2025.11.21 Incontro Digitale di Papa Leone XIV con i Giovani americani

Uchungu wa Papa kwa ajili ya watoto wasio na hatia na waathirika wa Mashariki ya Kati

Ofisi ya Habari ya Vatican,kupitia chaneli yake ya Telegram,ilitangaza kwamba Papa Leo XIV anaomba mwisho wa uhasama wote Mashariki ya Kati.Mawazo ya Papa yapo kwa"watu wengi wasio na hatia,wakiwemo watoto wengi"waliouawa katika mabomu na"wale waliowasaidia,"kama vile Padre Pierre El-Rahi,Padre Mmaronite aliyefariki Machi 9 katika shambulio nchini Lebanon.

Vatican News

Papa Leo XIV alionesha "huzuni kubwa" "kwa wahanga wote wa mabomu katika siku za hivi karibuni Mashariki ya Kati, kwa watu wengi wasio na hatia, wakiwemo watoto wengi, na kwa wale waliowasaidia, kama vile Padre Pierre El Raii." Huyu ndiye Padre Mmaronite aliyeuawa alasiri ya tarehe 9 Machi 2026 huko Qlaya wakati wa shambulio lililopiga nyumba karibu na parokia yake, milimani, na kumjeruhi mmoja wa waamini wa parokia hiyo.

Kama  vile Padre Toufic Bou Merhi(OFM) alivyo viambia vyombo vya habari vya Vatican, Padre Pierre alikimbia na vijana wengine kadhaa kumsaidia muumini wa parokia hiyo. Wakati huo, bomu lingine lilitokea kwenye nyumba hiyo hiyo, na Padre huyo akajeruhiwa na walimkimbiza hospitali ya eneo hilo, akafariki kabla ya matibabu.

Mawazo ya huzuni ya Papa yaliyotolewa kupitia chaneli ya Telegram ya Ofisi ya Habari ya Kiti Kitakatifu, yanamwendea yeye na wale wote waliopoteza maisha yao katika mashambulizi ya hivi karibuni Mashariki ya Kati. Watoto kwanza kabisa.

Kulingana na mashirika ya watoto kama vile UNICEF na Save the Children, takriban watoto 300 wameuawa tangu kuongezeka kwa mapigano.  Taarifa ya Vatican inasema Papa Leo XIV, "anafuatilia matukio hayo kwa wasiwasi na anaomba kusitishwa haraka kwa uhasama wote."

Asante kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here.

10 Machi 2026, 09:44