Papa atapokea Nishani ya Uhuru kwa jitihada za kuhamasisha uhuru
Vatican News
Kituo cha Katiba cha Kitaifa kitamtunuku Papa Leo XIV Nishani ya 38 ya Uhuru wakati wa sherehe ya umma mnamo tarehe 3 Julai 2026, usiku wa kuamkia miaka 250 ya kuanzishwa kwa Marekani, nje ya Ukumbi wa huru huko Philadelphia. Tuzo hiyo inatambua kazi ya Papa katika kuhamaisha uhuru wa dini, dhamiri, na kujieleza ulimwenguni kote kama ilivyoainishwa na Mababa waanzilishi wa Marekani katika Marekebisho ya Kwanza ya Katiba ya Marekani. Papa Leo XIV anakusudia kutoa hotuba yake ya kukubali moja kwa moja kutokea mjini Vatican kupitia kiungo pepe kitakachotangazwa mtandaoni.
Shukrani ya Papa
Msemaji wa Ofisi ya Vyombo vya Habari ya Vatican, Matteo Bruni, alisema, Papa anashukuru sana "kwa utambuzi huu wa kifahari, katika kumbukumbu muhimu kama hiyo kwa watu wa Marekani, wanaoitwa kutafakari miaka 250 ya historia yao, kuhifadhi Azimio la Uhuru, Katiba ya Marekani, na uhuru kama alama za urithi wao kwa vizazi vijavyo."
Kujitolea kwa Papa Leo XIV kwa Mazungumzo
Taarifa kwa vyombo vya habari ya Kituo cha Katiba ya Taifa inasisitiza kujitolea kwa Papa kwa mazungumzo ya kidini na kiekumene. "Kitendo chake, kinaonesha maono mapana ya kimaadili ambayo yanachukulia uhuru wa kidini si kama haki ya kufikirika, bali kama usemi halisi wa utu wa binadamu, hasa kwa jamii zilizotengwa, ikiwa ni pamoja na dini ndogo na zile zilizoathiriwa na migogoro."
Asili ya Utambuzi
Kituo cha Katiba ya Taifa huko Philadelphia huwaleta pamoja watu wa rika zote na mitazamo kutoka ulimwenguni kote ili kujifunza kuhusu, kujadili, na kusherehekea maono ya uhuru wa binadamu yaliyotangazwa na Katiba ya Marekani.
Nishani ya Uhuru - yaani Medali ya Uhuru ilianzishwa mwaka 1988 kuadhimisha miaka mia mbili ya Katiba ya Marekani. Ikitolewa kila mwaka, nishani hiyo inawaheshimu watu binafsi na mashirika jasiri na yenye dhamira yaliyojitolea kuhakikisha faida za uhuru kwa watu kote ulimwenguni.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku bonyeza hapa: Just click here.
