Venezuela: Jumatano Januari 11,2026Papa alikutana na Mshindi wa Tuzo ya Nobel Maria Corina Machado. Venezuela: Jumatano Januari 11,2026Papa alikutana na Mshindi wa Tuzo ya Nobel Maria Corina Machado. 

Papa akutana na Mshindi wa Tuzo ya Nobel,Maria Corina Machado

Mwanasiasa na mwanaharakati wa Venezuela Bi Machado alikutana na Baba Mtakatifu Leo XIV,Jumatatu Januari 12,katika Jumba la Kitume mjini Vatican.

Vatican News

Mwishoni mwa asubuhi iliyojaa mikutano katika Jumba la Kitume la Vatican, Baba Mtakatifu Leo XIV alikutana Jumatatu tarehe 12 Januari 2026, María Corina Machado, mbunge wa zamani wa Bunge la Venezuela ambaye alipewa Tuzo ya Nobel ya Amani mnamo mwezi Oktoba 2025.

Corina Machado,Mwanaharakati wa Venezuela
Corina Machado,Mwanaharakati wa Venezuela   (@Vatican Media)

Kukamatwa kwa Maduro mnamo Januari 3

Mkutano huo umefanyika kwa takriban siku kumi baada ya kukamatwa kwa Nicolas Maduro na mkewe, Cilia Flores, wakati wa operesheni ya kijeshi ya Marekani iitwayo "Operesheni Absolute Resolve" mnamo tarehe 3 Januari 2026  huko Caracas. Maduro, anayetuhumiwa kwa biashara ya dawa za kulevya na ugaidi wa dawa za kulevya, kwa sasa anashikiliwa katika Kituo cha Magereza cha Mji  wa  Brooklyn, nchini Marekani.

Kwa njia hiyo Mwanasiasa wa Venezuela na mwanaharakati wa haki za binadamu, Machado anaongoza chama cha kiliberali cha "Vente Venezuela", ambacho kimekuwa kikipinga serikali ya Maduro kila mara. Akiwa amekimbia nchi, alisafiri hadi Oslo mnamo Desemba kupokea heshima hiyo muhimu.  Wakati Juma hili huko Venezuela likitawaliwa kwa muda na Delcy Rodriguez, na huku kazi ikifanywa kwa ajili ya mpito unaoungwa mkono na Jumuiya ya kimataifa ( siku hizi, zaidi ya hayo, habari za kuachiliwa kwa wafungwa kadhaa wa kisiasa zikisikika), mshindi wa Tuzo ya Nobel  anatarajiwa kwenda Washington kwa ajili ya mkutano na Rais Donald Trump, kulingana na tangazo la mwisho.

Mwanaharakati wa Venezuela
Mwanaharakati wa Venezuela   (@Vatican Media)

Wito wa  Papa kwa Venezuela

Wakati huo huo, Januari 12, katika mkutano wa pamoja mjini Vatican, na Papa Leo XIV, ambaye katika  Sala ya Malaika wa Bwana mnamo Januari 4, siku moja baada ya kukamatwa kwa Maduro , ambapo takriban wanajeshi na raia 80 wa Venezuela na Cuba walifariki dunia  alisema jinsi ambavyo alikuwa akifuatilia matukio nchini Venezuela "kwa moyo uliojaa wasiwasi." "Wema wa watu wapendwa wa Venezuela lazima ushinde mambo mengine yote na kusababisha kushinda vurugu na kuanza njia za haki na amani, kuhakikisha uhuru wa nchi."


Papa alisema kutoka dirishani mwa Jumba la Kitume, huku akitoa wito wa kuheshimiwa kwa "haki za binadamu na za kiraia za kila mtu," kufanya kazi "kujenga pamoja mustakabali tulivu wa ushirikiano na maelewano, kwa umakini maalum kwa maskini zaidi wanaoteseka kutokana na hali ngumu ya kiuchumi." Wito huo pia ulirudiwa katika tarehe 9  Januari 2026  kwa kikundi cha  Kidiplomasia kilichoidhinishwa na Vatican wakati wa mkutano, alipotaja nchi ya  Venezuela, na kuwasihi "kujenga jamii iliyojengwa juu ya haki, ukweli, uhuru, na udugu, na hivyo kupona kutokana na mgogoro mkubwa ambao umeikumba nchi kwa miaka mingi." Pamoja na hayo, alihimiza "kuheshimu mapenzi ya watu wa Venezuela" na "kujitolea kulinda haki za binadamu na za kiraia za kila mtu na kujenga mustakabali wa utulivu na maelewano."

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here

12 Januari 2026, 16:37