Papa Leo:fadhila za ibada,upendo,huruma&kujikabidhi za Yosefu zitusindikize
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika Dominika ya Nne ya Majilio na ya Mwisho kabla ya sherehe za Kuzaliwa kwa Bwana, baba Mtakatifu Leo XIV Dominika tarehe 21 Desemba 2025 ameongoza tafakari ya sala ya Malaika wa Bwana kwa waamini na mahujaji waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, mjini Vatican. Akiwa katika Dirisha la Jumba la Kitume, Papa amewasalimia kaka na dada na kwamba katika “katika Dominika ya Nne ya Majilio, Liturujia inatualika kutafakari sura ya Mtakatifu Yosefu. Inatualika yeye kwa namna ya pekee katika wakati ambao Mungu anajionesha kwake, kupitia ndoto, na utume wake(Mt 1,18-24).
Hostoria ya Wokovu
Liturujia kwa njia hiyo Papa aliongeza, "inapendekeza namna hiyo sura nzuri sana ya Historia ya Wokovu, mahali ambapo aliye mstari wa mbele ni mwanamme dhaifu na wa kushindwa, kama sisi, na wakati huo huo jasiri na mwenye nguvu katika imani. Mwinjili Matayo anamwita “mtu mwenye haki(Mt 1,19), na yule anayetambulika kama Mwisraeli tasa wa ibada, ambaye alikuwa anatimiza sheria na kuudhuria hekalu. Zaidi ya hayo, Yosefu wa Nazareth anajionesha kwetu kama mtu makini sana na wa kibinadamu. Tunamwona wakati kabla hata Malaika kujionesha kwake fumbo ambalo linataka kutimizwa ndani ya Maria. Mbele ya hali ngumu ya kuelewa na ya kukubali, yeye hachagui makabiliano ya mchumba wake ajaye, njia ya kashfa na hukumu ya umma, lakini ile ya usiri na kumpa talaka kwa siri(Mt 1,19)."
Ibada ya kidini, ya huruma,usafi wa moyo na hisia adhimu za Yosefu
Baba Mtakatifu alisisitiza kuwa na hivyo anaonesha kutambua maana ya kina zaidi ya ibada yake ya kidini, ile ya huruma. Usafi wa moyo na hisia zake adhimu, lakini, zinageuka tena kuonesha zaidi wakati Bwana alijionesha katika ndoto ya wokovu, akamwelekeza wajibu wake hasiotarajia ambao yeye anapaswa kujikita nao wa kuwa mme wa Bikira Maria Mama wa Masiha. Kiukweli hapa Yosefu, kwa tendo la imani kubwa, anaacha wazi hata ufukwe wake wa usalama na kutupa hadi kulindini, kuelekea wakati ujao ambao hata hivyo, huko mikononi kabisa mwa Mungu. Mtakatifu Agostino, anaelezea namna hii: “katika ibada na kwa upendo wa Yosefu alizaliwa na Bikira Maria Mwana na hasa Mwana wa Mungu (tafakari ya 51, 20.30).
Ibada na upendo, huruma na kujikabidhi ni fadhila za Yosefu
Papa Leo XIV akiendelea alisema ibada na upendo, huruma na kujikabidhi, ndizo fadhila za mtu wa Nazareth ambazo Liturujia ya leo inapendekeza kwetu, ili ziweze kutusindikiza katika siku hizi za mwisho wa Majilio, kuelekea Noeli Takatifu. Ni tabia muhimu, ambazo zinaelimisha moyo katika kukutana na Kristo na kwa ndugu na kwamba tunaweza kusaidiana kuwa mmoja na mwingine , pango la kukaribisha, nyumba karimu, ndoto ya uwepo wa Mungu. Katika kipindi hiki cha neema, tusipoteze fursa kwa kujiweka katika matendo ya, kusamehana, kutiana moyo, kutoa matumaini kidogo kwa watu ambao tunaishi nao na wale ambao tunakutana nao; na kupyaisha katika sala kwa kujikabidihi kimwana kwa Bwana, na kwa mapaji yake, kwa kumkabidhi yote kwa imani. Bikira Maria na Mtakatifu Yosefu watusaidie katika hili, il kuwa kama wao wa kwanza pia na imani na upendo mkuu walimkaribisha Yesu, Mkombozi wa Ulimwengu.
Asante kwa kusoma makala haya. Ikiwa unataka kuendelea kupata taarifa mpya, tunakualika ujiandikishe kwa jarida kwa kubofya hapa: Just click here.
