Afrika,Hispania na Ufalme wa Monako:Baada ya Jubilei Papa anaanza kusafari!
Vatican News
Ziara ya siku kumi barani Afrika, mbili Ulaya, ya siku moja katika Ufalme wa Monako na moja kati ya siku sita nchini Hispania katika Visiwa vya Kihispania vya Kanari. Baada ya Ziara ya kitume yenye maana sana huko Turkiye na Lebanon, mwishoni mwa 2025 na baada ya kutangazwa kwa ziara zijazo nchini Italia ambazo zitampeleka hadi Lampedusa, Baba Mtakatifu Leo XIV anaanza hija yake Ulimwenguni kama ilivyotolewa taarifa, kutoka Ofisi ya Habari ya Kiti kitakatifu, Jumatano tarehe 25 Februari 2026. Kwa njia hiyo, safari ndefu kuanzia tarehe 13 hadi 23 Aprili, itakayompeleka katika nyayo za Mtakatifu Agostino huko Algeria (Algeri na Annaba); hivyo kuendelea Afrika ya Kati huko Camerun(Yaoundé, Bamenda na Douala); Angola (Luanda, Muxima na Saurimo) na mwisho huko Guinea ya Ikweta(Malabo, Mongomo na Bata).
Ni safari nzito ambayo wakati huo huo, ziara katika kumbukizi ya Mtakatifu wa Hippo (Mzaliwa wa Algeria) ambaye sura ya Mfuasi wa Mtume Petro ameunganishwa sana naye, ambapo baadaye aweze kugusa Nchi mbili zinazoendelea kupiga amendeleo, kwa umakini hasa kwa walio wa mwisho, maskini na wale ambao wanawatunza. Hata amani itakuwa moja ya malengo kwa sababu, Papa Leo XIV ataelekea kiukweli katika Kanda ya Kiingereza huko Kaskazini mwa Camerun, mahali ambapo miaka 10 iliyopita, vita vya wenyewe kwa wenyewe vimeendelea na ambavyo vinaendelezwa kati ya nguvu za Jeshi la kawaida na zile za kujitegemea. Hatua ya mwisho, inawakilishwa na Guinea ya Ikweta, moja ya Nchi ya Afrika ambayo sehemu moja inazungumza Kihispania. Hija ambayo inakaribia ile iliyotimizwa kunako mwaka 1985 na Mtakatifu Yohane Paulo II kwa nchini 7 alizotembelea kwa siku 11.
Ufalme wa Monaco
Nchi itakayozindua ziara za Baba Mtakatifu katika nchi za nje karibu ya nusu ya Mwaka 2026 safari ya haraka kwa siku moja, ni katika Ufalme wa Monaco, inayotarajiwa kufanyika tarehe 28 Machi 2026 katika mkesha wa Juma Kuu Takatifu. Papa Leo XIV alipendelea kutoa jibu chanya kwa mialiko mingi iliyorudiwa na Mamlaka ya Ufalme huo, awali ya yote kwa Papa Francisko na kisha Yeye mwenyewe.Ufalme wa Monaco unawakilisha hali halisi ya Ulaya mahali ambapo Ukatoliki ni Dini ya Serikali na mahali ambapo mazungumzo kati ya Taasisi za kiraia na Kanisa zimedumisha umuhimu maalum katika mijadala ya umma. Kuna maana kubwa hata jitihada za amani kwa Ufalme huo ambao utakaribisha kwa mara ya kwanza Papa katika nyakati za kisasa.
Ziara ya Hispania na Visiwa vyake vya Kanari
Mwishoni kuanzia tarehe 6 hadi 12 Juni, Papa leo XIV atatembelea nchini Hispania: katika Mji Mkuu Madrid na baadaye Barcellona, ili kuzindua Mnara mpya mrefu zaidi wa Basilika ya Familia Takatifu ambao ulibadilisha upya anga ya jiji la Kikatalani. Ziara hii inaangukia katika Maadhimisho ya Miaka 100 ya Kifo cha Mwakiliojia ambaye “aliota Ndoto” ya Basilika na akaanza kuitimiza, Antoni Gaudí, ambaye mwaka 2025 alitangazwa kuwa Mtumishi wa Mungu. Baba Mtakatifu kwa kubaki Hispania kutoka Barcellona atakwenda kwenye Visiwa vya Kanari, ili kutimiza safari ambayo ilikuwa tayari kwenye moyo wa Papa Francisko, kama alivyosititiza mwezi Januari iliyopita, Kardinali José Cobo Cano, Askofu Mkuu wa Madrid.
Vituo vitakuwa viwili Tenerife na Gran Canaria. Kwa kupitia ziara tatu hizi za Askofu wa Roma, kwa namna ya kufanya mikutano yenye aina tofauti zaidi ya Nchi, na ya hali halisi, atapitia taifa moja la kiislamu ambapo Wakristo ni wachache na mbegu ya udugu, kama vile Algeria, Nchi ambayo sehemu kubwa ya Wakristo wako katika moyo wa Bara la Afrika, kwa matatizo yao na ushuhuda wao wa imani ya furaha. Atafanya safari fupi kwenda nchi ya pili ndogo zaidi duniani baada ya Jiji la Vatican, lililoko kwenye Pwani ya Blu, na hivyo kwenda nda katika Nchi Kubwa ya Ulaya, Hispania, ambapo utambulisho wake ulibuniwa na imani ya Kikristo lakini inaathiriwa na mambo ya kidunia. Na Papa atahitimisha Ziara yake kwenye kisiwa cha Kanari, moja ya kisiwa chenye mapambano ya wahamiaji kutoka Afrika kuelekea Ulaya, kwa mamia elfu ya mitumbwi inayofika kila mwaka.
Asante kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here
