Jimbo Kuu la Bamenda nchini Camerun limempata  Askofu Msaidizi, John Berinyuy Tata. Jimbo Kuu la Bamenda nchini Camerun limempata Askofu Msaidizi, John Berinyuy Tata. 

Papa amemteua Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Bamenda,Camerun

Ijumaa tarehe 13 Februari 2026 Papa amemteua Padre John Berinyuy Tata kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Bamenda nchini Camerun.Alizaliwa tarehe 18 Desemba 1975,huko Mbuluf-Shisong,katika jimbo la Kumbo.Alipewa daraja la upadre mnamo tarehe 30 Machi 2005.

Vatican News.

Baba Mtakatifu amemteua John Berinyuy Tata, ambaye kwa sasa alikuwa ni Gambera wa  Chuo Kikuu  Katoliki cha Camerun huko Bamenda, kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Bamenda (Camerun).

Wasifu wake

Askofu Mteule  John Berinyuy Tata alizaliwa tarehe 18 Desemba 1975, huko Mbuluf-Shisong, katika jimbo la  Kumbo. Alisoma Falsafa na Taalimungu katika Seminari Kuu ya Mtakatifu Thomas Aquinas huko Bambui (Bamenda). Alipewa daraja la upadre mnamo tarehe 30 Machi 2005.

Ameshika nafasi zifuatazo na kuendelea na masomo zaidi: Majukumu katika Parokia ya Mtakatifu Yosefu huko Bafut (2005-2006) na Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Patrick huko Babanki-Tungo (2006-2010); masomo ya Tasaufi katika Monasteri ya Wadomenikani huko Bambui; Shahada ya Uzamivu katika Taalimungu na utaalamu katika Anthropolojia ya Kikristo kutoka Kitivo cha Taalimungu cha Kipapa cha Teresianum Roma; Mkurugenzi wa Kiroho na Profesa katika Seminari Kuu ya Mtakatifu Thomas Aquinas huko Bambui; Msimamizi wa  Harakati ya Karismatiki (CARIS) ya Jimbo na, hadi sasa, Gambera wa Chuo  Kikuu Katoliki cha Camerun huko Bamenda.

 

13 Februari 2026, 13:20