Papa Leo XIV kwa vijana-Taize:Pelekeni matumaini ya unyenyekevu na furaha kwa walio karibu nanyi!
Vatican News
Baba Mtakatifu Leo XIV aliwasilisha ujumbe kwa vijana waliokusanyika kuanzia tarehe 28 Desemba 2025, hadi tarehe 1 Januari 2026, huko eneo la Île-de-France -Paris, nchini Ufaransa kwa ajili ya mkutano wa XLVIII barani Ulaya, unaoandaliwa kila mwaka na Jumuiya ya Kiekumene Taizé. Katika ujumbe uliosainiwa na Katibu Mkuu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, kwa washiriki wapatao 15,000, wenye umri kati ya miaka 18 na 35, ambao, kwa mwaliko wa Makanisa ya Ulaya ya madhehebu mbalimbali, wanajikita katika sala na kushiriki, katika roho ya sherehe na urafiki.
Kuweni na uhakika wa kuwa na Yesu karibu
"Ninafurahi kujua kwamba vijana watakusanyika katika mji ulio na urithi mkubwa wa kidini, ulioundwa kwa karne nyingi na ushuhuda unaong'aa wa watu wengi watakatifu ambao, kila mmoja kwa njia yake mwenyewe, wameitikia wito wa Kristo kwa ujasiri, Papa alisema kwamba "mada ya Barua iliyoandikwa mwaka huu na Ndugu Mathayo, Mkuu wa Taizé, 'Unatafuta nini?' unashughulikia swali muhimu linalokaa moyoni mwa kila mwanadamu na inatualika tusiliogope, "bali tulibebe kwa maombi na ukimya," tukijua kwamba Kristo yuko kando yetu na hakika kwamba "anajiruhusu kupatikana na wale wanaomtafuta kwa moyo wa dhati."
Kuishi Injili katika Uhalisia Halisi
Kwa hiyo Papa Leo XIV, anaendelea kubainisha kuwa katika mwaka huu "uliojaa majaribu mengi" kwa wanadamu, ukarimu wa kukaribisha ambao vijana wanapokea huko Paris "kutoka kwa waamini wa asili zote na kutoka kwa watu wenye mapenzi mema ni ujumbe wenye nguvu kwa ulimwengu. Wakati wa maombi na kushirikishana ambao mtapitia katika siku hizi uwasadie kuimarisha imani yenu, mkitambua wazi zaidi jinsi ya kuishi Injili katika uhalisia halisi wa maisha yenu” ndilo tumaini lake Baba Mtakatifu.
Ushirika na Udugu
Ujumbe huo, unaoakisiwa wakati maalum wa kikanisa, unaoadhimishwa na kufungwa kwa Mwaka Mtakatifu wa Jubilei na maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 1700 ya Mtaguso wa Nicaea," kisha anakumbusha kwamba wakati wa mkutano wa maombi ya kiekumene huko Iznik, Papa alizungumzia upatanisho kama "wito unaotoka kwa wanadamu wote wanaosumbuliwa na migogoro na vurugu." Hatimaye, unasisitiza kwamba "hamu ya ushirika kamili miongoni mwa waamini wote katika Yesu Kristo daima huambatana na utafutaji wa udugu miongoni mwa wanadamu wote."
Asante kwa kusoma makala haya. Ikiwa unataka kuendelea kupata taarifa mpya, tunakualika ujiandikishe kwa jarida kwa kubofya hapa: Just click here.
