2025.11.28 Viaggio Apostolico in Turkiye - Visita alla casa di accoglienza per anziani delle Piccole Sorelle dei Poveri

Papa Leo XIV kwa FADICA:Yesu anatufundisha kutambua kumsaidia jirani

Katika Ujumbe wa Papa katika fursa ya Maadhimisho ya miaka 50 ya Mtandao wa Kikatoliki wa Upendo FADICA-anapongeza usaidizi wa mtandao huo kwa kuimarisha elimu ya Kikatoliki na kutetea maisha ya binadamu: "Kila tendo la upendo kwa jirani yetu ni kielelezo cha upendo wa kimungu. Na alisema kuwa wao ni vyombo katika mikono ya Bwana,kioo cha upendo wa kimungu ambao unaakisi hasa katika usaidizi kwa yule ambaye hana chochote cha kutoa.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Papa Leo XIV alituma ujumbe katika maadhimisho ya miaka 50 ya FADICA-Catholic Philanthropy Network, Mtandao wa Kikatoliki wa Upendo nchini Marekani ambao unakaribisha na kusaidia michango ya Mifuko, na wafadhili kwa ajili ya shughuli na mipango ya Kanisa Katoliki Ulimwenguni kote. Kwa njia hiyo, katika ujumbe huo akiulekeza kwa Bi Alexia Kelley, Mwenyekiti na Rais wa CEO FADICA kwa niaba ya wote, anawatakia matashi mema, wanapoadhimisha miaka hiyo. “Mnapoadhimisha miongo mitano ya kufanya kazi pamoja na kutoa “shukrani zangu kwa msaada wenu mkubwa kwa Maaskofu mbalimbali ya Mabaraza ya Kipapa ya Curia Romana pamoja na mipango ya Kikatoliki nchini Marekani na  ulimwenguni kote.”

Yesu anatufundisha kutambua kumsaidi jirani

Papa Leo XIV kadhalika alielezea mkusanyiko wao umewafanyika katika kipindi Kitakatifu cha “Kwaresima, wakati ambapo, pamoja na sala na kufunga, Kanisa linawaalika Wakatoliki wote kufanya matendo ya huruma kwa bidii zaidi. Yesu alitufundisha kwamba katika kutambua jinsi ya kumsaidia jirani yetu, ni lazima tuige mfano wa Msamaria Mwema, ambaye bila ubinafsi alitoa muda na rasilimali zake kwa mtu ambaye hajawahi kukutana naye hapo awali(taz. Lk 10:25-37).” Mfano huu, Papa aliongeza, “unatuonesha, kama Papa Francisko alivyosema mara nyingi, mtindo wa Mungu wa ukaribu, huruma na upendo mpole. Tunapowasaidia wale wanaohitaji, hasa wale ambao hawawezi kutulipa, tunakuwa vyombo vya Bwana, kwani "kila tendo la upendo kwa jirani kwa namna fulani ni kielelezo cha upendo wa kimungu" (Dilexi Te, 26).”

Michango ya kusaidiza progami za kuhamasisha haki ya kijamii na elimu ya kikatoliki

Katika suala hilo Papa alisisitiza “michango yao katika kusaidia programu zinazokuza haki ya kijamii, kuimarisha elimu ya Kikatoliki, kutetea utu wa binadamu na kuwatunza walio katika mazingira magumu zaidi ni dhihirisho la upendo wa kimungu.” Na kwa hiyo Papa anaonesha matumaini yake kuwa “Ni matumaini yangu kwamba kazi yenu pia itawatia moyo wengine kukutana upya na Kristo kupitia huduma kwa kaka na dada zake wadogo, na kushiriki kwa ufahamu zaidi katika utume wa Kanisa.”

Mwenyezi atazidisha ukarimu kwa wanaohuduma wenye kuhitaji

Kwa hisia hizo Papa Leo “anawatia moyo waendelee katika utume wao unaostahili, wakiwa na uhakika katika ufahamu kwamba "Mwenyezi atazidisha  ukarimu kwa wale wanaowahudumia watu wenye uhitaji zaidi". Huku akiwahakikishia maombi yake na kuwakabidhi wanachama wote wa Mtandao wa Upendo FADICA-Katoliki,  “kwa maombezi ya upendo ya Bikira Maria, Mama wa Kanisa, na kwa hiari yake Papa Leo XIV alitoa Baraka yake ya Kitume kama ahadi ya amani na furaha katika Bwana.”

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku bonyeza hapa: Just click here.

13 Machi 2026, 10:15