Papa abariki jiwe la msingi wa"Kituo cha Moyo-Papa Francisko"cha Hospitali ya Gemelli
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV alikutana na wawakilishi kutoka Chuo Kikuu Katoliki cha Moyo Mtakatifu, Taasisi ya G. Toniolo, Mfuko wa Hospitali ya Agostino Gemelli IRCCS, na Mfuko wa Roma, katika muktadha wa kubariki Jiwe la Msingi wa Kituo cha “Centro Cuore”- Papa Francesco” yaano “Kituo cha Moyo – Papa Francisko,” cha Hospitali hiyo Gemelli Roma, Jumatatu asubuhi tarehe 27 Aprili 2026, katika Ukumbi wa Mikutano wa Jumba la Kitume mjini Vatican. Papa Leo XIV alielezea furaha ya shauku yao ya tukio hilo ya kazi kubwa ya Hospitali ya Gemelli, iliyopewa Jina la Papa Francisko. Kwa maelezo Papa alisema “Jina moyo, lililopewa jengo jipya,” limempatia fursa ya kutoa tafakari fupi.
Kwanza, Papa alisema “tuseme utendaji kazi, ikimaanisha, unawakilisha huduma ya kipekee ya Moyo na Mishipa ya Damu iliyorekebishwa(Cardiovascular Unique Offer ReEngineered).” Hiyo ni, inaonesha, kwa kifupi, kinachofaa kwa haraka, sehemu hiyo ya kijiji kikubwa ambacho ni "Gemelli," mahali ambapo patajikita na kutibu magonjwa ya mfumo wa mishipa ya damu (cardiovascolari.). Papa alisema kuwa wao wanaelezea mtindo mpya ulioandaliwa kwa ajili ya mtu. Ni changamoto kweli ambayo Papa anawatakia mema wawze kukabiliana nayo kwa shauku, kushirikiana na kwa maombi. Lakini kwa neno “ Moyo,” kama kazi yao ya Hospitali, ina maana ya jambo kuu zaidi, kwa sababu iko katika jina lenyewe la Chuo Kikuu ambacho wanatokea cha Kikatoliki cha Moyo Mtakatifu.
Kwa mtazamo huo, Papa alipenda kukumbusha historia yake muhimu ya kipekee. Wakati ilipofika kipindi kilichokuwa kikitarajiwa sana cha utambuzi wa uwepo wa Chuo Kikuu kipya, wengi walimshauri Padre Gemelli hasikiite jina la Moyo Mtakatifu, kwa sababu jina hilo lingeonekana sana kama la kidini. Na mwanzilishi alijiuliza swali hilo kwa uaminifu. Lakini Mwenyeheri Armida Barelli hakuwa na shaka: “ Chuo Kikuu kilikuwa kiwe “cha Moyo Mtakatifu “kwa sababu ni kweli Moyo wa Kristo ulikuwa uonesha “miujiza” ambayo iliwezesha uwezekano wa kazi hiyo. Gemelli alisikiliza mhudumu wake mwaminifu na jina likakubalika hata kwa Mamlaka ya Serikali.
‘Dilexit nos’
Papa Leo XIV kwa hiyo alisema kuwa uchaguzi huo, wa kinabii wa wakati huo, upo hata leo hii, ikiwa tunafikiria kuwa Papa Francisko aliandika katika Waraka wake wa Mwisho Dilexi nos- ambao karibu ni wosia wake; ulijikita juu ya “Upendo wa kibinadamu na moyo wa kimungu wa Yesu Kristo.” Katika sehemu yake ya kwanza, inakubusha antropolojia ya Kikristo, ambayo inahusu moyo kama kiini na ufupisho wa mtu binadamu. Kwa kunukuu hatua moja wapo Papa alisema. Kiungo cha kila mwanadamu, kiini cha ndani kabisa, si kiungo cha roho, bali mtu mzima katika utambulisho wake ambao ni roho na mwili. Papa aliongeza, “yote yako kwenye moyo ambao unaweza kuwa makao ya upendo na sehemu zake zote za kiroho, kiakili na hata kimwili.” Na mwisho ikiwa mtu anatawaliwa na upendo anafikia utambulisho wake binafsi kwa namna kamili na angavu, kwa sababu kila binadamu ameumbwa awali ya yote kwa ajili ya upendo na amefanywa kwa viungo vyake vyote zaidi vya kina kwa ajili ya kupenda na kupendwa (n.21).
Katika sehemu hiyo ya Waraka, Papa Leo XIV aliwaeleza kuwa, wao wanaweza kujikuta katika picha ya msingi na thamani ambayo kwa misingi ya malezi katika Hospitali yao, mafunzo ambayo katika fursa hiyo, kwa urahisi aliwatia moyo kuwa: kwa kadiri Gemelli inavyokua, ndiyo inapaswa kutunza kwa mafunzo ya kibidamu na kikristo kwa wale ambao wanafanya kazi humo. Katika Kiini cha ujumbe wa Waraka wa Dilexi Nos, lakini ni wa kitaalimungu, na kiroho, ukijikita juu ya fumbo la Upendo wa Moyo wa Kristo, Msingi wa kisima cha kuhuisha na kusadia maisha yetu na kazi zetu.
Ndani ya Kanisa kuna mashahuda wa upendo
Kama mwali wa milele, upendo huo uliotoa ndani ya Kanisa idadi kubwa ya mashuhuda wa upendo, hata upendo wa kielimu na kijamii. Miongoni mwa hawa, Papa Leo XIV alisema tunaweza kuwataja, Padre Gemelii, Mwenyeheri Armida Barelli na waanzilishi wengine wengi wa Chuo kikuu Katoliki cha Moyo Mtakatifu. Papa Leo XIV alisisitiza inavyoeleweka jinsi ambavyo Padre Agostino Gemelli kwa muda mrefu alikuwa anatamani kitivo cha madawa, na “tunauhakika kwamba Yeye kutokea juu anaendelea kusindikiza maendeleo kwa namna ya pekee kuanzishwa kwa Kituo cha Moyo.” Kwa hisia hizo, Papa Leo XIV “aliwabariki wote na kwa jiwe la kwanza la jengo jipya, huku akiomba kwa maombezi ya Maria Mtakatifu, Kikao cha Hekima na Afya ya wagonjwa.”
