2026.03.16Wajumbe wa wafanyakazi wa uhariri wa TG2 ya RAI,katika hafla ya maadhimisho ya miaka 50 ya kuanzishwa kwake,pamoja na familia zao. 2026.03.16Wajumbe wa wafanyakazi wa uhariri wa TG2 ya RAI,katika hafla ya maadhimisho ya miaka 50 ya kuanzishwa kwake,pamoja na familia zao.  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV kwa TG2:hakuna uvumbuzi wa kiteknolojia unaoweza kuchukua nafasi ya uhuru wa mawazo!

Papa Leo XIV alikutana katika Ukumbi wa Clementine na wahariri wa Chaneli ya II(Tg2,)ya kipindi cha Matangazo cha Televisheni ya Italia(RAI),katika maadhimisho ya miaka 50 ya kuanzishwa kwake.Papa aliwasihi waandishi wa habari,"katika enzi ya akili Unde,waache kila wakati mfumo wa kibinadamu,ushinde,wakitofautisha kati ya njia na malengo."

Na Angella Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu  Leo XIV  akikutana na waandishi wa habari,  Jumatatu tarehe 16 Machi 2026, katika Ukumbi wa Clementina wa Jumba la Kitume, wahariri wa Tg2 wa kipindi cha habari cha Chaneli ya II ya umma ya Radio na Televisheni, Italia (RAI), katika hafla ya kumbukumbu ya miaka 50 ya kuzaliwa kwa matangazo hayo aliwaeleza kuwa "Siku hii ya kuzaliwa inatualika kutafakari safari mliyosafiri, kama mfano wa changamoto ambazo uandishi wa habari wa televisheni umekabiliana nazo na zile ambazo bado ziko mbele."

Papa akutana na Wahariri wa TG2 na familia zao
Papa akutana na Wahariri wa TG2 na familia zao   (@Vatican Media)

Papa Leo aliendelea kusema kuwa "Nafikiria mabadiliko kutoka kwa analogi hadi kidijitali, ambayo iliwafanya muwe wahusika wakuu katika kutumia fursa zake na kuelewa kwamba hakuna uvumbuzi wa kiteknolojia unaoweza kuchukua nafasi ya ubunifu, utambuzi muhimu, na uhuru wa mawazo." Na zaidi Papa aliongeza "Na ikiwa changamoto ya wakati wetu ni akili unde, nafikiria hitaji la kudhibiti mawasiliano kulingana na dhana ya kibinadamu, sio ile ya kiteknolojia, ambayo hatimaye inamaanisha kujua jinsi ya kutofautisha kati ya njia na malengo. " kwa hiyo Sifa tofauti ambazo zimewatambulisha tangu mwanzo ni usekula na wingi wa vyanzo vya habari, hata kwenye televisheni ya serikali.

Papa akutana na Wahariri wa TG 2 na familia zao
Papa akutana na Wahariri wa TG 2 na familia zao   (@Vatican Media)

Usekulari, unaoeleweka kama kukataa kiitikadi cha awali na mtazamo wazi kuhusu ukweli. Sote tunajua jinsi ilivyo vigumu kushangazwa na ukweli, kukutana, kutazama, na sauti za wengine; jinsi kishawishi kilivyo na nguvu cha kutafuta, kuona, na kusikiliza tu kile kinachothibitisha maoni ya mtu mwenyewe. Lakini hakuwezi kuwa na mawasiliano mazuri, wala uhuru wa kweli na wingi wenye afya bila uwazi huu. Misimamo tofauti ya kitamaduni imekuwepo katika historia yote ya Tg2. Utofauti huu, hasa unapochochewa na roho ya urafiki, umekuwa thamani ya ziada kwa utambulisho wako, utajiri, mfano wa mazungumzo, ambayo bado inaweza kutuambia mengi leo, katika enzi inayotawaliwa na mgawanyiko, kufungwa kwa kiitikadi, na kauli mbiu zinazotuzuia kuona na kuelewa ugumu wa ukweli.

Papa akiwapatia baraka wahariri wa TG na familia zao
Papa akiwapatia baraka wahariri wa TG na familia zao   (@Vatican Media)

Siku zote, Papa aliongeza lakini hasa katika hali ngumu za vita, kama ile tunayopitia, taarifa lazima zijilinde dhidi ya hatari ya kugeuka kuwa propaganda." Na kazi ya waandishi wa habari, katika kuthibitisha habari, ili wasiwe wasemaji wa mamlaka, inakuwa muhimu zaidi na ya haraka na , ningesema ni muhimu zaidi." Ni juu yao kuonesha mateso ambayo vita hupelekea kwa watu kila wakati; kuonesha uso wa vita na kuielezea kupitia macho ya waathiriwa ili wasiigeuze kuwa mchezo wa video". Hili Papa alisisitiza kuwa "si rahisi katika dakika chache za matangazo ya habari na sehemu zake za kina. Lakini hapa ndipo changamoto ilipo." Amewashukuru tena kwa ziara yao na aliwatakia matashi mema na kuwabai wote na kazi zao.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku bonyeza hapa: Just click here.

16 Machi 2026, 13:31