Vikosi vya Israeli vyaongeza uwepo wake kando ya mpaka na Lebanon. Vikosi vya Israeli vyaongeza uwepo wake kando ya mpaka na Lebanon.  (ANSA)

Papa atoa wito wa kusitisha mapigano huko Mashariki ya Kati

"Kwa niaba ya Wakristo wa Mashariki ya Kati na wanaume na wanawake wote wenye mapenzi mema,ninawaelekea wale waliohusika na mgogoro huu:sitishenimoto! Njia za mazungumzo zifunguliwe tena!Vurugu haziwezi kamwe kusababisha haki,utulivu na amani ambayo watu wanaisubiri."Ni wito wa Papa Leo XIV mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana,Machi 15,akieleza mateso ya watu wa Mashariki ya kati kutokana na vita.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana, Baba Mtakatifu Leo XIV, Dominika tarehe 15 Machi 2026 akiwa katika Dirisha la Jumba la Kitume alisema: “Kwa majima mawili, watu wa Mashariki ya Kati wamepitia vurugu kali za vita. Maelfu ya watu wasio na hatia wameuawa, na wengine wengi wamelazimika kukimbia makwao. Ninarudia kuonesha ukaribu wangu wa maombi kwa wale wote waliopoteza wapendwa wao katika mashambulizi ambayo yameathiri shule, hospitali, na maeneo ya makazi."

Papa Leo XIV aidha aliendelea kusema: "Hali nchini Lebanon ni jambo la wasiwasi mkubwa. Nanatumaini njia za mazungumzo ambazo zinaweza kusaidia mamlaka ya nchi hiyo katika kutekeleza suluhisho za kudumu kwa mgogoro mkubwa unaoendelea, kwa manufaa ya wote wa Lebanon."

Wito mkali wa Papa Leo XIV

Baba Mtakatifu alisema "Kwa niaba ya Wakristo wa Mashariki ya Kati na wanaume na wanawake wote wenye mapenzi mema, ninawaelekea wale waliohusika na mgogoro huu: Sitisheni moto! Njia za mazungumzo zifunguliwe tena! Vurugu haziwezi kamwe kusababisha haki, utulivu, na amani ambayo watu wanaisubiri."

Salamu kwa mahujaji

Papa Leo alendelea na salamu zake: "Ninawakaribisha nyote, mliopo leo katika Uwanja wa Mtakatifu Petro! Ninawasalimu waamini kutoka Valencia na Barcelona nchini Hispania, pamoja na wale kutoka Palermo. Ninawakaribisha kwa furaha makundi kadhaa ya vijana wanaojiandaa kupokea Sakramenti ya Kipaimara: kutoka Berceto,Jimbo la Parma; kutoka Tuto, Jimbo la Firenze; kutoka Torre Maina na Gorzano, Majimbo ya Modena-Nonantola. Pia ninawasalimu vijana wa Parokia ya Mtakatifu  Gregorio Mkuu, Roma na vijana wa Capriano del Colle na Azzano Mella, Jimbo la  Brescia. Ninawatakia kila mtu Dominika njema," alihitimisha Papa Leo XIV.

WITO WA PAPA WA KUSITISHWA MOTO

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku bonyeza hapa: Just click here.

15 Machi 2026, 13:48