Papa Leo XIV awashukuru Wapambaji na Ofisi ya Ujenzi kwa huduma ya busara na thamani
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Dominika tarehe 8 Februari 2026, Baba Mtakatifu Leo XIV alikutana mjini Vaticanna Wasimamizi na Wafanyakazi wa Ofisi ya Mau na Ujenzi. Katika hotuba yake awali ya yote alianza na ishara ya Msalaba: “Kwa jina la Baba na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amani iwe nanyi! Habari za asubuhi! Dominika njema na karibu! Kaka na dada wapendwa wa Wataalamu wa Maua na Idara ya Ujenzi, pamoja na familia zenu. Pia kuna wimbo unaotusindikiza, na ni mzuri sana... Na muendelee kuimba.” Papa alianza hivyo na kuendelea kuonesha alivyotaka kukutana nao kabla ya sala na baadaye kushiriki pamoja katika sala ya Malaika wa Bwana na waamini wote ambao walikuwa tayari wameanza kukusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro. Awali ya yote alikuwa na utashi wa kuwasalimia na kuwashukuru kwa kazi yao wanayofanya kwa bidii sasa. Kama wakuu, wafanyakazi na wataalamu katika sekta hiyo ya Mji wa Vatican, wamejipambanua kwa ari kubwa ya shughuli zao, hasa wakati wa mwaka wa Jubilei ambayo imehitimishwa hivi karibuni.
Shukrani hata kwa jitihada ya pamoja, mamilioni ya wanahija waliwezza kusihi kwa utaratibu, na utulivu wa njia ya kuelekea Mlango Mtakatifu, wakishirikimatunda mema katika maadhimisho ya kiliturujia, Katekesi na matukio mengine. Ni shukrani ambayo aliitoa kutoka moyoni mwake, na kwamba "inageuka kuwa mwamko kwa ajili ya mipango ijayo, ambayo inatazama, iwe kwa kusasisha kila wakati huduma za kiufundi na uendeshaji, na ile ya umakini wa utunzaji wa mazingira mjini Vatican, hasa kwenye nafasi za sala na katika mikutano na Papa." Kupamba sehemu na usalama wa majengo vinapata kiukweli maana yake ya juu zaidi katika kusaidia ibada inayotolewa kwa waamini na huduma ya kichungaji ya Makanisa.
Kwa namna ya pekee, katika Basilika ya Mtakatifu Petro ni mahali patakatifu ambapo panahitaji kulindwa hasa kama hekalu la kutafakari, kwa sala, na maajabu ya kiroho. Uwanja ambao unakumbatia ulimwengu kwa nguzo zake za kushangaza, ni “tiketi ya kuingia” kwa namna ya kuelezea, ya kukaribisha wote. Baba Mtakatifu kwa namna hiyo aliwaalika wakati wanajikita na shughuli za kazi zao za kila siku, kwamba ni ya busara na yenye thamani kwa utume wa Kitume wa Papa. Kiukweli ni sehemu ya shughuli tata za Gavana na Kurugenzi ya Miundombinu ya mji wa Vatican na huduma, ambazo “ninazipongeza kwa usimamizi wao wa bidii wa kazi nyingi ndani ya Vatican.
Kila mmoja kwa upande wake, hasa wakati wa majaribu, Papa alisema, "tukumbuke kwamba sisi ni viungo vya kiumbe kimoja, ambacho kusudi lake ni kushuhudia Injili kulingana na amri ya Bwana, Mchungaji Mwema na Kichwa cha Kanisa. Kama ishara ya shukrani zangu, nawabariki kwa moyo wote, familia zenu zinazowasindikiza leo, na kazi yenu. Asante sana.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here.
