Ujumbe wa Papa Leo XIV kwa TGcom24. Ujumbe wa Papa Leo XIV kwa TGcom24.  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV kwa Tgcom24:Taarifa huru na zenye heshima ni chombo cha amani

Katika ujumbe kwa mtandao wa habari wa Mediaset,katika hafla ya maadhimisho yake ya miaka 25,Papa Leo XIV anasisitiza dhamira muhimuya vyombo vya habari katika wakati wa mabadiliko na maneno yanayotamkwa mara nyingi mtandaoni.Mwaliko wake ni"kujenga madaraja ya mazungumzo na kukabiliana na habari potofu,sio tu kusimama kwenye uso wa habari,bali kwa kutazama pembezoni mwa mateso."

Vatican News

Ni ujumbe mfupi, lakini unaojumuisha misingi yote ya taarifa zinazojitangaza kweli. Ni ule uliotumwa na Baba Mtakatifu Leo XIV kwa Mkurugenzi na wafanyakazi wa uhariri wa Tgcom24. Hafla hii ni maadhimisho ya miaka ishirini na tano ya kuanzishwa kwa mtandao wa habari wa Mediaset.

Mazungumzo na heshima

Awali ya yote, Papa anaakisi nyakati za sasa, zilizo na alama ya mabadiliko makubwa na maneno yanayotamkwa mara nyingi kwenye Web-Wavuti." Kwa njia hiyo Papa anandika kuwa “Katika muktadha kama huo, dhamira muhimu ya vyombo vya habari inaibuka: ile ya "kujenga madaraja ya mazungumzo," huku ikihimiza uchambuzi wa kina. Hii ina maana, alielezea Papa Leo  XIV, kuwa "simulizi ambayo haiishii kwenye uso wa habari, lakini inaweza kutazama kwa heshima, mshikamano na huruma pembezoni mwa mateso."

Ukweli na Uwajibikaji

Kiini cha ujumbe wa Papa pia ni wito wa ukweli na "hisia ya kina ya uwajibikaji wa kimaadili," ili kukabiliana na "kuenea kwa habari za kugushi - ‘fake news’ " na kukuza "utamaduni wa kukutana" unaoweza "kuunganisha roho mbalimbali" za jamii.

Kwa amani isiyo na silaha na inayodumu

Pia Leo aidha anahimiza sana habari "huru na inayoheshimu utu wa binadamu," kwani inakuwa "chombo chenye nguvu" cha kuelekea "amani isiyo na siraha na inayodumu." Hatimaye, kabla ya kutoa baraka zake za kitume, Papa anaikabidhi timu ya Tgcom24 ulinzi wa Mtakatifu Francis de Sales, Mwalimu wa Kanisa na mlinzi wa vyombo vya habari vya Kikatoliki.

PAPA KWA TGcom24

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku bonyeza hapa: Just click here.

21 Machi 2026, 12:47