Vita vinavyoendelea huko Lebano Vita vinavyoendelea huko Lebano  (ANSA)

Papa Leo XIV:Mkristo anaalikwa kuwa chombo cha amani,upendo na maridhiano

Katika salamu zake mara baada ya tafakari ya katekesi katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican Papa Leo XIV alirudia wito wake wa amani kutawala miongoni mwa watu wote.Akiwasalimia hasa waamini kutoka Mashariki ya Kati aliwahimiza kuwa vyombo vya upatanisho."Wakristo wameitwa kuwa vyombo vya amani,upendo na upatanisho."Kwa wanaouzungumza Kiitaliano amekumbuka sherehe ya Mlinzi Mtakatifu Yosefu inayoadhimishwa Machi 19.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV, mara baada ya Katekesi  tarehe 18 Machi 2026 kwa waamini na mahujaji waliokusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, alifikiria hasa Mashariki ya Kati, kama alivyofanya Dominika iliyopita, ya tarehe 15 Machi,  baada ya sala ya Malaika wa Bwana. Kisha alielezea wasiwasi wake mkubwa kuhusu "vurugu kali za vita" zinazosababisha maelfu ya wahanga wasio na hatia katika eneo hilo.

Amani upendo na upatanisho

Baba Mtakatifu, katika salamu zake kwa waamini kwa Kiarabu, alirejea wito huo akiwaalika Wakristo kueneza amani: “Ninawasalimu waamini wanaozungumza Kiarabu, hasa wale kutoka Mashariki ya Kati. Wakristo wameitwa kuwa vyombo vya amani, upendo, na upatanisho, ili amani ya kweli iweze kutawala miongoni mwa watu wote. Bwana awabariki nyote na awalinde daima kutokana na uovu wote!”

Maisha yaliyoongozwa na maadili ya Kikristo

Na mwaliko wa kuwa wapatanishi ulirudiwa na Papa katika salamu zake kwa waamini wa Kichina: “Ninatoa salamu zangu za dhati kwa watu wanaozungumza Kichina. Kaka na dada wapendwa, endeleeni kuishi maisha yaliyoongozwa na maadili ya Kikristo ili kuwa vyombo vya amani katika jamii."

Kwa wanaozungumza Kiitaliano, Papa Leo XIV alisema kuwa: “Ninawakaribisha kwa dhati mahujaji wanaozungumza Kiitaliano, hasa wa Amini kutoka Riva presso Chieri na Rosciano, maafisa wa Ukaguzi wa Usalama wa Umma wa "Palazzo Chigi" huko Roma, wanafunzi wa Shule ya Maafisa Wadogo wa Jeshi la Wanamaji wa Taranto, Kikosi cha Msaada cha Italia cha Shirika la Malta, na Kiwanda cha Fiasconaro huko Castelbuono.

Sherehe ya Mtakatifu Yosefu

Mawazo yake hatimaye aliwageukia wagonjwa, wenye ndoa wapya, na vijana, hasa wale walio katika Shule ya Kristo Mfalme jijini Roma, Taasisi ya Mtakatifu Giorgio huko Pavia. Kwa wote aliwakadhi mawazo yake na matashi mema kwa kila mmoja ya Mtakatifu Yosefu, Mlinzi wa Mbinguni wa Kanisa la Ulimwengu, ambaye tutaadhimisha sherehe yake ya kiliturujia tarehe 19 Machi 2026.

Baada ya Ktekesi wito wa amani

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku bonyeza hapa: Just click here.

18 Machi 2026, 12:04