Moshi ukipanda baada ya shambulio la Israel katika vitongoji vya kusini mwa Beirut. Moshi ukipanda baada ya shambulio la Israel katika vitongoji vya kusini mwa Beirut. 

Maombi ya Papa Leo XIV kwa amani Iran&Mashariki ya Kati,majeruhi wengi na watoto wasio na hatia

Papa amekumbusha kifo na mazishi ya Padre Pierre El Raii,Padre wa parokia ya Wamaronite,katika moja ya vijiji vya Kikristo kusini mwa Lebanon aliyeuawa akitoa msaada wa mwana Parokia wake.“Bwana na amjalie damu yake iliyomwagika iwe mbegu ya amani kwa Lebanon mpendwa.”Ametoa wito wa kuendelea kuombea amani nchini Iran na kote Mashariki ya Kati,hasa kwa raia wahanga wengi,wakiwemo watoto wengi wasio na hatia.Sala zetu ziwe faraja kwa wale wanaoteseka na mbegu ya matumaini kwa siku zijazo.”

Na Angella Rwezaula -  Vatican.

Mara baada ya Katekesi  yake, Jumatano tarehe 11 Machi 2026, Baba Mtakatifu Leo XIV  kwa waamini na mahujaji waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, mjini Vatican  alioesha ukaribu wake kwa watu wa Lebanon ambao wanajikuta katika majaribu makubwa. Papa alisema: “Mazishi ya Padre Pierre El Raii, Padre wa Parokia ya Wamaronite, katika moja ya vijiji vya Kikristo kusini mwa Lebanon, ambayo kwa sasa inakabiliwa tena na mkasa wa vita, yanafanyika leo  hii huko Qlayaa, Lebanon.” Papa Leo XI aidha aliongeza kusema:  “ Niko karibu na watu wote wa Lebanon katika wakati huu wa majaribu makubwa. Kwa Kiarabu, "El Raii" (Alrai) inamaanisha "mchungaji."

Geneza la lenye mwili wa Padre Pierre mara baada ya misa ya mazishi
Geneza la lenye mwili wa Padre Pierre mara baada ya misa ya mazishi   (AFP or licensors)

Padre Pierre alikuwa mchungaji wa kweli

Kwa kumfafanua sifa za Padre huyo, Baba Mtakatifu Leo XIV alisema: “Padre Pierre alikuwa mchungaji wa kweli, ambaye siku zote alibaki karibu na watu wake kwa upendo na Sadaka ya Yesu Mchungaji Mwema. Mara tu aliposikia kwamba baadhi ya waamini wa parokia hiyo wamejeruhiwa na bomu, alikimbia bila kusita kuwasaidia. Bwana na amjalie damu yake iliyomwagika iwe mbegu ya amani kwa Lebanon mpendwa.”

Salamu mbali mbali

Vile vile Papa aliendelea na salamu kwa mahuaji kutoka Ulimwenguni kote, kufuatia hilo, ndipo Papa Leo XIV alisema, “Ninawakaribisha kwa dhati mahujaji wanaozungumza Kiitaliano, na hasa kwa Ndugu wa Mtakatifu Yohane wa Mungu, ambao ninawashukuru kwa huduma yao muhimu, hasa kwa walio katika mazingira magumu zaidi.”

Papa akibariki mwenge wa Mtakatifu Benedikto
Papa akibariki mwenge wa Mtakatifu Benedikto   (@VATICAN MEDIA)

Mtakatifu Benedikto, Mjumbe wa amani

Papa aliwasalimu Wajumbe wa "Mwenge wa Benediktini," wakiongozwa na Mameya wa Norcia, Subiaco, na Cassino, na kusindikizwaa na Askofu Mkuu Renato Boccardo. Papa aliongeza “Ninafurahi kubariki ishara hii ya udugu. Ninatumaini kwamba mwanga wake unaweza kuwatia moyo serikali na raia kujenga jamii inayotegemea maadili ya mshikamano na maelewano, wakifuata mfano wa Mtakatifu Benedikto, mjumbe wa amani.”

Tuendelee kujitolea katika safari kuelekea Pasaka

Hatimaye, mawazo ya Papa aliwageukia wagonjwa, wenye ndoa wapya, na vijana, hasa wanafunzi wa Shule  wa shule mbali mbali: ya Sekondari ya Galileo huko Siena, Taasisi ya Mtakatifu  Leo IX huko Sessa Aurunca, na Taasisi ya Gadda huko Quarto. Papa aliongeza kusema kuwa “Katika Kipindi hiki  Kwaresima, tuendelee na kujitolea katika safari ya kuelekea Pasaka, fumbo kuu la imani yetu.”

PICHA YA PAMOJA NA WATOTO WA SHULE
PICHA YA PAMOJA NA WATOTO WA SHULE   (@Vatican Media)

Kuombea amani nchin Iran na Mshariki ya kati

Papa Leo katika salamu zake, pia hakusahau kuombea watu wanaoteseka kwa vita na kusema kuwa “ Kaka na dada wapendwa, tuendelee kuombea amani nchini Iran na kote Mashariki ya Kati, hasa kwa wahanga wengi  raia, wakiwemo watoto wengi wasio na hatia. Sala zetu ziwe faraja kwa wale wanaoteseka na mbegu ya matumaini kwa siku zijazo.”

PAPA WITO LEBANON

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.

 

 

11 Machi 2026, 16:09