2026.03.13 Wajumbe wa Mfuko Katoliki. 2026.03.13 Wajumbe wa Mfuko Katoliki.  (@VATICAN MEDIA)

Papa Leo XIV:kukuza programu za maendeleo ya vijana kwa njia za kielimu

Baba Mtakatifu Leo XIV wakati akipongeza juhudi za Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Kikatoli,Italia aliokutana nao Ijumaa tarehe 13 Machi 2026,aliwahimiza wakuze daima roho ambayo inahusisha na mtindo wa kiinjili,kwa sababu uendane kati ya malengo wanayopendekeza na njia na vyombo wanavyotumia kuyafuatilia.”

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV amekutana na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya “Mfuko wa Kikatoliki- tarehe 13 Machi 2026, mjini Vatican. Alikuwa na furaha ya kukutana nao, awali ya yote kwa sababu ilimpatia njia ya kuelezea shukrani zake kwa Mfuko huo Katoliki na Chama cha Bima Katoliki kwa ajili ya jitihada za kila mara kusaidai uwepo hai wa Wakatoliki katika jamii ya kiitalia. Ziara yao zaidi, Papa alibainisha kuwa inampatia fursa ya kusisitiza jinsi gani ilivyo muhimu, katika wakati wetu, kujifunza, na kuthamanisha historia ya harakati Katolikia nchini Italia, kupata msukumo  na kuutafsiri katika leo hii ya ufahamu na zoefu za wanaume na wanawake ambao katika maisha yao waliunganisha Imani na jitihada  kwa ajili ya haki.

Kuandaa hata ngazi ya kiuchumi ili kukabiliana na masuala ya kijamii

Papa Leo XIV aidha alisema “Mamia ya vyama vya ushirika, benki za vijijini na vyama vya misaada ya pande zote vilikuwa mwitikio wa dhati  kwa mwaliko uliotolewa na Papa Leo XIII, katika Waraka wake wa Rerum Novarum, kuandaa hata kwa ngazi  ya kiuchumi ili kukabiliana na masuala ya kijamii.”  Miongoni mwa waanzilishi, alikuwa hata Mwanzilishi wa Chama Katoliki cha Bima, Kikundi cha Mapadre, na Walei ambapo kunako mwaka 1896  Verona wa kuanzisha chama cha ushirika, kilichoinuka kwa ushikiri wa watu ambao baadaye kiliendelea kuongezeka katika Nchi, kwa kusaidia Jumuiya kushida viwewe vya Vita mbili za Kidunia. Papa aidha aliendelea kukazia kuwa, miaka 20 iliyopita, katika muktadha unaoongezeka, lakini kuanzia na mizizi ile, Mfuko wa Kikatoliki ulizaliwa, kwa kutambua nafasi msingi katika usaidizi wa Jumuiya, watu na familia ambazo zinaisha katika hali ya udhaifu sana na Kutengwa kijamii. Kwa njia hiyo kwa kusaidia mipango mingi ya vijana, na makampuni ya kijamii, mfuko na mashirika ya kidini, wametoa mchango muhimu wa mshikamano wa kijamii na ulinzi wa watu walio katika mazingira magumu zaidi.

Kuwatia moyo waendeleea na Ahadi hiyo

Kwa hivyo Papa aliwatia moyo waendelee na ahadi hiyo, pia kwa kufanya kazi, kama, wanavyofanya tayari, ili kukuza programu maendeleo ya vijana kupitia za kielimu, kiutamaduni, na shirikishi. Nyongeza ya hivi karibuni katika uwanja huu ni Chuo wanakiita kwa Kiingereza: Chuo cha Sekta ya Tatu, kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Moyo Mtakatifu huko Milano, ambacho wanakusudia kukipanua hadi LUMSA huko Roma.

Kukuza roho ya mtindo wa kijamii

Na hatimaya, Baba Mtakatifu Leo XIV aliwashukuru kwa msaada ambao walitoa kwa miaka hii katika Tamasha la Mafundisho Katoliki ya Kijamii, mpango ambao ulikuwa moyoni sana wa Papa Francisko na ambapo, kwa roho hiyo hiyo, Mapitio ya Washairi wa Kijamii yameongezwa hivi karibuni. Baba Mtakatifu wakati akipongeza juhudi zao, amewahimiza wakuze daima roho ambayo inahusisha na mtindo wa Kiinjili, kwa sababu uendane kati ya malengo wanayopendekeza na njia na vyombo wanavyotumia kuyafuatilia. Mafundisho ya Mwenyeheri Giuseppe Toniolo, yawaangazie na kuwahuisha daima na kuwasaidia hata baraka yake ambayo Papa aliwapatia kwa moyo wao, na wapendwa wao. Walisali pamoja Sala ya Baba Yetu na akatoa Baraka.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku bonyeza hapa: Just click here

13 Machi 2026, 12:31