, watawa wa kiume na kike, waseminari, wagombea wa maisha ya wakfu, na waamini wote walei. Alikumbuka kwamba uchaguzi uliofanyika “siku ambayo liturujia ya Wakaldayo ilikuwa ikiadhimisha mkutano wa Kristo Mfufuka na Mtakatifu Thomaso, ambapo mila na tamaduni hai ya Kanisa hilo inaanzia.” Katika majeraha ya Yesu yanayong’aa, Thomaso alitambua “udhihirisho wa huruma ya Bwana wake.” Hivyo ni tumaini kwamba Mungu atamsindikiza katika huduma ya Patriaki “katika ishara ya imani, ambayo inahitaji ujasiri na uvumilivu kutoka kwa waamini wengi wa jumuiya za Wakaldayo ambao, kama waamini wa kweli, wanakabiliwa na kiburi cha Kanisa na mara nyingi majaribu magumu.”

PAPA PATRIAKI POLIS

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here

28 Aprili 2026, 15:05