Colosseum,Papa Leo XIV:Mungu wa huruma katika taabu zetu,utujalie upendo wako!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV amekuwa Papa wa pili kubeba Msalaba katika Ibada ya Njia ya Msalaba kupitia vituo vyote 14 katika magofu ya jengo la kale la Kirumi lililowashwa na mishumaa. Uwanja huo ulioshuhudia mauaji ya Wakristo wengi wakitetea imani yao. Kwa njia hiyo usiku wa Ijumaa Kuu Takatifu, tarehe 3 Aprili 2026, kama utamaduni, uliwaona waamini wapatao 30,000 wakiwa ni wazazi na watoto wao, wavulana na wasichana, mapadrei na watawa, wa kike na kiume na mahujaji kutoka sehemu mbalimbali wakijazana katika nafasi zilizotengwa maalum kwa ajili ya tukio hili, lakini pia na watu wengi wasiohesabika ulimwenguni kupitia mitandao ya kijamii, televisheni, na radio wakifuatilia ibada hii muhimu katika historia ya Maisha ya Kikristo.
Uwanja huo ulioanzishwa na Mfalme Vespasian na kukamilika mwaka 80 BK na Mfalme Tito, ni ukumbi mkubwa zaidi wa kale wa mviringo hatimaye uliwekwa wakfu kama wa Kanisa Katoliki. Kila mwaka, Papa na waamini wa Roma na kutoka nje ya nchi hukusanyika katika Colosseum ili kufanya hija ya kiroho kupitia Vituo kumi na vinne vya njia ya Msalaba vinavyokumbusha mateso, kifo na maziko na ufufuko wa Yesu.
Baba Mtakatifu Leo XIV kwa njia hiyo amefuata nyayo za Papa Mtakatifu Yohane Paulo II, ambaye alibeba Msalaba kama huo kuanzia 1980 hadi 1994. Baada ya njia ya Msalaba, ambayo iliongozwa na tafakari iliyoandaliwa na Padre Francesco Patton(OFM), Ndugu Mdogo na Msimamzi wa zamani wa Nchi Takatifu, ambaye alitafakari kwa kina ulimwengu wa leo hii katika safari ya Yesu kwenda Golgotha.
Sala ya Mtakatifu Francis wa Assisi, ilifunga ambayo ni Barua kwa Shirika lale lote la Kifransiskani ambapo Papa aliomba: “Mwishoni mwa Njia hii ya Msalaba, hebu tufanye maombi yetu ambayo Mtakatifu Francis anatualika kuishi maisha yetu kama safari ya kujihusisha kimaendeleo katika uhusiano wa upendo unaowaunganisha Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu.”
Kisha Papa alisali: “Mungu Mwenyezi, wa milele, mwenye haki, na mwenye rehema, utujalie, katika taabu zetu, kufanya, kwa ajili ya upendo wako, kile tunachojua unataka, na kutamani kila wakati kile kinachokupendeza, ili tukiwa tumetakaswa ndani, tukiwa tumeangaziwa ndani na kuwashwa na moto wa Roho Mtakatifu, tuweze kufuata nyayo za Mwanao mpendwa, Bwana wetu Yesu Kristo, na kwa neema yako pekee, tuje kwako. Ee Uliye Juu Zaidi, ambaye katika Utatu Mkamilifu na Umoja rahisi unaishi na kutawala na kutukuzwa, Mungu Mwenyezi, milele na milele. Amina”(rej kifungu cha 50-52: FF 233).
Papa Leo XIV alihitimisha na Baraka ya kizamani ya kibiblia kutoka kitabu cha (Hes 6,24-26),) ambayo Mtakatifu Francis alikuwa akiwabariki watawa na watu wote, hata ikawa baraka "yake" (FF 262).
Bwana nanyi Bwana
℟. Na roho mwako
Bwana akubariki na kukulinda.
℟. Amina.
Akuangazie uso wake na kukufadhili.
℟. Amina.
Akuinue uso wake na kukupa amani yake.
℟. Amina.
Na bara ya Mungu Mwenyezi
E la benedizione di Dio onnipotente,
Baba ✠ na Mwana ✠ na Roho ✠ Mtakatifu
Iwashukie na kukaa nanyi daima.
℟. Amina.
