Papa Leo XIV wakati wa sala kwa ajili ya zawadi ya amani Aprili 11,2026 Papa Leo XIV wakati wa sala kwa ajili ya zawadi ya amani Aprili 11,2026  (@Vatican Media) Tahariri

Mapapa na vita katika enzi za kisasa

Mbele ya kukabiliwa na nguvu ya uharibifu unaotokana na silaha za kisasa ni vigumu sana kusema,kama ilivyofanyika katika karne zilizopita,kuhusu uwezekano wa"vita ya haki."Tayari mnamo 1963,Papa Yohane XXIII,katika Waraka wa Pacem in Terris,aliandika:"katika enzi ya atomiki ni vigumu kufikiria vita kama chombo cha haki."Papa Leo XIV anaendeleza njia hiyo kwa kufanya amani kuwa moja ya mada kuu za upapa wake.Ni katika tahariri ya Mwariri Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano.

Andrea Tornielli

Tunaporudi kwenye mada ya "vita vya haki," inafaa kukumbuka mafundisho ya amani kutoka kwa Mapapa waliofuatana kwenye Kiti cha Petro katika miaka mia moja iliyopita. Mafundisho ambayo yameimarika na kuzidi kuwa ya kina, na kufikia hatua ya kufafanua uwezekano wa "vita vya haki" kuwa magumu zaidi. Tafakari kuhusu taalimungu ya karne zilizopita na uhalalishaji unaowezekana wa vita hushindwa kuzingatia ukweli kwamba Wataalimungu wa zamani walipoandika kuhusu mada hizi, vita vilifanyika kwa mapanga na marungu na si kwa vifaa vya kulipuka vyenye hatari na ndege zisizo na rubani zinazoongozwa na mashine, jambo linaloibua maswali ya kimaadili yenye nguvu kubwa. Hakika, kuna ufahamu unaoongezeka kwamba vita si chaguo linalowezekana.

Kutoka katika barua ya Papa Benedikto XV ya mwaka 1917 kwa wapiganaji,  ikiita Vita vya Kwanza vya Dunia kama "mauaji yasiyo na maana" hadi majaribio ya Papa Pio XII ya kuzuia kuzuka kwa Vita vya Pili vya Dunia; kutoka kwa maneno ya Papa Yohane  XXIII katika Waraka wa Kitume wa "Pacem in Terris," ambaye mapema mwaka 1963 aliandika kwamba "ni vigumu kufikiria kwamba katika enzi ya atomiki vita vinaweza kutumika kama chombo cha haki." Kuanzia kilio cha Paulo VI katika  Umoja wa Mataifa cha "vita havitarudiwa" hadi majaribio yasiyotiliwa maanani ya Papa Yohane Paulo II ya kuzuia migogoro mibaya katika Mashariki ya Kati; Warithi wa Mtume  Petro hawajashindwa kupaza sauti zao, zikiwa na unabii na uhalisia, ambao, kwa bahati mbaya, mara nyingi haujasikika.

Maandishi ya marejeo, kwanza kabisa, ni Katekisimu ya Kanisa Katoliki,(KKK) ambayo inazingatia haki ya ulinzi halali lakini pia inaweka "masharti makali" kwenye vita vya kujilinda: “Wakati huo huo, ni muhimu: ​​kwamba uharibifu unaosababishwa na mchokozi kwa taifa au jamii ya mataifa uwe wa kudumu, mkubwa, na wa uhakika; kwamba njia zingine zote za kuumaliza zimethibitika kuwa haziwezekani au hazina ufanisi; kwamba kuna masharti ya msingi ya kufanikiwa; na kwamba kukimbilia na silaha hakusababishi maovu na matatizo makubwa zaidi kuliko uovu kuondolewa.

Katika kutathmini hali hii, nguvu ya njia za kisasa za uharibifu ina jukumu muhimu sana. Nani anaweza kukataa kwamba ubinadamu leo ​​umesimama ukingoni mwa shimo kwa sababu hasa ya kuongezeka kwa migogoro na nguvu ya "njia za kisasa za uharibifu"? "Hakuna" kwa vita ilirudiwa kwa nguvu inayoongezeka hata wakati wa upapa wa Papa Francisko, ambaye aliandika katika waraka wake wa  "Fratelli Tutti:" "Ni rahisi kuchagua vita kwa kuendeleza kila aina ya visingizio vinavyoonekana kuwa vya kibinadamu, vya kujilinda, au vya kuzuia, hata kutumia udanganyifu wa taarifa. Kiukweli, katika miongo ya hivi karibuni, vita vyote vimedai kuwa na 'uhalali' (...) Tatizo ni kwamba, kuanzia na maendeleo ya silaha za nyuklia, kemikali, na kibiolojia, na uwezekano mkubwa na unaoongezeka unaotolewa na teknolojia mpya, vita vimepewa nguvu ya uharibifu isiyodhibitiwa, inayoathiri raia wengi wasio na hatia.

Kiukweli, 'binadamu haijawahi kuwa na nguvu nyingi juu yake, na hakuna kinachohakikisha kwamba itaitumia vizuri.' Kwa hivyo, hatuwezi tena kufikiria vita kama suluhisho, kwani hatari zinaweza kuzidi matumizi ya kinadharia yanayohusishwa nayo. Akikabiliwa na ukweli huu, ni vigumu sana leo hii kudumisha vigezo vya busara vilivyotengenezwa katika karne zilizopita kuzungumzia uwezekano wa 'vita vya haki.' Vita visirudiwe tena! Mrithi wake, Papa Leo XIV, alifanya amani kuwa moja ya mada kuu za upapa wake: akikabiliwa na wazimu  wa kuongezeka kwa vita na matumizi yasiyo ya kawaida ya silaha, alifuata kwa uhalisia sawa na kutabiri njia ambayo tayari ilitengenezwa na watangulizi wake, huku akitoa wito wa amani, mazungumzo, na maridhiano

Mauaji ya raia yaliyofanywa katika miaka ya hivi karibuni yametikisa dhamiri za mabilioni ya watu ulimwenguni kote, ambao wanamtazama Askofu wa Roma. Papa Leo, kama Yesu alivyofanya huko Gethsemane, anahimiza kwa nguvu turudishe panga zetu kwenye ala: "Kila mahali tunasikia vitisho badala ya wito wa kusikiliza na kukutana nao," alisema wakati wa Mkesha wa Maombi Jumamosi, tarehe 11 Aprili 2026. Alieleza kwamba "wale wanaoomba wanajua mapungufu yao wenyewe; na hawaui na hawatishii kifo. Kwa upande mwingine, wale ambao wamemgeuzia Mungu aliye hai kisogo wamekuwa  watumwa wa kifo, wakijifanya wao wenyewe na nguvu zao kuwa sanamu bubu, kipofu, na kiziwi, ambao wanajitolea kila thamani na kudai kwamba ulimwengu mzima upige goti. Inatosha kwa ibada ya sanamu ya nafsi na pesa! Inatosha kwa kuonesha nguvu! Inatosha kwa vita! Nguvu ya kweli inadhihirishwa katika kutumikia maisha."

Papa akihutubia Taifa la Cameroon
Papa akihutubia Taifa la Cameroon   (@Vatican Media)
Hotuba ya Papa kwa Mamlaka na asasi za kiraia na wanadiplomasia huko Cameroon

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here

15 Aprili 2026, 19:40