2026.02.09 Msaada wa jenereta na madawa kutoka kwa Papa(Kardinali Krajewski). 2026.02.09 Msaada wa jenereta na madawa kutoka kwa Papa(Kardinali Krajewski).  (cardinale Krajewski)

Ukraine:Katika hali halisi ya baridi kali mshikamano wa Papa umefika

Papa Leo XIV, kupitia Ofisi ya Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendoi lifikisha msaada wa jenereta 80 za umeme kwa nchi ya Mashariki kwa ajili ya wakazi wanaosumbuliwa na vita na baridi kali.Dawa kama vile viuasumu,dawa za kupunguza uvimbe,virutubisho na vifaa vya chakula pia vilitumwa.

Na Angella Rwezaula, - Vatican

Sala kwa ajili ya Ukraine iliyoombwa na Papa katika katekesi yake  Jumatano, Februari 4, inakuwa ishara ya upendo mbele ya "matokeo ya mabomu ambayo," Papa Leo XIV alisema, "pia yameanza kuathiri miundombinu ya nishati tena." Kutoka Ukumbi wa Paulo VI, ombi hilo, lililoambatana na maneno ya shukrani kwa mipango ya mshikamano ambayo imestawi katika majimbo mengi, hasa nchini Poland, likawa ukweli kutokana na Ofisi ya Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo, ambayo, kwa ombi la Papa, ilituma malori matatu yenye jenereta 80.

Wakati wa kupakia msaada kwa ajili ya Ukraine
Wakati wa kupakia msaada kwa ajili ya Ukraine   (cardinale Krajewski)

Kwa hivyo, Papa alikubali ombi la Maaskofu wengi, wakijua mateso ya watu kutokana na vita na ugumu unaosababishwa na hali ya baridi kali inayoikumba nchi ya Ukraine. Hali ya bari kali kwa usiku, kiukweli, hufikia nyuzi joto  hasi -15 , wakati wa mchana ikibadilika kati ya nyuzi joto  hasi -10 na - 12. Wengi wanalazimika kuacha nyumba zao kutafuta joto katika makazi yenye joto ambapo, shukrani kwa jenereta, wanaweza pia kupata mlo wa moto.

Kufika kwa dawa na vifaa vingine vya msaada
Kufika kwa dawa na vifaa vingine vya msaada   (cardinale Krajewski)

Jenereta na Dawa

Magari yaliondoka kutoka Hagia Sophia jijini  Roma, Kanisa la Kiukraini nchini Italia, na tayari yamefika Fastiv na Kyiv, hasa yameathiriwa na mashambulizi ya hivi karibuni. Hatua za kijeshi pia zilifanywa usiku huko Odessa na Kharkiv, na kusababisha kifo mtoto wa  miaka 10. Vita havina huruma, hata kwa watoto wadogo. Katika hali hii ya hofu na vurugu, kila ishara ya mshikamano ni pumzi ya utulivu kwa wale ambao wamekuwa wakipitia kiwewe cha mzozo kwa miaka minne sasa. Kando na jenereta, maelfu ya dawa, virutubisho, na melatonin, ambayo inahitajika sana kwa sababu inasaidia kukuza usingizi katika nyakati hizi za hofu na msongo wa mawazo wa kila mara, zimetumwa Ukraine.

Mwanamke aliyepokea madawa huko Ukraine
Mwanamke aliyepokea madawa huko Ukraine   (cardinale Krajewski)

Shukrani kwa wale wanaosaidia bila kuchoka

Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo pia lilitangaza kwamba lori lililojaa maelfu ya viuasumu, dawa za kupunguza uvimbe, dawa za kupunguza shinikizo la damu, na vifaa mbalimbali vimekamilika. Mara tu msaada utakapofika nchini, usambazaji utafanywa kupitia mtandao wa parokia za majimbo mbalimbali. Wimbi hili la michango ya bure linawezekana kutokana na Benki ya Dawa na mtandao wa makampuni mbalimbali ya dawa, kundi la Procter & Gamble, na, alisisitiza Kardinali Konrad Krajewski, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo ambaye aliwashukuru kwa niaba ya Papa, watu wote wenye mapenzi mema ambao huwasaidia bila kuchoka wale wanaoteseka.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here.

 

 

 

09 Februari 2026, 17:10