2026.02.12 Papa akutana na Askofu Mkuu  Sviatoslav Shevchuk, wa Kyiv-Halic nchini Ukraine. 2026.02.12 Papa akutana na Askofu Mkuu Sviatoslav Shevchuk, wa Kyiv-Halic nchini Ukraine.  (@Vatican Media)

Papa akutana na Shevchuk,Mkuu wa Kanisa Katoliki la Kigiriki la Ukraine

Askofu Mkuu Mkuu wa Kyiv-Halič alipokelewa katika Jumba la Kitume la Vatican na Baba Mtakatifu tarehe 12 Februari 2026.Alimpatia Leo XIV orodha ya majina ya wafungwa na sanamu iliyowekwa kwa ajili ya amani.Kisha akamshukuru Papa kwa mshikamano na usaidizi kutoka Kiti Kitakatifu kwa dhamira ya kuokoa maisha ya wanadamu tangu mwanzo wa vita.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

"Karibu." "Nimefurahi kuweza kufika na kukuona." Alhamisi Februari 12, Papa Leo XIV alifungua siku yake na mktano na Mkuu wa Kanisa Katoliki la Kigiriki la Ukraine, Sviatoslav Shevchuk, katika Jumba la Kitume la Vatican. Askofu Mkuu wa Kyiv-Halich, kulingana na taarifa, alimshukuru Papa kwa mshikamano na usaidizi wake kwa Ukraine, na pia kwa juhudi za kidiplomasia za Vatican katika njia ya amani ya haki na ya kudumu nchini Ukraine.

Papa akimpokea Askofu Mkuu wa Ukraine
Papa akimpokea Askofu Mkuu wa Ukraine   (@Vatican Media)

 

Asante kwa mshikamano na usaidizi kwa Ukraine

Uangalifu maalum ulipewa kwa maisha ya sasa ya Kanisa Katoliki la Kigiriki la Ukraine na kiwango cha kimataifa cha huduma yake. Shevchuk alisisitiza kwamba Kanisa Katoliki la Kigiriki la Ukraine ni Kanisa maalum, lakini wakati huo huo la kimataifa, lililopo katika kila bara la dunia: "Kanisa letu maalum la Ukristo la Kiev lina asili ya Kiukraine, lakini si Kanisa la Waukraine, pekee, bali liko wazi kwa kutangaza kwa Injili kwa watu wote, hasa kutokana na ushirika kamili unaoonekana na Mrithi wa Mtume Petro," alimwambia Papa. Askofu mkuu pia aliripoti kwa Papa Leo XIV  kuhusu mipango kadhaa ya Kanisa Katoliki la Kigiriki la Kiukraine ya kushirikiana na jamii ya kiraia ya Kiukraine na jumuiya ya kimataifa, na pia aliwasilisha orodha ya wafungwa, waliopokelewa moja kwa moja kutoka kwa familia za wafungwa na watu waliopotea. Hatimaye alimshukuru Papa tena kwa dhamira muhimu ya kuokoa maisha ya wanadamu, ambayo Vatican imeshiriki kimfumo tangu mwanzo wa vita vikubwa nchini Ukraine.

Wakati wa mazungumzo yao
Wakati wa mazungumzo yao   (@Vatican Media)

Zawadi ya njiwa ya amani

Mwishoni mwa Mkutano huo, Askofu Mkuu Shevchuk alirejea mwaliko wake kwa Papa Leo XIV kutembelea Ukraine. Kama zawadi, alimkabidhi sanamu ya mchongaji na mtaalamu wa moyo wa Italia Luciano Capriotti, yenye kichwa "Njiwa ya Amani Wakati wa Vita.”  Mchoro wa kauri unaonesha njiwa dhaifu na mnyonge aliyepigwa na kipande cha chuma kutokana na kombora la Urusi lililorushwa Kharkiv. Jeraha hili linasababisha "maumivu makubwa" kwa ndege huyo, lakini bado yuko hai: "Ni ishara nzuri ya Ukraine ya kisasa, iliyojeruhiwa lakini hai," alisema mkuu wa Kanisa Katoliki la Kigiriki la Ukraine alipokuwa akimkabidhi Papa zawadi hiyo. Kabla ya kuondoka, aliomba baraka za Papa Leo XIV kwa ajili ya watu wa Ukraine. Na Papa, kwa upande wake, alimhakikishia maombi yake ya mara kwa mara kwa ajili ya Ukraine.

Askofu Mkuu wa Ukraine na Papa
Askofu Mkuu wa Ukraine na Papa   (@Vatican Media)

Mkutano huo  ulikuwa wa  pili y faragha kati ya mkuu wa Kanisa Katoliki la Kigiriki la Ukraine na Papa Leo XIV tangu kuchaguliwa kwake kuwa Papa. Mkutano wa kwanza ulifanyika tarehe 15 Mei  2025, tena katika Jumba la Kitume. Wakati wa Mkutano huo, Askofu Mkuu Shevchuk aliwasilisha orodha yenye majina ya wafungwa 500 wa Ukraine na watu waliopotea na akawasilisha uchoraji wenye jina la Requiem, uliowekwa wakfu kwa watoto ambao hawajazaliwa kutokana na vita. Papa na Shevchuk walikutana tena mnamo Juni 28, katika Basilika ya Mtakatifu Petro, wakati Papa Leo alipokutana na mahujaji wa Ukraine waliokuja Roma kwa ajili ya Jubilei ya Kanisa Katoliki la Kigiriki la Ukraine.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Bonyeza hapa tu: Just click here.

12 Februari 2026, 16:30