Papa Leo XIV,Gazeti la ili Foglio:Sauti ya kuhakikisha uhuru bila mgawanyiko
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Uhuru wa maoni, uwajibikaji katika kuripoti ukweli, heshima kwa utofauti wa mawazo, mazungumzo ili kukabiliana na ubaguzi wa msimamo mkali na udanganyifu, kuelimisha kwa kutoa taarifa, na mustakabali wa kukutana, ndizo mada msingi ambazo Baba Mtakatifu Leo XIV amezionesha ili kuzitumia katika kujenga ulimwengu wa haki na amani zaidi katika ujumbe wake wa tarehe 23 Januari 2026, ulioutumwa kwa Claudio Cerasa, mhariri wa Gazeti la Il Foglio, la Italia , wakati wa maadhimisho ya miaka 30 ya gazeti hilo. Gazeti hili lilianzishwa mjini Roma kunako tarehe 30 Januari 1996, na Giuliano Ferrara, ambaye aliliongoza hadi mwaka 2015,ambapo gazeti hilo lililenga tangu mwanzo kuwa jukwaa la kubadilishana maoni.
Uwezo wa kusambaza maoni na kutoa tafsiri tofauti za ukweli
Papa Leo XIV alitoa matashi mema na akakumbusha kwamba katika miaka ya mabadiliko makubwa kama haya, uwepo wa toleo la wingi katika uwanja wa habari, ambao wamechangia katika kazi yao, umekuwa na ni dhamana ya uhuru. Uwezo wa kusambaza maoni mbalimbali na kutoa tafsiri tofauti za ukweli ni msingi halisi wa ubadilishanaji huru wa mawazo ambao bila huo hakuna uhuru wa mawazo, bali ni kunyimwa hadhi ya kila mwanadamu na haki yake ya kufikiri.
Tuendeleza mazungumzo na tusijisalimishwa upendeleo wa misimamo mikali
Kuanzia na dhana hizi, Baba Mtakatifu alisisitiza hitaji la majadiliano ili kuepuka kuanguka katika makundi yenye mipaka ambayo hayawezi kukamata ukweli. “Ni lazima tuendeleze mazungumzo na tusijisalimishe kwa upendeleo wa msimamo mkali na wa udanganyifu ambao hupunguza ukweli kuwa mzaha, mizizi ya kiutamaduni na kidini karibu na lebo za kuonyeshwa, na kufikiriwa kuwa hesabu.”
Vyombo vya habari huru na kwa vyote vina kazi maalum ya kuelimisha kwa kutoa taarifa sahihi
Katika ujumbe huo Papa Leo anabainisha kuwa , “Vyombo vya habari huru, na kwa ujumla vyombo vyote vya habari vina kazi hii maalum ya kuelimisha kwa kutoa taarifa. Kazi inayopaswa kufanywa kwa hisia kubwa ya uwajibikaji, ikitofautisha kati ya kuripoti ukweli kwa njia isiyo na upendeleo na usemi wa maoni juu yake, ambayo huwa wazi kila wakati kwa majadiliano. Na hivyo kuchangia katika ujenzi wa ulimwengu wa haki na amani zaidi.” Matashi yake mema Papa Leo XIV kwa wahariri wa gazeti hilo ni "kuhamasishwa kila wakati na hamu hii ya kujenga mustakabali wa kukutana na sio migogoro, na hivyo kutetea uzuri wa maisha yetu.”
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here
