2025.11.17 Vescovi Conferenza Epsicopale Kenya Programma Portoghese

Papa amemteua Askofu Mkuu Mwandamizi wa Mombasa Kenya,Dominic Kimengich

Askofu Dominic Kimengich hadi uteuzi huo alikuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Eldoret.Alizaliwa tarehe 23 aprili 1961,Kituro nchini Kenya.

Na Angella Rwezaula, - Vataican

Jumatano tarehe 28 Januari 2026, Baba Mtakatifu Leo  XIV alimteua Askofu Dominic Kimengich kuwa Askofu Mkuu Mwandamizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Mombasa nchini Kenya. Hadi uteuzi huo alikuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la  la Eldoret.

Alizaliwa kunako tarehe 23 aprili 1961, Kituro. Majindo yake: Alisoma Falsafa katika Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustine na Taalimungu  katika Seminari Kuu ya Mtakatifu Thomas Aquinas jijini Nairobi. Alipewa daraja la Upadre  mnam tarehe 14 Septemba 1986.

Nyadhifa

Katika Utume wake wa kichungaji ameshikilia nafasi mbali mbali na kuendelea na masomo zaidi: Paroko wa Parokia huko Ndana (1986-1988); Paroki wa  Parokia huko Kipsaraman (1988-1993); Cheti na Shahada ya Uzamivu katika Sheria ya Kanisa kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Msalaba Mtakatifu jijini Roma; Mkuu wa Seminari Ndogo ya Mtakatifu Joseph huko Molo (1997-2001); Paroko katika Parokia ya Jimbo la  Nakuru (2001-2007); na Mkuu wa Seminari Kuu ya Mtakatifu Matthias Mulumba huko Tindinyo (2007-2008).

Mnamo tarehe 20 Machi  2010,aliteuliwa kuwa Askofu Msaidizi wa Lodwar na kuwa na kiti cha Tanaramusa.  Mnamo tarehe 5 Machi 2011 aliteuliwa kuwa Askofu wa Lodwar na, mnamo tarehe 16 Novemba 2019, aliteuliwa kuwa Askofu wa Eldoret.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here

 

28 Januari 2026, 17:44