Papa Leo XIV: Mtakatifu Yohane Henry Newman, Padre na Mwalimu wa Kanisa, aandikwe kwenye Kalenda ya Jumla ya Kiroma Papa Leo XIV: Mtakatifu Yohane Henry Newman, Padre na Mwalimu wa Kanisa, aandikwe kwenye Kalenda ya Jumla ya Kiroma  

Kumbukumbu ya Hiyari ya Mtakatifu Yohane Henry Newman 9 Oktoba!

Baba Mtakatifu Leo XIV baada ya Mama Kanisa kumtangaza Mwenyeheri Yohane Henry Newman, Padre na Mwalimu wa Kanisa, kuwa Mtakatifu, sasa anaamuru kwamba: Mtakatifu Yohane Henry Newman, Padre na Mwalimu wa Kanisa, aandikwe kwenye Kalenda ya Jumla ya Kiroma na Kumbukumbu yake ya Hiari, itakuwa inaadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 9 Oktoba. Alijisadaka kwa ajili ya huduma ya kiakili, Kuhubiri na Kufundisha pamoja na kuwahudumia maskini

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Nuru ya upole na neema ya Mwenyezi Mungu, iliyokuja katika ulimwengu huu kuwaangazia watu wa Mataifa (Rej Lk 2:32), ilimwongoza Mtakatifu Yohane Henry Newman kupata amani katika Kanisa Katoliki na kumpa nguvu kiasi kwamba, aliweza kusema “Mungu ameniumba ili nimfanyie huduma fulani ya uhakika … Katika maisha yake marefu Kardinali Newman alijisadaka bila ya kujibakia katika huduma hii aliyokuwa ameitiwa. Hii ni Huduma ya uchunguzi wa kiakili; huduma ya kuhubiri na kufundisha; pamoja na huduma kwa maskini na wadogo. Akili yake hai imeliachia Kanisa amana, utajiri na umuhimu mkubwa katika nyanja za taalimungu, Mafundisho juu ya Kanisa, nyimbo za ushiri pamoja na Ibada. Ni mtu aliyetafuta ukweli na kuingia katika utimilifu wake na hivyo kuwa kweli kielelezo kwa kila Mfuasi wa Kristo Mfufuka.

Mtakatifu Yohane Henry Newman: Padre na Mwalimu wa Kanisa
Mtakatifu Yohane Henry Newman: Padre na Mwalimu wa Kanisa   (@VATICAN MEDIA)

Hivyo, kwa namna ya pekee, Mtakatifu Yohane Henry Newman, Padre na Mwalimu wa Kanisa, “John Henry Newman” akiwa ametambuliwa kuwa ni nuru angavu kwa Kanisa katika hija ya maisha na utume wake; kupitia historia, anaweza sasa kuhesabiwa kwa haki kuwa ni miongoni mwa Walimu wa Kanisa na watakatifu walioandikwa katika Kalenda ya Jumla ya Kiroma. Baba Mtakatifu Leo XIV baada ya Mama Kanisa kumtangaza Mwenyeheri Yohane Henry Newman, Padre na Mwalimu wa Kanisa, kuwa Mtakatifu, sasa anaamuru kwamba: Mtakatifu Yohane Henry Newman, Padre na Mwalimu wa Kanisa, aandikwe kwenye Kalenda ya Jumla ya Kiroma na Kumbukumbu yake ya Hiari, itakuwa inaadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 9 Oktoba.

Kumbukumbu hii inapaswa kuingizwa kwenye Kalenda na Vitabu vyote vya Liturujia ya Kanisa kwa ajili ya adhimisho la Ibada ya Misa Takatifu na Liturujia ya Vipindi kwa kufanya rejea katika Tamko la Baraza la Kipapa la Ibada na Nidhamu ya Sakramenti za Kanisa lililotolewa tarehe 9 Novemba 2025, Sikukuu ya Kutabarukiwa kwa Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane wa Laterani; Tafsiri hiyo baada ya kuchapishwa na Mabaraza ya Maaskofu Katoliki sehemu mbalimbali za dunia, itapaswa kuidhinishwa na Baraza la Kipapa la Ibada na Nidhamu ya Sakramenti za Kanisa, tayari kwa matumizi ya Liturujia ya Kanisa.

Mtakatifu Yohane Henry Newman kuadhimishwa kila mwaka 9Oktoba
Mtakatifu Yohane Henry Newman kuadhimishwa kila mwaka 9Oktoba   (ANSA)

Itakumbukwa kwamba, Mtakatifu Yohane Henry Newman, Padre na Mwalimu wa Kanisa alizaliwa tarehe 21 Februari 1801 huko nchini Uingereza. Kunako mwaka 1845 akaongokea Ukatoliki kutoka katika Kanisa Anglikani. Tarehe 30 Mei 1847 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre ndani ya Kanisa Katoliki. Katika maisha na utume wake kama Padre akonesha bidii ya kuhubiri, kufundisha na kuwahudumia maskini na wote waliokuwa wanasukumizwa pembezoni mwa jamii. Tarehe 12 Mei 1879 Papa Leo XIII akamsimika kuwa ni Kardinali.Akafariki dunia tarehe 11 Agosti 1890. Akatangazwa kuwa ni Mwenyeheri na Baba Mtakatifu Benedikto XVI huko Birmingham, Uingereza tarehe 19 Septemba 2010. Na ilipogota tarehe 13 Oktoba 2019 Baba Mtakatifu Francisko akamtangaza kuwa ni Mtakatifu. Ibada hii iliadhimishwa kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican. Na Baba Mtakatifu Leo XIV, tarehe Mosi Novemba 2025 akamtangaza kuwa ni Mwalimu wa Kanisa.

Mt. Newman 9 Oktoba
03 Februari 2026, 15:07