2026.01.28 Mkutano wa XIII wa Shirikisho la Makanisa ya Afrika ya Kati(ACERAC)huko N’Djaména-Chad. 2026.01.28 Mkutano wa XIII wa Shirikisho la Makanisa ya Afrika ya Kati(ACERAC)huko N’Djaména-Chad. 

Papa Leo XIV,Maaskofu wa ACERAC:Kuifanya Injili iwepo katika kiungo cha kijamii!

Katika ujumbe wake,uliosainiwa na Katibu Mkuu wa Vatican,Kardinali Parolin,katika fursa ya Mkutano Mkuu wa XIII wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Kanda ya Afrika ya Kati,Papa Leo XIV alihimiza uinjilishaji mpya mbele ya maovu yanayodhoofisha jamii,kama vile ukabila,migogoro ya kikabila,vita na mgawanyiko wa kifamilia.Lazima kutafuta mitindo inayofaa kwa ajli ya kutangaza Injili kwa kila utamaduni.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV alituma ujumbe wake uliosainiwa na Katibu Mkuu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, kwenye hafla ya Mkutano Mkuu XIII wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Kanda ya Afrika ya Kati, (ACERAC). Papa katika barua hiyo anaeleza kuwa: “Kila sehemu ya dunia ina majeraha yake. Katika Afrika ya Kati, majeraha haya huchukua umbo la "ukabila," migogoro ya "kabila" na mgawanyiko ndani ya familia. Lakini pamoja na majeraha haya, tamaduni tajiri na tofauti zinaishi pamoja, zikiitwa kuwa ardhi yenye rutuba kwa ajili ya kutangaza Neno. Papa Leo aliongeza kusema kuwa hili sio suala la "kuibadilisha Injili na ulimwengu," bali kuanzisha "uinjilishaji mpya" wenye uwezo wa kuzungumza na mioyo na kuzalisha upatanisho. Pia wanaoshiriki katika tukio hilo ni pamoja na Kardinali Fridolin Ambongo, Askofu Mkuu wa Kinshasa, na Rais wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika na Madagascar (SECAM), na Kardinali Michael Czerny, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Maendeleo Fungamani ya Binadamu.

Mkutano wa Kanda ya Kati wa Maaskofu
Mkutano wa Kanda ya Kati wa Maaskofu

Kuifanya Injili iwepo katika kiungo cha Kijamii

Maandishi ya Kifaransa, yaliyosomwa mnamo tarehe 26 Januari 2026 wakati wa ufunguzi wa Mkutano huko mji mkuu N'Djamena,  nchini Chad, na Balozi wa Vatican, Giuseppe Laterza, yalianza na salamu kwa Rais wa Acerac, Askofu Martin Waïngue Bani. Kisha mawazo ya Baba Mtakatifu kwa Maaskofu, ambao hujitolea kila siku kuhudumia jamii zilizokabidhiwa kwao, na kwa mapadre, "washirika wao wa kwanza." Mikutano ya kawaida ya Acerac, inakuza ushirikiano wa pande zote, ikiimarisha ukweli wa Kikristo na kukuza uhusiano na jamii zingine za kidini na mamlaka za kiraia. Kuifanya Injili iwepo katika utamaduni na muundo wa jamii; kukuza ulinzi wa maisha ya binadamu, amani, na haki; kuwatunza waathiriwa walio hatarini wa migogoro; na kutetea kazi ya uumbaji.

Mkutano Mkuu wa Maaskofu wa Afrika Kati
Mkutano Mkuu wa Maaskofu wa Afrika Kati

Papa pia alikumbuka kwamba mwaka huu 2026, Kanisa linaadhimisha kumbukumbu ya miaka 31 ya Wosia wa Kitume wa baada ya Sinodi, "Ecclesia in Africa", (Kanisa  Barani Afrika) ambao unasema kwamba bara linapitia "kile kinachoweza kuitwa ishara ya nyakati, wakati wa kufariji, siku ya wokovu." Jumuiya ya Kanisa mahalia, Papa Leo XIV aliongeza kuwa, ni ukweli ulio hai, imara, na wenye nguvu, na maneno ya Wosia yanabaki wakati unaofaa kabisa katika kukabiliana na changamoto za leo. Kama wachungaji, kama Familia ya Mungu, mnajikuta mnakabiliwa na masuala ya dharura ambayo yanajitokeza kwa ukali maalum katika kazi yenu ya kichungaji. Eneo muhimu ni utamaduni wa imani. Sio suala la kurekebisha Injili kulingana na ulimwengu, bali ni kutafuta katika kila utamaduni njia zinazofaa za kutangaza Neno ambalo halipiti kamwe, linalotajirisha na kutumikia uwepo wa mwanadamu.”

PAPA KWA AFRIKA YA KATI

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here.

29 Januari 2026, 17:44