2026.02.04 Tuzo ya Zayed 2026. 2026.02.04 Tuzo ya Zayed 2026. 

Papa Leo XIV:Mwingine sio kama mgeni tena au tishio,bali atambulike kama kaka au dada!

Katika ujumbe wake kwa Siku ya Kimataifa ya Udugu wa Kibinadamu na wakati wa kuwasilishwa kwa Tuzo ya Zayed iliyotengwa kwa ajili yake,Papa asisizitiza ulazima wa dharura,wenye nguvu zaidi kuliko migogoro,tofauti na mivutano.Papa alionya kuwa“kubaki katika ulimwengu wa mawazo pia kutakuwa uharibifu wa matarajio hayo.Lazima kumwona mwingine kama kaka au dada,na kamwe si kama chombo cha kutumia au tishio.Ni kutangaza Udugu katika ulimwengu unaopuuza amani.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV alituma ujumbe wake katika fursa ya Siku ya Kimataifa ya Udugu wa Kibinadamu na uwakilishi wa Tuzo ya Zayed kwa ajili ya Udugu wa Kibinadamu tarehe 4 Februari 2026.  Papa Leo kwa furaha kubwa na kwa “moyo uliojaa matumaini” anawageukia wao kwa mara ya kwanza katika tukio hilo na Toloe la 7 la Kimataifa kwa tangu kutiwa Saini ya Hati kuhusu  Udugu wa Kibinadamu kati ya Papa Francisko na Imam Mkuu wa Alzar, Ahmad Al-Tayyeb. Katika fursa hiyo wanahasisha kitu chenye thamani na cha ubinadamu wetu Ulimwenguni: Udugu wetu, mfungamano usiotengenishwa ambao unaunganisha binadamu wote, walioumbwa  kwa mfano wa Mungu. Papa Leo XIV aliendelea kueleza kuwa leo hii uhitaji wa udugu huo siyo wazo la mbali, badala yake ni ulazima na dharura. Hatuwezi kudharau kutokana na kwamba, kaka na dada zetu kwa sasa wako wanateseka na vurugu za kutisha na vita.

Lazima tutangaze udugu wa kibinadamu ulio hai

Baba Mtakatifu anabainisha kuwa, lazima tukumbuke kwamba “katika kila vita kinachoharibiwa ni ‘mpango halisi wa udugu, ulioandikwa katika wito wa familia ya binadamu. Tunakumbushwa kuwa "kila kitu ambacho kina thamani na wakati huo huo mpango wa udugu ulitiwa muhuri katika familia ya binadamu (Papa Francisko, Fratelli tutti, 3 Oktoba 2020, nambari 26). Katika wakati ambapo ndoto ya kujenga amani pamoja mara nyingi hupuuzwa kama "utopia wa enzi nyingine" (FT, 30), lazima tutangaze kwa kusadiki kwamba udugu wa kibinadamu ni ukweli ulio hai, wenye nguvu kuliko migogoro yote, tofauti, na mivutano.

Ndoto zetu za thamani

Ni uwezo ambao lazima utimizwe kupitia kujitolea kwa kila siku kwa heshima, kushiriki, na huruma. Katika suala hili, kama nilivyowarudia hivi majuzi kwa wajumbe wa Kamati ya Tuzo ya Zayed, "maneno hayatoshi" (11 Desemba 2025). Imani zetu za ndani kabisa zinahitaji kuimarishwa kila mara kupitia juhudi inayoonekana. Kwa kweli, "kubaki katika ulimwengu wa mawazo na majadiliano, bila ishara za kibinafsi za mara kwa mara na za dhati, kutaharibu ndoto zetu za thamani zaidi"(Wosia wa Kitume Dilexi te, 4 Oktoba 2025, n. 119). Kama kaka na dada, sote tumeitwa kwenda nje ya mipaka na kuungana kuelekea hisia kamili ya kuwa pamoja (taz. Fratelli tutti, n. 95).

Maadili kuwa ushuhuda halisi

Kupitia Tuzo ya Zayed kwa Udugu wa Kibinadamu, leo tunawashukuru wale ambao wametafsiri maadili haya kuwa ushuhuda halisi wa "fadhili na upendo wa kibinadamu" (Salamu kwa Wajumbe wa Kamati ya Tuzo ya Zayed kwa Udugu wa Kibinadamu 2026, Desemba 11, 2025). Washindi wetu—Mheshimiwa Ilham Aliyev, Rais wa Jamhuri ya Azerbaijan; Mheshimiwa Nikol Pashinyan, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Armenia; Bi. Zarqa Yaftali; na shirika la Palestina Taawon, ni wapandaji wa matumaini katika ulimwengu ambao mara nyingi hujenga kuta badala ya madaraja. Kwa kuchagua njia ngumu ya mshikamano badala ya njia rahisi ya kutojali, wameonyesha kwamba hata migawanyiko mikubwa zaidi inaweza kuponywa kupitia hatua halisi. Kazi yao inashuhudia imani kwamba nuru ya udugu inaweza kushinda giza la mauaji ya ndugu.

Shukrani wa Rais wa Falme za Kiarabu

Hatimaye Papa alitoa shukrani zake kwa Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan, Rais wa Falme za Kiarabu, kwa msaada wake usioyumba kwa mpango huo, na pia kwa Kamati ya Zayed kwa maono yake na imani yake ya kimaadili. “Tuendelee kufanya kazi pamoja, ili nguvu ya upendo wa kidugu iweze kuwa njia ya pamoja kwa wote, na ili "mwingine" asiweze kuonekana tena kama mgeni au tishio, bali atambulike kama kaka au dada. Mungu, Baba yetu, awabariki kila mmoja wenu na wanadamu wote.”

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here

05 Februari 2026, 17:20