Siku ya Kimataifa ya HJisabati. Siku ya Kimataifa ya HJisabati. 

Papa Leo XIV:Kukuza maendeleo ya AI inayofanya nyanja ya kidijitali kuwa ya kibinadamu

Papa Leo XIV ametuma ujumbe uliotiwa Saini na Katibu Mkuu wa Vatican,kwa washiriki wa Siku ya Kimataifa ya Hisabati “kuzingatia jinsi wanahisabati wanavyoweza kuwa ishara za matumaini kwa ulimwengu mpana.Katika suala hili, eneo lenye matunda hasa la utafiti ni matumizi ya algoriti-mashine,hasa katika uwanja wa akili unde(AI).Kazi kama hiyo haihitaji juhudi za kiakili na werevu tu,bali ukuaji kamili wa mtu mzima,ili kujumuisha kiwango cha maadili cha teknolojia hizi zinazoibuka.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Tarehe 14 Machi 2026 ya kila Mwaka ni Siku ya Hisabati Ulimwenguni. Ni katika Muktadha huo ambapo Baba Mtakatifu Leo XIV alituma ujumbe wake uliosainiwa na Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican, katika fursa hiyo ya Siku ya Kimataifa ya Hisabati. Katika ujumbe huo uliotumwa kwa Profesa Betül Tanbay(1960) mtaalamu wa hisabati, mwanasayansi na profesa wa hisabati wa Kituruki katika Chuo Kikuu cha Boğaziçi huko Istanbul, na rais wa kwanza mwanamke wa Jumuiya ya Hisabati ya Kituruki kati ya 2010 na 2016.

Mwenyekiti wa Siku ya Kimataifa ya Hisabati

Baba Mtakatifu Leo XIV alifurahi kupokea bara yake ikimtaarifa yeye kuhusu siku ya Hisabati inayfanyika katika Mtandao tarehe 13 Machi 2026. Katika hisia ya furaha huyo anaelezea na kutima matashi mwema kwa wanaoshiriki. Mnapotafakari mada "Hisabati na Matumaini" katika muktadha wa changamoto nyingi zinazoikabili familia ya binadamu, hasa maendeleo ya haraka ya kiteknolojia pamoja na uwezo wake wote wa mema au mabaya, Baba Mtakatifu anawahimiza washiriki kuzingatia jinsi wanahisabati wanavyoweza kuwa ishara za matumaini kwa ulimwengu mpana.”

Kujumuisha kiwango cha maadili cha teknolojia

Katika suala hilo, eneo lenye matunda hasa la utafiti ni matumizi ya algoriti-mashine, hasa katika uwanja wa akili unde(AI). Kazi kama hiyo haihitaji juhudi za kiakili na werevu tu bali ukuaji kamili wa mtu mzima, ili kujumuisha kiwango cha maadili cha teknolojia hizi zinazoibuka. Hakika, akikumbuka wakati wake mwenyewe kama mwalimu wa hisabati na fizikia, Papa Leo XIV aliwakumbusha wanafunzi waliokusanyika kwa ajili ya Jubilei ya Ulimwengu wa Elimu: "Kuwa na maarifa mengi haitoshi ikiwa hatujui sisi ni nani au maana ya maisha ni nini". Hakika, akikumbuka wakati wake mwenyewe kama mwalimu wa hisabati na fizikia, Papa Leo XIV aliwakumbusha wanafunzi waliokusanyika kwa ajili ya Jubilei ya Ulimwengu wa Elimu:"Kuwa na maarifa mengi haitoshi ikiwa hatujui sisi ni nani au maana ya maisha ni nini" (Hotuba 30 Oktoba 2025).

Kwa njia hiyo Papa Leo XIV, anasali ili kila mmoja anayehusika kwenye tukio hilo atakuwa makini kwa mahitaji ya kina ya moyo wa binadamu, atatafuta njia za ubinadamu katika mzunguko wa kidijitali, kuunda fursa zenyewe kwa udugu na ubunifu, na atakuwa nabii wa matumaini, ukweli, na wema katika Ulimwengu.” Juu ya washiriki wote wa siku ya kimataifa ya mwaka huu 2026, Baba Mtakatifu Leo XIV  anawaombea baraka nyingi za kimungu za Hekima, furaha na amani.”

Mwenyekiti wa Siku ya Kimataifa ya Hisabati 2025 - 2028

Kwa sasa, Mwenyekiti wa Kimataifa wa Siku ya Hisababati inaongozwa na Bi Betül Tanbay, ambaye ameanza muhula wa huduma hiyo tangu 2025 -2028. Hii ni bodi ambayo husimamiwa na Umoja wa Kimataifa wa Hisabati (IMU) na wakati Bodi yake husimamia shughuli ya miktadha ya Kimataifa ya tukio kama hilo ambalo hufanyika kila ifikapo tarehe 14 Machi ya kila mwaka. Mwanzilishi ni Christiane Rousseau, ambaye hadi sasa anaendelea kuishughulia tangu 2025-2026).

Bi Betül Tanbay aliandika kuwa:“Hisabati hujaza maisha, inakupatia nguvu. Unapohisi kukata tamaa kuhusu ulimwengu, hisabati bado inadumu. Haiathiriwi na mabadiliko ya hali ya tabianchi, na ugomvi, siasa au uchumi. Sio suala la kuwa mzuri katika hisabati au la, ni suala la kuipenda. Pia, inakuwa nzuri zaidi unapoweza kushiriki udadisi na kazi.”

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku bonyeza hapa: Just click here

 

 

13 Machi 2026, 14:15