Papa awateua Maaskofu 4 wasaidizi wa Jimbo kuu la Roma
Vatican News
Hawa ni Maparoko kuanzia Padre Sparapani, Zenobbi, Carlevale, Valenti mapadre wanne ambao wanakuwa Maaskofu wapya wasaidizi wa Jimbo Kuu la Roma na wote wanatoka kwenye Ukleri wa Kijimbo ambao, siku ya Alhamisi tarehe 25 Februari 2026, wameteuliwa na Baba Mtakatifu Leo XIV.
Wasifu wa Sparapani
Monsinyo Stefano Sparapani alizaliwa Roma mnamo tarehe 24 Julai 1956. Alipata diploma ya upimaji na kuhudhuria Chuo cha Regina Apostolorum, chama cha Wakatoliki wa parokia mbalimbali. Alijiunga na Kitivo cha Falsafa katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Laterano, Roma na baadaye akajiunga na chuo cha Almo cha Capranica, akiendelea na masomo yake kwa ajili ya utaalamu wa Taalimungu ya Maadili katika Chuo cha Alphonsian, Roma.
Alipewa daraja la upadre kwa ajili ya Jimbo la Roma mnamo tarehe 4 Oktoba 1991. Alihudumu kama Padre msaidizi wa parokia (1991-1995) na Padre wa Parokia (1995-2010) huko Corviale; tangu 2010, amekuwa Padre wa Parokia ya Mtakatifu Basili, wakati 2015, amekuwa mkurugenzi wa kiroho Chuo cha Almo cha Capranica, na tangu 2025, aliteuliwa kuwa Msimamizi wa Sekta ya Kaskazini ya Roma.
Wasifu wa Zenobbi
Monsinyo Alessandro Zenobbi alizaliwa tarehe 10 Novemba 1969, jijini Roma. Alijiunga na Seminari Kuu ya Kipapa ya Kirumi. Alipewa daradaja la upadre wa Jimbo la Roma mnamo tarehe 28 Aprili 1996. Alihudumu kama Msaidizi wa Parokia (1996-2008) na Padre wa Parokia (2008-2017) ya Mtakatifu Policarpo. Tangu 2017, amekuwa Padre wa Parokia ya Mtakatifu Lucia na, na tangu 2025, Msimamizi wa Sekta ya Magharibi ya Roma.
Wasifu wa Carlevale
Monsinyo Andrea Carlevale alizaliwa Roma mnamo tarehe 8 Aprili 1971. Alijiunga na Seminari Kuu ya Kipapa ya Kirumi. Alipewa daraja la Upadre kwa ajili ya Jimbo la Roma mnamo tarehe 3 Mei 1998. Alihudumu kama Padre msaidizi wa Parokia huko Mtakatifu Galla ya Garbatella (1998-2003); Padre wa Parokia ya Mtakatifu Ireneo huko Centocelle (2003-2009); Msaidizi katika Seminari Kuu ya Kipapa ya Roma (2009-2015); Paroko wa Mtakatifu Maria wa Loreto huko Castelverde-Lunghezza (2015-2025). Katika kipindi hiki, pia alichaguliwa kuwa mkuu Kanda ya Mapadre wa kanda yake. Tangu 2025, amekuwa Padre wa Parokia ya Mtakatifu Yohane Mbatizaji ya de Rossi katika eneo la Appio-Latino. Papa amempatia makao ya Atella.
Wasifu wa Valenti
Monsinyo Marco Valenti alizaliwa mnamo tarehe 28 Februari 1961, huko Cantalupo ya Sabina, katika jimbo la Rieti na Sabina-Poggio Mirteto. Alijiunga na Seminari Ndogo ya Kipapa ya Kirumi na kisha Seminari Kuu ya Kipapa ya Kirumi. Alipata shahada ya kwanza katika falsafa kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Laterano, Roma na shahada ya kwanza katika Taalimungu kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregorian jijini Roma. Baadaye alipata cheti cha Taalimungu na shahada katika historia ya sanaa kutoka Kitivo cha Barua katika Chuo Kikuu cha La Sapienza huko Roma.
Alipewa daraja la Upadre kwa ajili ya Jimbo la Roma Roma mnamo tarehe 26 Aprili 1986. Amehudumu kama Padre msaidizi wa Parokia ya Mtakatifu Maria Goretti (1986-1989); Padre msaidizi wa Parokia ya Mtakatifu Maria Maddalena wa Pazzi (1990-1994); Padre msaidizi wa parokia ya Maria Mama wa Mungu(1994-1996); Padre wa Parokia ya Mtakatifu Yosefu Mfanyakazi (1996-2010); na Padre wa Parokia ya Mtakatifu Saturnino (2010-2024). Tangu 2024, amekuwa Padre wa Parokia ya Kugeuka Sura kwa Bwana Wetu Yesu Kristo. Kwa kupewa makao ya Atella.
Asante kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here
