2025.10.11 Wakati wa Mkesha wa Sala na Rozari kwa ajili ya amani (11.10.2025). 2025.10.11 Wakati wa Mkesha wa Sala na Rozari kwa ajili ya amani (11.10.2025).  (@Vatican Media)

Nia za Maombi za Papa Leo XIV kwa Mwaka 2027

Utu wa binadamu,sanaa,maisha,wahamiaji,wazee,vijana,akili unde,ni baadhi ya mada zilizo katikati ya nia maombi ambazo Papa amekabidhi kwa Mtandao wake wa Maombi Ulimwenguni kwa mwaka ujao.

Ifuatayo  ni orodha ya nia za maombi kwa kila mwezi ambazo Baba Mtakatifu Leo XIV alikabidhi Mtandao wake wa "Nia za Maombi ya Papa Ulimwenguni kwa Mwaka 2027":

Januari 

Kwa ajili ya kugundua nguvu ya sala. Tusali ili sisi sote, katika Kanisa, tugundue nguvu ya sala kama mkutano wa kibinafsi na Bwana, ambaye anabadili moyo wetu na Ulimwengu.

Februari

Kwa ajili ya utunzaji wa wale wanaowajali wengine. Tunawaombea wale wanaojali afya kamili ya wengine: ili wapate msaada unaohitajika na, kwa uvumilivu, hekima, na nguvu, njia wazi za uponyaji wa ndani na matumaini.

Machi 

Kwa ajili ya kuheshimu utu wa maisha ya mwanadamu. Tuombe ili, mbele ya utamaduni unaozingatia uzalishaji na uharaka, tuweze kutambua na kuthamini hadhi ya kipekee ya kila mtu: ile yetu na ya wengine.

Aprili

Kwa ajili ya sanaa, zawadi inayofanya binadamu kuwa wa kawaida. Tuombe ili sanaa ikaribishwe kama zawadi ya kweli inayotufanya tuwe wanadamu zaidi, inayoinua roho zetu, na kutusaidia kutafakari uzuri wa Mungu katika uumbaji.

Mei

Kwa ajili ya fursa za kazi kwa wote. Tuombe ili maendeleo ya kiteknolojia yafungue njia za kazi zenye heshima, na kwamba ushirikiano kati ya vizazi utawezesha mustakabali ambapo kila mtu anaweza kutoa vipaji vyake katika huduma kwa manufaa ya wote.

Juni

Kwa ajili ya matumizi mazuri ya Akili Unde. Tuombe ili maendeleo ya Akili Unde(AI), yawe daima katika huduma ya hadhi ya binadamu, na ili  tujue jinsi ya kuitumia kwa busara.

Julai

Kwa ajili ya babu na bibi na wazee. Tuombe ili sisi sote, washiriki wa Kanisa, tuweze kuthamini hazina ya imani na hekima ambayo babu na bibi na wazee wanatupatia na kuwa tayari kujifunza kutokana na uzoefu wao.

Agosti

Kwa ajili ya wito wa vijana. Tuombe ili vijana, katika kutafuta wito wao, waweze kumtambua katika Yesu Kristo kuwa mwenza wa safari ambaye wanaweza kumfungulia mioyo yao.

Septemba

Kwa ajili ya ubadilishaji fungamani wa ikolojia. Tuombe ili tuweze kujifunza kuishi uhusiano mpya na uumbaji, tukiulinda kwa haki na kupata katika kutafakari uumbaji njia ya kuelekea maisha yenye upatanisho zaidi na utambuzi wa shukrani.

Oktoba

Kwa ajili ya Jumuiya za Kikristo. Tuombe ili kila parokia, jumuiya, au kikundi cha Kikristo kiweze kuwa kitovu cha utume wa kimisionari, kuwafundisha wanafunzi wapya katika huduma ya Injili.

Novemba

Kwa ajili ya ujumuishaji wa wahamiaji. Tuombe ili wahamiaji na watu waliohamishwa, wakisindikizwa na kufarijiwa na Familia Takatifu katika safari yao ya kuhama, waweze kupata jumuiya zinazowakaribisha kwa heshima, mshikamano na ujumuishaji wa kweli.

Desemba

Kwa ajili ya wito wa Kikristo wa familia. Tuombe ili familia za Kikristo ziweze kuwa mashuhuda hai wa Injili katika jamii, zikijifunza zaidi kuwa nyumba ambapo imani, matumaini na upendo vinalishwa.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here

30 Januari 2026, 19:05