Cameroon wanamsubiri Papa Leo XIV,changamoto na utajiri,nchi itafutayo umoja
Na Francesca Sabatinelli - Yaoundé.
Nchi changa, ya Cameroon yenye utajiri wa mila na tamaduni, yenye sifa ya hisia kali ya jamii miongoni mwa raia wake, lakini pia iliyo na mzozo mkubwa wa kiuchumi, kutokuwa na utulivu wa kisiasa, na vurugu zilizosababishwa na muongo mmoja wa mapigano kati ya jeshi na vikundi vya kujitenga vya Kanda ya Kiingereza kaskazini magharibi na kusini magharibi, na vurugu zilizofanywa na Boko Haram kaskazini, inayopakana na Nigeria. Cameroon ambayo inajionesha kwa Baba Mtakatifu Leo XIV katika ziara yake ya nne ya Papa nchini, kufuatia na ya Watangulizi wake Mtakatifu Yohane Paulo II kunako mwaka 1985 na 1995, na Papa Benedikto XVI mwaka 2009, inataka zaidi ya yote kuonesha hadhi yake kama "muhamasishaji wa amani," mwenye uwezo wa "imani na upatanisho wa mioyo," mwenye uwezo wa "kuponya mataifa." Huu ni ujumbe unaotolewa na mabango yanayomkaribisha Papa Leo XIV ambayo yamepamba mji mkuu wa nchi hiyo huko Yaoundé, yakimkaribisha kutoka Algeria kama ishara ya hamu ya kweli ya nchi hiyo ya kushinda migawanyiko na mivutano. Shauku inayowaunganisha kila mtu, si tu ya wale walio katika maeneo yanayokumbwa na vurugu, kwa sababu watu wa Cameroon, kama kila mtu anavyosema, "ni watu wamoja."
Kukutana na Watu
Kwa mujibu wa Maelezo ya Padre Luca Galimberti, mmisionari wa PIME huko Yaoundé, akizungumza na mwandishi wetu wa Vatican news aliyeko huko Francesca Sabattinelli, katika fursa ya Ziara ya Kitume, alibainisha kuwa " Papa anawapata vijana, ua la uzima wakitafuta njia. Hii ndiyo sababu mkutano kati yake na watu utakuwa mzuri, mkutano wa matamanio, wa matarajio," lakini pia wa ugumu wa maisha ya vijana wengi, ambao, wakiwa na nafasi ndogo au bila nafasi ya kupata kazi, wanaendelea kuwa na matumaini yasiyowezekana ya kuondoka Cameroon, ya kwenda nje ya nchi.
Pia idadi hiyo inazingatia idadi kubwa sana, takriban 500,000, ya wakimbizi na wanaotafuta hifadhi kutoka nchi jirani, kama vile Sudan na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na hivyo kusababisha hali ngumu na muhimu ya kijamii. Pia, mvutano unaochochea ni upande mkubwa wa ukabila ambao, pamoja na ukosefu wa usalama na kutokuwa na uhakika kuhusu mustakabali, "husukuma kila mtu kupigania maisha yake", pia huleta nguvu ambazo "zinaweza kuwa chanzo cha mgawanyiko".
Amani inayosubiriwa kwa muda mrefu
Ziara ya Papa ni muhimu kwa wale wote wanaohisi wameachwa: watoto wa Kituo cha Yatima cha Ngul Zamba huko Yaundé au wagonjwa wa Hospitali ya Katoliki ya Mtakatifu Paulo huko Douala. "Papa atawapatia tumaini na furaha,"alielezea Padre Charles Marie Houngbo, Mfransiskani wa Moyo Safi wa Maria wa Parokia ya Pentekoste huko Newtown katika Uwanja wa Ndege na Askofu Mkuu wa Eneo la Kichungaji la Wouri VI katika Jimbo Kuu la Douala
"Ziara yake katika maeneo haya ni ukumbusho, akiwapatia changamoto mamlaka, za kiraia na za kidini, kuelewa kwamba lazima wafikirie ustawi wa wale wanaoteseka." Uchaguzi wa rais wa Oktoba uliopita, ambao ulithibitisha Rais Paul Biya kwa muhula wa nane, ulisababisha mvutano mkubwa nchini kutokana na matarajio yasiyotimizwa ya wengi. Maandamano hayo, ambayo hayakuwahi kusababisha mapigano ya kutumia silaha, hata hivyo yalikandamizwa sana, na kusababisha idadi kubwa ya majeruhi. Kukatishwa tamaa bado kunabaki, Padre Galimberti aliendelea kusema, "kwa sababu kulikuwa na matarajio mengi kwa mustakabali ambao, hata hivyo, haujafika mwisho. Mipango hiyo haiahidi, kwa hivyo watu wamekata tamaa na ndiyo maana mvutano unaibuka. Tunahitaji kuisaidia Cameroon kufikia mwendelezo wa amani, amani hiyo iliyosubiriwa kwa muda mrefu."
Kitendo cha Kanisa
Kanisa kijana Katoliki la hapa, ambalo utume wake uliingia nchini mwaka 1890 kutokana na kazi ya Wamisionari Wapallottini wa Ujerumani, leo hii linachukuliwa kwa usahihi kama nguzo ya jamii, nguvu inayoendesha mazungumzo kati ya majimbo mbalimbali ya kikanisa, mpatanishi muhimu katika nyanja ya kijamii, na msaidizi aliyeazimia wale wanaoteseka kutokana na vurugu za migogoro ya ndani. Pia lina sifa ya upanuzi mkubwa wa idadi, unaoambatana na ukuaji mkubwa wa waamini katika harakati zao za kutafuta haki ya kijamii na uthabiti wa taasisi za kiraia. Wakati wa ziara ya Papa Leo XIV, Kanisa litamwonesha Papa kazi muhimu ya umoja inayofanywa, inayothibitishwa na mkutano wa Papa na waamini ambao, licha ya tofauti zao katika lugha na uhusiano wa kikabila, watashiriki katika mkutano na Papa Leo XIV, wote kwa furaha ile ile, kwa heshima na uelewa."
![]()
Tangazo la makaribisho.
Ziara ya Papa Leo XIV
Papa Prevost atatembelea miji mitatu: pamoja na mji mkuu wa Yaoundé, atatembelea Bamenda, kitovu cha mgogoro wa Kanda ya Kiingereza, na Douala, bandari kubwa kwenye Ghuba ya Guinea na mji mkuu wa kibiashara wa nchi hiyo. Matarajio makubwa yanalenga hasa ujumbe ambao Papa ataupeleka kwa Bamenda, eneo la Kanda ya Kiingereza iliyomezwa na vurugu, ikishuhudia mapigano kati ya vikosi vya kijeshi na vikundi vya kujitenga vilivyojihami vinavyofanya kazi ili kukabiliana na kile kinachoonekana kama kutengwa kwao na serikali kuu ya Kifaransa. Maneno ya Papa huko Bamenda yanaweza kuwa na "matokeo makubwa," alielezea Padre Luca. "Uwepo wake utakuwa baraka mahali ambapo mvutano na mateso yanaonekana, na zaidi ya yote, inatumainiwa, inaweza kuwa kichocheo cha kuanza tena kwa mazungumzo." Kila mtu anatumaini kwamba Papa Leo XIV, huko Bamenda, anaweza kuwa sauti ya mateso ya watu waliosahaulika, kwamba kwa ujumbe wake unaweza kuwahimiza kila mtu kugundua upya utambulisho wao wa pamoja, zaidi ya mgawanyiko wa kisiasa na kikabila.
![]()
Ndani ya Kanisa Kuu la Youndé
Makubaliano ya kusitisha vita huko Bamenda
Wito wa Papa Leo XIV huko Bamenda, Padre Charles anaonesha, utakuwa wa amani, unaoelekezwa kwa vijana wote "ambao wana silaha mikononi mwao, kuweka bunduki zao chini, kufikiria njia tofauti ya kutatua suala hilo. Na pia ni wito kwetu sote, unaotuomba tuombe, lakini pia kuwasiliana, kuzungumza na watu na mamlaka. Ni wito wa kuwaleta Wacameroon wote pamoja, kuishi kama kitu kimoja. Tunafurahi kumkaribisha Papa, na matumaini yetu ni kwamba, baada ya kuondoka kwake, ujumbe huu utabaki, ujumbe ambao utawasukuma mamlaka, raia wote, kuelewa kwamba mabadiliko yanahitajika. Tunasubiri mabadiliko haya na maisha mapya kwa Wacameroon wote." Wakati huo huo, waliojetenga wa Kanda ya Kiingereza wametangaza kufanya makubaliano ya amani wakati wa ziara ya Papa Leo XIV katika eneo hilo. Tangazo hilo lilitolewa na Muungano wa Umoja, jukwaa linalowakutanisha makundi mbalimbali, likionesha kwamba hatua hiyo, ambayo itadumu kwa siku tatu, itachukuliwa kwa kutambua "umuhimu mkubwa wa kiroho" wa ziara ya Papa.
Kurudia tena kwa migogoro
Maisha ya wakazi wa maeneo yaliyoathiriwa na migogoro na shughuli za kigaidi za Boko Haram yanashikiliwa mateka na vurugu, na hapa pia jukumu muhimu la Kanisa linahusika, mwezeshaji wa kukutana na maridhiano, ambaye hatua yake inategemea hasa uwezo wa kudumisha umoja na kuhamasisha ushirikiano na uwajibikaji miongoni mwa raia. Mfano wa hili ulikuwa ni kujitolea kwa Kanisa, kabla ya uchaguzi, kwa kampeni kubwa ya kuwaita watu kupiga kura na kujiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura, ikisisitiza umuhimu wa kupiga kura kama uwezekano wa mabadiliko. "Kanisa," aliongeza Padre Galimberti, "limekuwa chanzo cha mwongozo na ufahamu kwa watu, ili ubinadamu uweze kujidhihirisha katika udugu na haki ambayo kila mtu anadai." Lakini njia ya kusonga mbele nchini Cameroon inabaki kuwa ngumu. Hatima ya nchi "haiko mikononi mwa Kanisa," licha ya hatua yake kubwa, na ukuaji wake wa kiuchumi unabaki kuhusishwa bila kutenganishwa na maendeleo ya kimataifa na athari za migogoro mikubwa inayoendelea katika nchi kadhaa. Kipengele kimoja kinachoitambulisha nchi, kama ilivyo kwa Ulimwengu wote, ni ongezeko la matumizi ya silaha, ambalo linashuhudia kucheleweshwa kwa "fedha kubwa kutoka kwa usimamizi wa kawaida wa nchi ambayo tayari inakabiliwa na mateso."
![]()
Youndé, Kituo cha watoto Yatima atakachotembelea Papa Leo XIV huko Ngul Zamba
Ushuhuda wa upendo
Matokeo ya migogoro ya kimataifa, kama ilivyo katika nchi zingine za Afrika, pia zinaonekana kwa nguvu nchini Cameroon, ambapo kupunguzwa kwa misaada ya maendeleo kutoka nchi zenye kipato cha juu kumesababisha kufungwa kwa mipango mingi ya kibinadamu na kupungua kwa kasi kwa ushirikiano na mashirika ya kimataifa. Hapa pia, kazi ya Kanisa mahalia hapo lililoimarika vizuri linabaki kuwa muhimu. Inamsubiri Papa, Padre Luca anaendelea, "kushiriki uzoefu na kushuhudia kwa furaha kitendo hicho katika nchi ambayo imani iko hai na ipo. Kanisa lenye jukumu la kutoa ushuhuda kwa Yesu na nguvu zake, ambalo hubadilisha mahusiano na kuruhusu uhuru wa moyo. Kanisa linaishi mwilini mwa watu hawa, ambao mateso yao mara nyingi hupuuzwa." Wazo, Padre Galimberti alihitimisha, ni kuzingatia kila wakati mambo muhimu, kuongozana na watu katika kuishi imani yao kama Bwana anavyoomba, kama ushuhuda wa maisha ya kidugu na upendo kwa maskini zaidi. Hili halipaswi kusahaulika kamwe na hivi ndivyo Kanisa nchini Cameroon linavyoendelea kufanya."
Sasisho la mwisho saa 7.00 , Jumatano 15 Aprili na Angella Rwezaula
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.
