Papa akutana na Maaskofu wa Slovenia:Wito wa Sinodi na Udugu

Baba Mtakatifu Leo XIV ameanza kupokea Maaskofu wakiwa katika Ziara ya kichungaji (Visita ad limina),Ijumaa Januari 16 kwa kupokea Baraza la Maaskofu wa Slovenia katika Jumba la Kitume mjini,Vatican.Askofu Saje,Rais wa Baraza hilo,alibanisha kuwa:"alitukaribisha na kutusikiliza kwa njia ya udugu,akiwa makini sana na changamoto na maisha ya Kanisa letu."

Vatican News

Juma moja la mikutano, sala, na majadiliano ilifikia kilele cha Mkutano katika Jumba la Kitume mjini Vatican na Baba Mtakatifu Leo XIV, Ijumaa tarehe 16 Januari 2026. Hawa ni Maaskofu wa nchini Slovenia wakielezea ziara yao ya Kichungaji ijulikanayo “Visita ad limina” kwa vyombo vya habari vya Vatican. Desturi hii ya Maaskofu ilianza tena na Papa Leo XIV, mara baada ya mapumziko marefu kutokana na kulazwa hospitalini na kifo cha Papa Francisko. Kwa njia hiyo wamekuwa wa kwanza kwa Papa Leo kama mwendelezo wa kiutamaduni wa ziara hii ya kichungaji.

Mkutano wa Maaskofu wa Slovenia na Papa Leo XIV
Mkutano wa Maaskofu wa Slovenia na Papa Leo XIV   (@Vatican Media)

Askofu Andrej Saje, rais wa Baraza la  Maaskofu wa Slovenia, alisisitiza kwamba “mkutano na Papa Leo XIV, ambaye alikuwa amekutana naye alipokuwa Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Maaskofu, ulikuwa "uzoefu mzuri" hata kwa Maaskofu wengine  waliokuwa wakifanya ziara yao ya "Visita ad limina," kwa mara yao ya kwanza. "Alitupokea kidugu sana," alisisitiza Askofu  Saje, ambaye aliwasilisha salamu na sala za waamini kutoka  Slovenia kwa Papa Leo XIV.

Miongoni mwa mada zilizojadiliwa ni maisha ya Kanisa mahalia na changamoto zinazolikabili kanisa hilo "ambazo," Askofu alisema, "zinafanana na zile za nchi nyinginezo, lakini zenye mambo fulani maalum, kama vile urithi wa ukomunisti."

Ziara ya Kichungaji ya Maaskofu wa Slovenia
Ziara ya Kichungaji ya Maaskofu wa Slovenia   (@Vatican Media)

Ushirika na Sinodi

Askofu Saje kadhalika alisisitiza kuwa, “Papa Leo XIV, pamoja na kutoa wito wa maendeleo katika njia ya sinodi, alitutia moyo kusonga mbele, akipendekeza "ushirika," miongoni mwetu maaskofu, mapadre, watawa wa kike na kiume, familia, na watu wa kawaida walei." Na zaidi ushiriki huu lazima uhusishe kumsikiliza Roho ili kuelewa vyema kile ambacho Bwana anasema na kumkabidhi hata wasiwasi wa wakati huu.” "Kuweni marafiki, na ndugu," Papa alisema, "kwa sababu ninyi ni warithi wa mitume. Wainjilishaji," aliongeza rais wa Baraza la Maaskofu wa Slovenia, "ili kueneza Injili kwa upana zaidi."

Mkutano wa Papa na Baraza la Maaskofu wa Slovenia
Mkutano wa Papa na Baraza la Maaskofu wa Slovenia   (@Vatican Media)

Wakati wa Juma hili la Ziara yao ya Kichungaji katika Mji Mtakatifu, Maaskofu walipata kutoa heshima kwa makaburi ya Watakatifu Petro na Paulo na kufanya mikutano ipatayo ishirini katika Mabaraza ya Curia Romana.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here

 

16 Januari 2026, 18:26