Papa Leo XIV,Ubatizo wa Bwana:Ubatizo ni nuru na upatanisho
Na Angella Rwezaula-Vatican.
Sakramenti ya Ubatizo inatimiza tukio hili la kila wakati na kila mahali, kwa kuanzisha upya kwa kila mmoja wetu katika Kanisa, ambalo ni Watu wa Mungu, walioundwa wanaume na wanawake wa kila taifa, na utamaduni, waliozaliwa na Roho wake. Tujikite kuanzia siku hii, kufanya kumbukumbu ya zawadi kubwa tuliyoipokea, tujitahidi kuishuhudia kwa faraha na kwa uthabiti. Haya yamo katika mahubiri ya Baba Mtakatifu Leo XIV, kabla ya sala ya Malaika wa Bwana Dominika ya Sherehe za Ubatizo wa Bwana ambapo Papa alibatiza pia baadhi ya Watoto wa Wafanyakazi wa Vatican ishirini tarehe 11 Januari 2026.
Akiwageukia waamini na mahujaji wapatao 25,000 waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, Papa Leo XIV alisema "siku kuu ya Ubatizo wa Bwana ambayo leo tunaadhimisha, inatoa mwanzo wa Kipindi cha Kawaida, kipindi hiki cha mwaka wa kiliturujia kinachotualika kufuata pamoja Bwana, kusikiliza Neno lake na kuiga ishara zake za upendo kuelekea jirani. Na ndivyo hivyo kiukweli, ambavyo tunajithibitisha na kujipyaisha ubatizo wetu, yaani Sakramenti ambayo inatufanya kuwa wakristo, kutukomboa kutoka katika dhambi na kutubadilisha kuwa wana wa Mungu, kwa uwezo wa Roho wake wa maisha."
Papa Leo XIV, aliendelea kukazia kuwa Injili ambayo tulisikiliza inasimulia jinsi ishara hiyo inavyozaliwa kwa dhati kutoka katika neema. Yohane alipobatizwa katika Mto Yordani, Yesu aliona "Roho wa Mungu akishuka kama Hua na kushuka juu yake(Mt 3,16). Na wakati huo huo, Mbingu zilifunguka na ikasikika sauti ya Baba ikisema, “Huyo ni Mwanangu mpendwa”(Mt 3, 17). Kwa hiyo Utatu wote unakuwepo katika historia: kama Mwana aliyeshuka katika maji ya Yordani, na ndivyo Roho Mtakatifu anashukuka juu Yake, na kwa njia yake, tunapewa kwa nguvu ya wokovu.
Baba Mtakatifu Leo XIV aliendelea kusema, "Wapendwa Mungu hatazami dunia kwa mbali, bila kugusa maisha yetu, makosa yetu na matarajio yetu! Yeye anakuja katikati yetu kwa hekima ya Neno lake lililofanyika mwili, kwa kutuhusisha kwa mshangao wa mpango wa upendo kwa ajili ya ubinadamu wote. Tazama ndiyo maana, Yohane Mbatizaji, kwa kujazwa na mshangao anauliza Yesu: “Wewe unakuja kwangu (Mt 3,14). Ndiyo, katika utakatifu wake Bwana anajifanya kubatizwa kama wadhambi wote, ili kuonesha huruma ya Mungu isiyo na kikomo. Mzaliwa wa kwanza ambaye sisi ni kaka na dada, anakuja kwa hakika kuhudumu na siyo kwa ajili ya kutawala, kwa ajli ya kuokoa na siyo kwa ajili ya kuhukumu. Yeye ni Kristo Mkombozi: anachukua kile ambacho ni chetu na anatupatia kile ambacho ni chake, yaani neema ya maisha mapya na ya milele.
Baba Mtakatifu alisisitiza kwamba: "Sakramenti ya Ubatizo inatimiza tukio hili la kila wakati na kila mahali, kwa kuanzisha upya kwa kila mmoja wetu katika Kanisa, ambalo ni Watu wa Mungu, walioundwa wanaume na wanawake wa kila taifa, na utamaduni, waliozaliwa na Roho wake. Tujikite kuanzia siku hii kufanya kumbukumbu ya zawadi kubwa tuliyoipokea, tujitahidi kuishuhudia kwa faraha na kwa uthabiti.”
Ni kwa njia hiyo, Papa aliongeza, leo nimebatiza baadhi ya watoto, ambao wamewakuwa kaka na dada wapya katika imani: ni jinsi gani ilivyo nzuri kuwa kama familia moja ya upendo wa Mungu, ambaye anatuita kwa jina na anatukomboa dhidi ya ubayal Moja ya Sakramenti ni ishara takatifu ambayo inatuzindikiza milele. Katika masaa ya giza, Ubatizo ni nuru; katika migogoro ya maisha, Ubatizo ni upataisho; katika saa ya kifo, Ubatizo ni mlango Wa mbingu. Kwa kuhitimisha Papa alisema: "tusali pamoja na Bikira Maria kwa kuomba kwamba atusindikize kila siku imani yetu na utume wa Kanisa.”
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.
