Rais wa Palestina Bwan Mahmoud Abbas. Rais wa Palestina Bwan Mahmoud Abbas.  (Copyright 2025 The Associated Press. All rights reserved)

Nov 6, Papa Leo XIV atakutana na Rais wa Palestina,Abbas

Mkutano huo utafanyika saa 4.30 masaa ya Ulaya.Ni wa kwanza kati yao,baada ya simu iliyopigwa kunako Julai iliyopita kuhusu kuendelea kwa migogoro huko Gaza na katika Ukingo wa Magharibi.

Na Salvatore Cernuzio – Vatican.

Kwa mara ya kwanza, Baba Mtakatifu  Leo XIV atakutana na Rais wa Palestina , Bwana Mahmoud Abbas. Mkutano huo umepangwa  kufanyika tarehe 6  Novemba 2025, saa 4:30 asubuhi, Majira ya Ulaya katika Jumba la Kitume la Vatican. Papa alikuwa na mazungumzo ya simu na kiongozi wa Palestina, ambaye miaka kumi na moja iliyopita alishiriki katika wakati wa kihistoria wa maombi katika Bustani za Vatican pamoja na Papa Francisko na Rais wa Israeli wa wakati huo Shimon Peres, mnamo Julai 21. Mkazo ulikuwa katika maendeleo ya mgogoro katika Ukanda wa Gaza na vurugu katika Ukingo wa Magharibi. Na wakati wa mazungumzo, kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Habari ya Vatican  iliripoti siku hiyo kuwa Papa alirejesha wito wake wa kuheshimu kikamilifu sheria za kimataifa za kibinadamu, huku akisisitiza wajibu wa kulinda raia na maeneo matakatifu na kupiga marufuku ya matumizi ya nguvu bila ubaguzi na uhamisho wa watu kwa nguvu.

Mkataba uliosainia 2015

Katika mazungumzo hayo ya simu, Papa Leo XIV alikumbuka "miaka kumi ya Mkataba Kamili kati ya Vatican  na Nchi ya  Palestina," uliosainiwa tarehe 26 Juni 2015 na kuanza kutumika tarehe 2 Januari 2016. Kwa hivyo, sasa, Mkutano huo unafanyika mwezi mmoja baada ya kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza, ambapo mashambulizi mapya ya Israeli yamerekodiwa katika siku za hivi karibuni, na kuacha makubaliano ya amani yakiendelea. Hii hakika si ziara ya kwanza ya Abbas  jijini  Vatican.

Maombi ya 2014

Yeye alikutana na Papa Francisko mara kadhaa kwa miaka mingi, na kumekuwa na simu za mara kwa mara kufuatia shambulio la kikatili la Hamas la  tarehe 7 Oktoba 2023, na majibu ya Israeli huko Gaza, ambayo yalionesha mwanzo wa mzozo. Mnamo 2014, wakati wa maombi uliotajwa hapo juu ulifanyika katika Bustani za Vatican, pamoja na kupanda mti wa mzeituni, mbele ya Patriaki wa Kiorthodox Bartholomew I. Tukio hilo, katika kumbukumbu yake ya miaka kumi, vile vile iliadhimishwa na Papa wa Argentina katika eneo hilo hilo mnamo tarehe 7 Juni 2024.

Mkutano wa mwisho  kati ya Rais wa Palestina na Papa Francisko  ilifanyika mnamo tarehe 12 Desemba  2024, ikifuatiwa na majadiliano katika Sekretarieti ya Vatican, ambapo uharaka wa "kupunguza hali mbaya sana ya kibinadamu huko Gaza" ulirudiwa na "umuhimu wa kufikia suluhisho la mataifa mawili kupitia mazungumzo na diplomasia pekee, kuhakikisha kwamba Yerusalemu, iliyolindwa na sheria maalum, inaweza kuwa mahali pa kukutana na urafiki kati ya dini tatu kubwa za Mungu mmoja."

Papa Leo atakutana na Abbas
05 Novemba 2025, 11:06