Papa kwa chakula cha mchana cha kushtukiza na Maaskofu wa Peru,mjini Roma
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Ishara ya ukaribu na ushirika ambao unaongeza nguvu ya utume wa kichungaji wa Kanisa nchini Peru. Hivi ndivyo ulivyoelezwa "mshangao mzuri na usiotarajiwa" ambao Maaskofu wa nchi ya Amerika Kusini waliupokea, Alhamisi tarehe 29 Januari 2026, kutoka kwa Papa Leo XIV.
![]()
Papa aliwatembelea Maaskofu wa Peru wakati wa "chakula cha mchana cha kidugu," kama ilivyoelezwa katika Ukurasa wa X wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Peru, wakiwa Roma kwa ziara yao ya Kichungaji(Visita ad limina,) iliyopangwa tangu Januari 26 hadi 31.
![]()
Maaskofu 46 wanashiriki Ziara ya Kichungaji mjini Vatican na Roma
Wanaoshiriki katika Ziara hiyo ya Kichungaji ni Maaskofu walioko katika mamlaka 46 za kikanisa za nchi hiyo ya Amerika Kusini, ambapo, Askofu Robert Francis Prevost wa wakati ule alihudumu kama mmisionari kwa zaidi ya miaka ishirini na baadaye kama Askofu wa Jimbo la Chiclayo. Maaskofu wanatrajiwa kukutana na Baba Mtakatifu Leo XIV, Ijumaa tarehe 30 Januari 2026.
![]()
"Ungana na Uongeze"
"Tuko hapa kuomba amani na mustakabali wa Peru, ili ziara hii ituimarishe sote na kututia moyo katika imani ili tuhudumie vyema,"alisema Askofu Carlos García Camader, Askofu wa Jimbo la Lurín na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Peru. "Tunaomba kwamba viongozi wetu wa baadaye wawe wanaume na wanawake wema wanaotumikia taifa, wanaotafuta manufaa ya wote, na, zaidi ya yote, wajitahidi kuungana na kuongeza, si kupunguza au kugawanya," aliongeza.
![]()
Zawadi ya Musa na Picha ya Mtakatifu Rosa wa Lima
Baraza la Maaskofu wa Peru wametoa zawadi ya Picha ya Bikira Maria Mwenye Heri na picha ya Mtakatifu Rosa wa Lima, ambayo itabarikiwa na kuwekwa katika Bustani za Vatican Jumamosi, tarehe 31 Januari 2026. Ziara mbili za mwisho za kichungaji (Visita ad limina) za Maaskofu wa nchi hiyo ya Peru zilikuwa: Mei 2017, na Papa Francisko na mnamo Mei 2009, na Papa Benedikto XVI.
![]()
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here
