Papa Leo na Waagostinian:Uwepo wenu Kanisani unasisitiza ushuhuda wa upendo
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV alikutana mjini Vatican Alhamisi tarehe 13 Novemba 2025 wawakilishi wa Shirikisho la Monasteri za Kiagostinian nchini Italia. Katika hotuba yake alielekeza kwenye mwelekeo wa sinodi wa shirika hilo, kwani watawa wanaoishi katika monasteri zinazojitegemea nchini Italia wanakutana ili kuchunguza pamoja karama yao ya pamoja. Kwa njia hiyo aliwapongeza ushuhuda wa ushirika unaotolewa na hali halisi mbalimbali za kitawa zinazounda shirikisho na zimeunganishwa na viapo vyao vya kuishi kulingana na Kanuni ya Mtakatifu Agostino.
Papa alisema “ kusikilizana na kuishi katika utofauti, ushuhuda wa kinabii wa upendo, unaohitajika hasa katika ulimwengu ambao kwa njia nyingi unazidi kuwa wazi kwa mazungumzo na kushiriki." Papa alitoa mwaliko kwao kwamba “ ni kujitolea kwa upendo usiogawanyika kwa wito huu, mkikumbatia kwa shauku maisha ya kikuhani: Liturujia, sala ya pamoja na ya kibinafsi, ibada, tafakari juu ya Neno la Mungu, msaada wa pande zote katika maisha ya jamii. Hii itawapatia amani na faraja, na kwa wale wanaobisha mlango wa monasteri zenu, ujumbe wa matumaini wenye ufasaha zaidi kuliko maneno elfu.”
Papa Leo vile vile alisema kuwa “Monasteri zinazoshiriki karama moja hazibaki zimetengwa bali huzihifadhi kwa uaminifu na, zikipeana usaidizi wa kidugu, ziishi thamani isiyoweza kuepukika ya ushirika. Haya yote yanaangazia jinsi Kanisa linavyothamini aina za ushirikiano zilizotajwa, pamoja na hitaji la kila mtu kukuza na kupata uzoefu halisi wa kuwa sehemu yao, kushiriki katika mipango iliyopendekezwa, ikiwa ni pamoja na katika ngazi ya kitaifa, na kujifungua, inapobidi, fursa maalum za usaidizi kama vile ushirika.
Ni changamoto inayohitaji juhudi nyingi, aliongeza Baba Mtakatifu, "lakini ambayo hatuwezi kuiepuka, hata kwa gharama ya kufanya maamuzi magumu na kujitolea, na kushinda kishawishi fulani cha "kujihusisha" ambacho wakati mwingine kinaweza kuingia katika mazingira yetu. Hii hakika italeta faida kubwa kwa jamii, katika nyanja mbalimbali, hasa ile ya msingi ya malezi. Tukumbuke kile ambacho Mtakatifu Agostino alisema: "Kile mnachotamani ni kizuri, na kinastahili kupendwa sana [...]."
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here
