2026.04.27 Papa Leo XIV na Sarah Mullally, Askofu Mkuu wa Canterbury. 2026.04.27 Papa Leo XIV na Sarah Mullally, Askofu Mkuu wa Canterbury.  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV:Waanglikani na Wakatoliki wajitahidi kushinda tofauti

Akikutana kwa mara ya kwanza na Askofu Mkuu mpya wa Canterbury,Papa Leo XIV alihimiza Wakatoliki na Waanglikani kumtangaza Kristo katika ulimwengu pamoja,wakifanya kazi ili kushinda tofauti na changamoto zozote.Papa alikumbuka mkutano wa miaka 60 iliyopita,kati ya Askofu Mkuu Michael Ramsey na Mtakatifu Paulo VI waliotangaza mazungumzo ya kwanza ya kitaalimgu kati ya Waanglikani na Wakatoliki.

Na Angella Rwezaula–Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV alikutana Jumatatu tarehe 27 Aprili 2026 na Askofu Mkuu wa Canterbury, Uingereza, Mheshimiwa Bi Sarah Mullally, na akasali pamoja naye katika Kanisa la Urbano VIII katika Jumba la Kitume, Vatican. Katika salamu zake, Papa Leo XIV alishirikisha furaha yake ya kumpokea Askofu Mkuu wakati wa kipindi hiki cha Pasaka, akikumbuka mkutano wa kihistoria kati ya Papa Mtakatifu Paulo VI na Askofu Mkuu Michael Ramsey, wa Kianglikani, uliofanyika miaka 60 iliyopita. Pia alielezea shukrani kwa huduma ya Kituo cha Kianglikani jijini  Roma, na kumsalimu Mkurugenzi wa kituo hicho, Askofu Anthony Ball, ambaye anawakilisha Askofu Mkuu wa Canterbury katika mji wa Vatican. Kisha Papa Leo XIV alishirikisha salamu yake ya Pasaka ya amani ya Kristo, ambayo alisema inatoa mwaliko kwa Wakristo wote na amani.

Mkutano wa Papa na Askofu Mkuu wa Kianglikani
Mkutano wa Papa na Askofu Mkuu wa Kianglikani   (@Vatican Media)

Amani ya Aliyefufuka haina silaha

Papa alirudia kusema kuwa "mara nyingi nimetaja kwamba amani ya Bwana aliyefufuka 'haina silaha'. Hii ni kwa sababu Yeye hujibu vurugu na uchokozi kila wakati kwa njia isiyo na silaha, akitualika kufanya vivyo hivyo. Akiendelea Papa alisema “ miongoni mwa Wakristo, migawanyiko hudhoofisha uwezo wetu wa kubeba amani ya Kristo kwa ulimwengu kwa ufanisi. Ikiwa ulimwengu utazingatia mahubiri yetu,kwa hivyo, ni lazima tuwe wa maombi ya kudumu na juhudi zetu za kuondoa vizuizi vyovyote vinavyozuia kutangazwa kwa Injili kwa ufasaha."

Papa na ujumbe kutoka Uingereza
Papa na ujumbe kutoka Uingereza   (@Vatican Media)

Mazungumzo ya Kitaalimungu kati ya Wakatoliki na Waanglikani

Papa Leo XIV alikumbuka miongo mingi ya juhudi za mazungumzo ya kitaalimungu, kati ya Wakatoliki na Waanglikani ambazo zimefanywa katika njia ya kurejesha ushirika kamili katika imani na maisha ya kisakramenti. Licha ya ugumu wake, safari hii ya kiekumeni imezaa matunda kuhusu masuala mbalimbali ya kihistoria yenye mgawanyiko, akibainisha kuwa Usharika wa Kianglikani kwa sasa unakabiliwa na maswali mengi kama haya ya wakati huu. Hata hivyo, hatupaswi kuruhusu changamoto hizi zinazoendelea kutuzuia kutumia kila fursa inayowezekana kumtangaza Kristo kwa ulimwengu pamoja."

Wakati wa kubadilishana zawadi
Wakati wa kubadilishana zawadi   (@Vatican Media)

Ni kashifa kuwa na migawanyiko kati yetu

Katika kukumbuka maneno ya Papa Francisko mnamo Mei 2024, kwa Mkuu wa Usharika wa Kianglikani Papa alisema,"itakuwa kashfa ikiwa, kutokana na mgawanyiko wetu, hatutatimiza wito wetu wa pamoja wa kumjulisha Kristo. Kwa upande wangu,naongeza kwamba pia itakuwa kashfa ikiwa hatutaendelea kufanya kazi ili kushinda tofauti zetu, bila kujali jinsi zinavyoonekana kuwa ngumu." Akihitimisha hotuba yake, Papa Leo XIV alimshukuru Askofu Mkuu Mullally kwa ziara yake na akaomba kwamba Waanglikani na Wakatoliki waendelee kutembea pamoja katika urafiki na mazungumzo, wakiongozwa na Roho Mtakatifu, alisema Papa Leo XIV.

PAPA NA ASKOFU MKUU SARAH M.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here

27 Aprili 2026, 14:45