Kupewa daraja la Upadre. Kupewa daraja la Upadre.  (Vatican Media)

Papa atawaweka Daraja la Upadre Mashemasi 8 wa Jimbo Kuu la Roma

Pamoja na kuwekwa Daraja la Upadre katika Kanisa Kuu la Vatican,Papa Leo XIV pia aliidhinisha kuwekwa daraja la mashemasi saba wa kudumu,watakaowekwa wakfu tarehe 18 Aprili 2026 katika Kanisa Kuu la Mwokozi Mtakatifu Sana na Watakatifu Yohane Mbatizaji na Mwinjili huko Laterani katika mikono ya Makamu wa Papa,Kardinali Reina.

Vatican News

Baba Mtakatifu Leo XIV, mnamo tarehe 7 Machi 2026 alitoa idhini ya kuwaweka wakfu wa Kikuhani na Ushemasi wa Kudumu wa Jimbo Kuu la Roma, iliyowasilishwa na Tume husika za Promovendis ad Ordines Sacros, yaani kwa ajili ya kupandishwa hadhi hadi Daraja Takatifu.

Wagombea wa kupewa daraja la Upadre

Papa Leo XIV kwa njia hiyo atawaweka wakfu wa Daraja la Upadre watarajiwa, Jumamosi tarehe 26 Aprili 2026, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Vatican (Dominika ya Nne ya Pasaka, inayojulikana kama Dominika ya Mchungaji Mwema). Hawa ni: Guglielmo Lapenna, Giorgio Larosa, José Emanuele Nleme Sabate, Giovanni Emanuele Nunziante Salazar, Antonino Ordine, Yordan Camilo Ramos Medina, Daniele Riscica, na Cristian Sguazzino. Kanisa lote kuu la Roma linafurahi, kulingana na taarifa kutoka Vikarieti.

Wa Daraja la Ushemasi wa Kudumu

Wagombea wa Ushemasi wa Kudumu ni: Attilio Altamura, Alfredo Arolchi, Roberto Carletti, Mauro Chialastri, Salvatore Cottu, Giuliano Ferraro, na Igino Travaglino. Hawa watawekwa wakfu Jumamosi, tarehe 18 Aprili 2026, saa 4:00 asubuhi majira ya Ulaya, katika Kanisa Kuu la Papa la Mwokozi Mtakatifu Sana na la Watakatifu Yohane Mbatizaji na Mwinjili, huko Lateran, kwa kuwekewa mikono na Kardinali Baldassare Reina, Makamu wa Papa, Jimbo Kuu la Roma.

Katika sala iliyoshirikishwa na Jimbo Kuu la Roma, ni kwamba wahusika hawa: "Na wawe waaminifu kwa wito waliopokea na kuwa, kwa moyo wa Kristo, watumishi wanyenyekevu na wenye furaha wa Injili," na kuwaalika waamini wote kujiunga katika kuomba kwa ujasiri "zawadi ya miito mipya na mitakatifu ya Upadre na Ushemasi, ili Bwana aendelee kujenga Kanisa lake na kuwapa wachungaji na wahudumu wakarimu kwa watu wake."

Asante kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here.

09 Machi 2026, 18:00