Papa Leo XIV:Tuchangie dawa katika siku za ukusanyaji wa Dawa
Edoardo Giribaldi na Angella Rwezaula – Vatican.
Ukweli: nchini Italia, watu nusu milioni wanaishi katika hali ya "umaskini wa kiafya." Na njia halisi ya kuwasaidia na matibabu yao: kuchangia dawa katika maduka ya dawa kuanzia Februari 10 hadi 16, 2026, katika wakati wa Siku za Ukusanyaji wa Dawa zinazotangazwa na Benki ya Dawa. Huu ni mwaliko uliozinduliwa na Papa Leo XIV kupitia wasifu wake kwa lugha ya Kiitaliano, @Pontifex_it. Chapisho hilo linabainisha kwamba dawa zitakazokusanywa zitawasilishwa "kwa zaidi ya mashirika elfu mbili ya upendo na ustawi Italia yote, ambayo yatawasambazia wale wanaohitaji."
Kwa miaka 24, zaidi madawa milioni saba yamekusanywa
Mpango huu umekuwa ukifanyika kila Februari tangu 2000, huku maelfu ya watu wa kujitolea wakiwa na wafanyakazi wa maduka ya dawa yanayoshiriki,wakiwaalika wakazi kuchangia dawa moja au zaidi kwa mashirika ya kutoa misaada ya ndani. Mkusanyiko huu unashughulikia aina zote za dawa zinazouzwa bila agizo la daktari, na wafamasia, kwa maelekezo ya vyama, mara nyingi hutambua wale wanaohitaji zaidi. Katika miaka 24, Siku ya Ukusanyaji wa Dawa imekusanya zaidi ya dawa 7,991,000, zenye thamani ya zaidi ya Euro million 29.7. Toleo jipya zaidi lilihusisha maduka ya dawa 5,684 na zaidi ya watu wa kujitolea 25,600; kati ya dawa 588,013 zilizokusanywa, angalau watu 430,000 walinufaika, wakisaidiwa na mashirika 2,011 yanayohusiana na Benki ya Dawa.
Historia ya Benki ya Dawa
Mpango huo ulianzishwa mwaka 2000 na kundi la Wafamasi vijana, wakijua hitaji la kushughulikia "umaskini wa huduma ya afya" unaotajwa na Papa. Kwa msaada wa Cdo Opere Sociali na Federfarma, kikundi hicho kiliweka misingi ya shirika hilo, kikiiga mfano wa ukusanyaji huo kulingana na uzoefu wa Siku ya Kitaifa ya Ukusanyaji wa Chakula cha Benki ya Chakula. Ukusanyaji wa kwanza wa dawa ulifanyika Milano mwaka 2000, huku maduka ya dawa 250 yakishiriki, na kutoa jumla ya dawa 15,000.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here.
