Amani iwe kwenu. Amani iwe kwenu.  (@VATICAN MEDIA)

Papa Leo XIV:Ni mioyo yenye amani tu inaweza kujenga amani ya haki na ya kudumu

Tunachapisha utangulizi wa kitabu kipya cha Papa Leo XIV chenye kichwa:“Peace Be with You!” kilichohaririwa na Nyumba ya Vitabu ya Harper Collins ambacho tangu Februari 24,kinapatikana katika maduka ya vitabu ya Marekani na Nchi zinazozungumza Kiingereza.Ni toleo la kitabu cha Kiingeza “Amani Iwe nayi,”kilichochapishwa kunako Agosti 2025 katika Duka la Vitabu la Vatican.

Leo XIV

Amani ni moja ya mada muhimu sana katika wakati wetu na ni zawadi yenye kudai: zwadi ya Mungu iliyojengwa na wanawake na wanaume kwa karne. Tunaishi katika dunia iliyojeruhiwa na migogoro mingi na kukumbwa na uadui wa kikatili. Utaifa wa kutisha unaokanyaga haki za walio wadhaifu zaidi. Mapema zaidi kabla ya kuvunjwavunjwa katika kambi ya mapambano, amani inashindwa katika moyo wa ubinadamu, wakati tuangukia katika ubinafsi na ukavu  na wakati tunaporuhusu  maslahi  ya pande kushinda badala ya kutazama wema wa pamoja.

Waandishi wengi walisema kuwa ni pale ambapo tunapokaa kusikiliza historia za watu wengineo, ambao tunaanza kuwanyima hadhi zao. Kujifanya kuchukua hadhi  utu wa wengine ni hatua ya kwanza kuelekea vita yoyote. Hata hivyo, kuwajua wengine ni kielelezo cha amani. Lakini ili kutambua, awali ya yote inahitajika kujua kupenda. Mtakatifu Agostino alisema kuwa, “huwezi kumjua mtu ikiwa siyo kupitia urafiki”(Masuala 83 tofauti,71). Ninapenda kutafakari hapa juu ya aina mbili za amani, ambayo ni wima yaani (amani kama zawadi kutoka juu) na mlalo(amani kama uwajibikaji wa kila mtu.) Amani ni zawadi ambayo Mungu alitoa kwa wanaume na wawake wa kila wakati kwa njia ya kuzaliwa ya Yesu wa Bethlehemu. Malaika walitangaza amani duniani, kwa sababu Mungu alifanyika mwanadamu. Yeye alikumbatia ubinadamu kwa namna ya kina zaidi cha kuharibu kwa msalaba wake uadui wa dhambi.

Mtakatifu Agostino anaandika: “hata sisi tutatukuzwa kwa Mungu huko juu mbinguni katika ufufuko wa mwili wa kiroho, tutakapo nyakuliwa katika mawingu kukutana na Kristo: lakini kwa sababu,sasa tukiwa duniani, tutafute  amani kwa mapenzi mema (Hotuba ,193). Utukufu wa Mungu umeshuka duniani kwa ajili ya kutufanya tushiriki wema wake usioisha.  Zawadi hii inaalika tendo la uwajibikaji wa jibu letu, la “mapenzi yetu mema.” Zaidi ya hayo, amani ni zawadi ambayp Mfufuka alitoa kwa mitume wake. Ni amani “iliyojeruhiwa” na majeraha ya kusulibiwa, kwa sababu amani ya Yesu inayobubujika kutoka moyo unaopenda na ambao unaacha kuguswa na mateso ya kila wakati na kila mahali. Bwana baada ya ufufuko aliwatokea mitume wake na kuwasalimia akisema: “Amani iwe nanyi.” Kwa njia hiyo ndiyo maana amani ni salamu ya wokovu, kwa kuwa neno lenyewe “Salamu” linachukua jina kutoka wokovu(Mtakatifu Agostino,Hotuba,116).

Amani pia ni juhudi na uwajibikaji kwa kila mmoja wetu. Amani ina maana ya kufundisha watoto kuheshimu wengine na siyo kuwanyanyapaa wengine wakati wanacheza. Amani maana yake ni kushinda ubinafsi wetu na kuacha nafasi ya mwingine, katika udhaifu wetu, kazini na katika michezo. Amani ni wakati moyo wetu na maisha yetu yanatawaliwa na kimya, kwa kutafakari na kwa kusikiliza Mungu, kwa sababu Mungu habariki kamwe vurugu, hakubaliani kamwe kuchuka fursa za wengine au unyanyasaji wa aridhi ambayo iko inabadilisha Muumba, na  bembelezo la Muumbaji.

Tunaweza kujihisi wasio na nguvu mbele ya vita vingi ambayo vinaendelea kupiganiwa katika ulimwengu. Tunaweza kujibu kwa namna mbali mbali kwa kile nilichokifafanua kama “utandawazi wa kutokuwa na uwezo:” wanaoamini wanaweza awali ya yote na zaidi kutoa sauti kwa sala. Sala ni nguvu “isiyo na silaha” ambayo inatafuta wema tu, bila ubaguzi. Kwa kusali, tunapokonya ubinafsi wetu na tunakuwa na uwezo wa bure na ukweli. Zaidi ya hayo moyo wetu ni kambi ya mapambano muhimu sana. Ni pale ambapo tunapaswa kujifunza ushindi usio na damu lakini wa lazima juu ya msukumo wa kifo na tabia ya utawala: ni mioyo ya amani tu ambayo inaweza kujenga ulimwengu wa amani.

Tunapaswa kufanya zoezi la utamaduni wa maridhiano, kwa kuunda maabara yasiyo na vurugu, matendo ambayo ya kutoaminiana kuelekeza wengine ili kuweza kuwa fursa ya kukutana. Moyo ni kisima cha amani, hapa tunapaswa kujifunza kukutana badala ya kugongana, kuaminiana, badala ya kishukiana, kusikilizana na kuelewana badala ya kujifunga wenyewe. Mwishowe, sera za kisiasa na jumuiya ya kimataifa, wanawajibu wa kuwezesha uingiliaji  kati katika migogoro, kwa kutumia sanaa ya mazungumzo na ya diplomasia. Bwana Mungu(…)utujalie amani ya kupumzika, amani ya Jumamosi, amani bila machweo:” Kwa maneno haya ya Mtakatifu Agostino, tuombe Baba ajalia ulimwengu wetu, na watu wake wote hasa wale ambao wamesahulika zaidi na ambao wanateseka zaidi, neema iliyobarikiwa ya amani ya haki na ya kudumu.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here

 

 

24 Februari 2026, 15:49