Papa Leo XIV:Mitume wameitwa kulinda na kuhifadhi mafundisho ya Mwalimu yanayookoa!

Katika Katekesi yake Papa Leo XIV kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro,Machi 25,amejikita na mada ya Mfumo wa kihierarkia wa Kanisa,kuanzia na Hati ya Lumen Gentium.Mitume ni nguzo hai za mwili wake wa fumbo katika huduma ya umoja,utume na utakaso wa wajumbe wake wote.Kwa hiyo Maaskofu wako katika huduma ya Watu wa Mungu,walinzi wa hazina ya imani.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

“Lumen Gentium inakumbusha kwa ufanisi mara kwa mara asili ya kiushirika na ya kijumuiya ya utume wa kitume, ikirudia kwamba "Huduma ambayo Bwana amewakabidhi wachungaji wa watu wake ni huduma ya kweli, ambayo katika Maandiko Matakatifu inaitwa kwa kiasi kikubwa 'diakonia,- ushemasi' yaani, huduma" (Lumen Gentium, 24). Haya yamo katika Katekesi ya Baba Mtakatifu Leo XIV kwa mahujaji na waamini waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, wapatao 16,000, Jumatano tarehe 25 Machi 2026, Mama Kanisa akiwa anaadhimisha sherehe ya Kupashwa habari kwa Mama Bikira Maria. 

Ni katika  mwendelezo wa Katekesi za Papa kuhusu Mtaguso wa II wa Vatican, hasa kipengele cha Lumen Gentium, kwa mada “  msingi wa Mitume: Kanisa katika kiwango chake cha kihierarkia, lilisomwa: “Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu. Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni(Efe 2,19-20).

Waamini katika Katekesi ya Papa Leo XIV
Waamini katika Katekesi ya Papa Leo XIV   (@Vatican Media)

Kwa njia hiyo, Baba Mtakatifu Leo XIV alisema kuwa “Tuendelee na Katekesi kuhusu Hati ya Mtaguso wa II wa Vatican, kwa kutafakari Katiba ya kidogma ya Lumen Gentium, kuhusu Kanisa (LG). Baada ya kuwakilisha kama watu wa Mungu, leo tufikirie muundo wake wa Kihierarkia. Kanisa Katoliki linapata msingi wake katika Mitume, waliopendwa na Kristo kama nguzo hai ya Mwili wa fumbo, na ina ukuu wa kihierarkia",ambao unafanya kazi ya huduma ya umoja, ya utume na ya kutakatifuza wajumbe wake.  Utaratibu huu Mtakatifu ni wa kudumu ulio na msingi  wa Mitume (Ef 2,20; Ufu 21,14) ukiwa kama ushuhuda wa juu wa ufufuko wa Yesu(Mdo 1,22; 1Cor 15,7) na waliotumwa kutoka kwa Bwana mwenyewe katika utume Ulimwenguni(Mk 16,15; Mt 28,19).

Kwa kuwa Mitume wameitwa kulinda kwa kuhifadhi kwa uaminifu mafundisho yanayookoa ya Mwalimu (2Tm 1,13-14), wao wanaeneza huduma yao kwa watu ambao hadi kurudi kwa Kristo, wanaendelea kutakatifuza, kuongoza na kujenga Kanisa, shukrani kwa wafuasi wao katika utume wa kichungaji(KKK , 857). Urithi huu wa kitume, ulioanzishwa katika Injili na Mapokeo, unachunguzwa kwa undani zaidi katika Sura ya III ya Lumen Gentium, yenye kichwa: "Katiba ya Kihierarkia ya Kanisa na Hasa ya Uaskofu." Mtaguso unafundisha kwamba muundo wa kihierarkia, si muundo wa kibinadamu, unaohudumia shirika la ndani la Kanisa kama mwili wa kijumuiya (taz. LG, 8), bali ni muundo wa taasisi ya Kimungu inayolenga kuendeleza utume uliotolewa na Kristo kwa Mitume hadi mwisho wa wakati.

Waamini katika Katekesi ya Papa Leo XIV
Waamini katika Katekesi ya Papa Leo XIV   (@Vatican Media)

Papa Leo XIV aliendelea kusisitiza kwamba ikiwa kweli kwamba mada hii inazungumziwa katika sura ya tatu, baada sura mbili za kwanza zikitafakari Kanisa (taz. Acta Synodalia III/1, 209-210), haimaanishi kwamba katiba ya kihierarkia ni kipengele kinachofuata kuhusiana na watu wa Mungu: kama Hati ya  Ad gentes inavyosema, "Mitume walikuwa wakati huo huo mbegu ya Israeli mpya na asili ya uongozi mtakatifu"(n. 5), kama jumuiya ya wale waliokombolewa na Pasaka ya Kristo, iliyoanzishwa kama njia ya wokovu kwa ulimwengu. Ili kuelewa nia ya Mtaguso, ni muhimu kusoma kwa makini kichwa cha sura ya Tatu ya Lumen Gentium, kinachoelezea muundo wa msingi wa Kanisa, uliopokelewa kutoka kwa Mungu Baba kupitia Mwana na kukamilika kwa kumiminwa  kwa Roho Mtakatifu.

Mababa wa Mtaguso hawakutaka kuwasilisha vipengele vya kitaasisi vya Kanisa, kama nomino "katiba" inavyoweza kupendekeza ikiwa itaeleweka kwa maana ya kisasa. Hati hiyo badala yake Papa aliongeza “inazingatia ‘ukuhani wa kihuduma au wa kihierarkia’, ambao hutofautiana "kimsingi na si kwa kiwango tu" na ukuhani wa kawaida wa waamini, ikikumbusha kwamba hawa "wamepangwa kwa kila mmoja, kwani wote wawili, kila mmoja kwa njia yake mwenyewe, wanashiriki katika ukuhani mmoja wa Kristo.” (LG 10).

Katekesi ya Papa Leo XIV
Katekesi ya Papa Leo XIV   (@Vatican Media)

 Kwa hivyo, Mtaguso  Papa Leo XIV aliendelea, unashughulikia huduma inayotolewa kwa wanaume waliopewa daraja Takatifu (sacra potestas) (taz. LG, 18) kwa ajili ya huduma katika Kanisa: linalenga hasa uaskofu (LG, 18-27), kisha kwa Wachungaji  wa Kanisa (LG, 28) na ushemasi (LG, 29) kama daraja za sakramenti moja ya Daraja Takatifu. Kwa hivyo, kwa kivumishi "kihierarkia," Mtaguso unataka kuonesha asili takatifu ya huduma ya kitume katika tendo la Yesu, Mchungaji Mwema, pamoja na uhusiano wake wa ndani.

Kwanza kabisa, maaskofu, na kupitia wao makuhani na mashemasi, wamepokea majukumu (kwa Kilatini, munera) ambayo yanawaongoza katika huduma ya "wote walio wa Watu wa Mungu," ili "waweze kujitahidi kwa uhuru na kwa utaratibu kuelekea lengo moja na kupata wokovu" (LG, 18). Papa Leo XIV, kadhalika alielendelea kusema kuwa “Lumen Gentium inakumbusha kwa ufanisi mara kwa mara asili ya kiushirika na ya kijumuiya ya utume huu wa kitume, ikirudia kwamba "Huduma ambayo Bwana amewakabidhi wachungaji wa watu wake ni huduma ya kweli, ambayo katika Maandiko Matakatifu inaitwa kwa kiasi kikubwa 'diakonia,- ushemasi' yaani, huduma" (Lumen Gentium, 24).

Waamini katika katekesi ya Papa Leo XIV
Waamini katika katekesi ya Papa Leo XIV   (@Vatican Media)

Kwa hivyo inaeleweka kwa nini Mtakatifu Paulo VI aliwasilisha uongozi kama ukweli "uliozaliwa kutokana na upendo wa Kristo, ili kukamilisha, kueneza, na kuhakikisha upitishaji kamili na wenye matunda wa hazina ya imani, mfano, maagizo, na karama, zilizoachwa na Kristo kwa Kanisa lake”( Alloc. 14 sept. 1964, in Acta Synodalia III/1, 147). “Kwa kuhitimisha Papa alisema tuombe Bwana, ili atume katika Kanisa lake Wahudumu ambao wana upendo wa kiinjili, wanaojikita kwa wema wa wabatizwa wote, na wamisionari wajasiri kwa kila sehemu ya Ulimwengu.

KATEKESI PAPA MACHI 25

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.

25 Machi 2026, 11:24