Papa akutana na Spika wa Bunge la Ulaya,Roberta Metsola
Vatican News.
"Ilikuwa asubuhi yenye maana mjini Vatican wakati wa Mkutano na Baba Mtakatifu Leo XIV. Tunashukuru kwa uwazi wa nia zake na kwa tafakari zetu za pamoja kuhusu maendeleo ya amani kupitia mazungumzo barani Ulaya na duniani." Haya yamo katika chapisho lililochapishwa kwenye akaunti yake rasmi ya X, ya Spika wa Bunge la Ulaya, Bi Roberta Metsola, akitoa maoni kuhusu Mkutano wake, Alhamisi tarehe 29 Januari 2026, na Papa Leo XIV katika Jumba la Kitume mjini Vatican.
Bi Metsola alitembelea Roma ambapo alipokelewa na Papa, akifuatana na ujumbe wa watu watano, na baadaye alikutana na Katibu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin.
Katika ziara yake pia asubuhi hiyo, alikuwa akutane na mamlaka ya Jamhuri ya Italia, kama sehemu ya mazungumzo kati ya taasisi za kitaifa na kidini za Ulaya kuhusu mada za mwanzilishi wa Umoja wa Ulaya; Mkutano na Waziri Mkuu Giorgia Meloni katika Jumbe la Chigi. Alasiri, Spika wa Bunge la Ulaya alikuwa azungumze kuhusu hafla ya: "Urithi wa De Gasperi: Ulaya katika Kutetea Uhuru," iliyofanyika katika jengo la Bunge la Ulaya kwenye Uwanja wa Venezia.
Matukio hayo yalikuwa yanajumuisha mkutano kati ya Metsola na Mkuu wa Shirika la Kijeshi la Malta, Ndugu' John Dunlap, katika Jumba la Mahakimu Roma. "Ziara ya heshima, wakati huo hiyo" taarifa ilielezea, "ilikuwa fursa ya kupata taarifa mpya kuhusu shughuli za Shirika la Kijeshi la Malta katika zaidi ya nchi 130 duniani kote. Spika alitoa shukrani kubwa kwa kazi ya kibinadamu ya Shirika katika hali ngumu kama vile Ukraine na Gaza."
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here
