Picha ya baadhi ya  Mapadre wa Taasisi ya Kanisa ya Elimu aliokutana nao tarehe 20 Juni 2025. Picha ya baadhi ya Mapadre wa Taasisi ya Kanisa ya Elimu aliokutana nao tarehe 20 Juni 2025.  (@VATICAN MEDIA)

Papa Leo XIV:wanadiplomasia wa Papa wawe madaraja yasiyoonekana ya usaidizi

Katika barua kwa Chuo cha Kipapa cha Kanisa katika hafla ya Maadhimisho ya miaka 325 ya kuanzishwa kwake,Papa Leo XIV alieleza kuwa:“Diplomasia inatafuta njia za upatanisho ambapo kuta na kutoaminiana huinuliwa.Wanadiplomasia wa Papa sio wa kimkakati,bali ni upendo wenye mawazo;hawatafuti washindi wala walioshindwa,hawajengi vikwazo,bali huanzisha tena vifungo halisi.Aliwashukuru wakuu wa chuo hicho na wanafunzi kwa safari ya ushirika na upya inayofanywa kwa roho ya imani na uwazi.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV tarehe 17 Januari 2026 alituma Barua kwa Chuo cha Kipapa cha Kanisa katika hafla ya maadhimisho ya miaka 325 ya kuanzishwa kwa Chuo na kwamba pamoja nao anamshukuru Bwana kwa historia ndefu na yenye matunda ya taasisi hiyo inayostahili, iliyowekwa kwa ajili ya huduma ya Mrithi wa Petro. Kunako mwaka 1701, kwa mapenzi ya Papa Clement XI, utume unaosifiwa sana ulianza, ambao roho yake ilihifadhiwa na ukuaji wake uliongozwa na watangulizi wake  wengi, ukiambatana na maendeleo yake kwa kuzingatia mahitaji yaliyooneshwa na Kanisa na diplomasia kwa karne nyingi. Papa Leo XIV, anathibitisha kuwa katika miaka ya hivi karibuni, Papa Francisko, pamoja na Katiba ya Kitume Praedicate Evangelium, yaani “Hubirini Injili”Injili ilithibitisha nafasi ya Chuo hicho ndani ya muundo wa Sekretarieti ya Vatican, ikiiweka kuhusiana na Kitengo cha Wafanyakazi wa Kidiplomasia wa Kiti Kitakatifu. Kisha, Barua ya Mkono wake wa hati ya “Il Ministero Petrino,” yaani “Huduma ya Petro ya tarehe 25 Machi 2025, kiliinuliwa kuwa kama Kituo cha Juu cha Mafunzo ya Kitaaluma na Utafiti wa hali ya Juu katika Sayansi ya Kidiplomasia, chombo cha moja kwa moja cha hatua ya kidiplomasia ya Kiti Kitakatifu.

Huduma ya kidiplomasia si taalumabali ni wito wa kichungaji

Baba Mtakatifu anaendelea kukazia kuwa “Mageuzi haya ya hivi karibuni yanaonesha lengo la kutoa mtaala ambao, kwa msingi imara wa kisayansi, unaunganisha ujuzi wa kisheria, kihistoria, kisiasa, kiuchumi, na lugha na kuuchanganya na sifa za kibinadamu na kikuhani za mapadre vijana.” Kwa njia hiyo Papa aliongeza kuwashukuru Wakuu na wanafunzi wa Chuo cha Kipapa cha Kanisa kwa safari ya ushirika na upya inayofanywa katika roho ya imani na uwazi, ikikumbatia mabadiliko bila kusahau mizizi yetu.” Ni matumaini ya Baba Mtakatifu kwamba “maadhimisho haya mazuri yatawatia moyo wanafunzi kujitolea upya kwa kuendelea katika malezi yao, wakikumbuka kwamba huduma ya kidiplomasia si taaluma, bali ni wito wa kichungaji: ni sanaa ya kiinjili ya kukutana, ambayo hutafuta njia za upatanisho ambapo watu hujenga kuta na kutoaminiana.” Kwa kukazia zaidi alisema “Diplomasia yetu, kiukweli, huzaliwa kutokana na Injili: si Mkakati,  bali ni upendo wenye mawazo; haitaji washindi wala walioshindwa, haijengi vikwazo, lakini hujenga upya vifungo vya kweli.”

Wanadipolamsia wa Papa wameitwa kuwa madaraja

Na ili  kujenga ushirika huu, Papa alitoa ushauri kuwa “kila neno linalosemwa lazima litanguliwe na kusikiliza: kumsikiliza Mungu na kuwasikiliza wadogo, wale ambao sauti zao mara nyingi hazisikiki. Wanadiplomasia wa Papa wameitwa kuwa madaraja: madaraja yasiyoonekana ya usaidizi, madaraja imara wakati matukio yanaonekana kuwa hayawezi kuzuilika, na madaraja ya matumaini wakati wema unapopungua. Kwa kumwiga Mtakatifu Antoni Abate, mlinzi wao aliyebadilisha ukimya wa jangwani kuwa mazungumzo yenye matunda na Mungu, Papa amewashauri wawe “makuhani wa kiroho cha kina, mkichota kutoka katika sala nguvu ya kukutana na wengine." "Na macho yenu yanapofunguka kwa utume unaowangojea, ninawakabidhi kila mmoja wenu kwa Maria, Mama wa Kanisa, ili awatunze na kuwafanya muwe watiifu kwa mapenzi ya Mungu katika huduma ya Kiti cha Petro. Kwa matashi haya, ninawapatia kwa moyo mkunjufu Baraka yangu ya Kitume kwenu na kwa wote wanaoshiriki katika maadhimisho haya muhimu.” Papa Leo alihitimisha barua yake."

Papa kwa Chuo cha Kanisa

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here

17 Januari 2026, 14:24