2025.11.10 Picha ya Makala ya "Leo from Chicago." 2025.11.10 Picha ya Makala ya "Leo from Chicago." 

Kaka“Rob,"Padre“Bob:”safari ya Marekani katika nyayo za safari ya Robert Francis Prevost

Safari ya Marekani,ardhi asili ya Baba Mtakatifu,kati ya sauti,picha na shuhuda kuhusu sura,historia,mizizi,mahusiano na wito wa ambaye tarehe 8 Mei 2025 alichaguliwa kuongoza Kanisa Katoliki la Ulimwengu.

Na Salvatore Cernuzio - Chicago.

"Rob," kaka; "Bob," kaka; "Robert," rafiki, mwenza katika masomo, picnic, na maandamano ya haki za binadamu; "Prevost," mwanafunzi mwerevu, mmisionari, "kiongozi" katika uongozi wa mojawapo ya dini zilizoenea zaidi duniani. Na kisha "Leo," Papa. Papa ambaye kwa kuchaguliwa kwake kila mtu huko Peru kulikuwa na uhakika kwamba kungekuwa, huku Amerika wakitumaini, ndiyo, lakini walikuwa na imani kidogo "kwa sababu alikuwa Mmarekani."

Maisha ya Leo kutoka Chicago
Maisha ya Leo kutoka Chicago

Huko Chicago yake ya asili (Marekani), Robert Francis Prevost daima aliacha alama kwa kila mtu aliyekutana naye, muda mrefu kabla ya kuwa Papa Leo XIV. Shukrani kwa utu wake wa adabu, mkarimu, na utulivu, lakini sio sana kiasi cha kumzuia kujumuika na kupata marafiki wapya. Kama wakati huo huko Beaubien Woods, msitu ulio  kilometa chache kutoka nyumbani kwake utotoni huko Dolton, kitongoji cha Chicago, ambapo alitoka kwa baiskeli yake na kaka yake mkubwa Louis, akikutana na genge la watoto wakitisha kuwapiga. "Rob alisema, 'Acha nizungumze nao.' Alishuka, akafika, na kwa namna fulani akawatuliza.

Historia ya Papa  Leo
Historia ya Papa Leo

Aliwafanya... marafiki," anakumbuka Louis, ambaye sasa ni mkazi wa Florida, ambaye huwasiliana kila jioni na kaka yake mashuhuri na kaka yake wa kati, John, anayejulikana kama Jay—kupitia simu ya video ("Kwa kawaida tunatumia dakika 15 hadi 20 kwenye simu zetu, kuzungumzia tu kile tunachofanya, na kile anachofanya").

Padre Robert il giorno della sua ordinazione

Padre Robert katika siku yake ya kupewa daraja la Upadre 

Mazungumzo, majadiliano, urafiki

Historia hii ya utotoni haikusudiwi kuonesha upekee wa mtu aliyechaguliwa kuwa Papa wa Kanisa la Ulimwengu mnamo Mei 8, bali kutusaidia kugundua utu ambao, tangu miaka yake ya mwanzo, ulionesha mwelekeo wa mazungumzo, majadiliano, na urafiki. Urafiki na watawa wenzake, wanandoa, na familia, hata na mchungaji wa Kilutheri, John Snider wa Minneapolis ambaye, wakati hakwenda kwenye sinema kuona 'The Blues Brothers,' alitumia muda kula chakula cha jioni  huku “akihoji baadhi ya desturi za Kikatoliki.”

Historia ya Papa Leo
Historia ya Papa Leo

Hizi zote ni sifa za kina za mazungumzo, majadiliano, na urafiki za Muagostinian. Wito ambao kijana “Bob” ("Sasa ni Leo, lakini moyoni mwangu yeye ni Bob kila wakati," kila mtu huko Chicago anasema) alikumbatia katika ujana wake na ambayo ilikuwa njia aliyofuata wakati wa masomo yake katika Chuo Kikuu cha Villanova huko Philadelphia na Muungano wa Kitaalimungu wa Kikatoliki huko Chicago.

"Chaguo"

"Alikuwa na heshima kwa wanaume na wanawake. Hakuna shaka kwamba alizingatia wito wake, lakini hiyo ilijumuisha kuwa na marafiki wapendwa sana," anasema Mary Donar-Reale, rafiki wa Prevost kutoka enzi zao za Villanova. Hakuwa mwanafunzi mwenzake, bali alikuwa mwenzake katika safari za kwenda Washington na kikundi cha Pro-Life kushiriki katika Machi ya Maisha, maandamano ya kutetea uhai na haki zote za binadamu.

Hizi ndizo haki ambazo Padre Robert alitetea wakati wa miaka yake huko Peru, ambapo alichagua kuondoka kufuatia ajali mbaya iliyopunguza nusu ya utume wa Mtakatifu Agostino. Ilikuwa wakati muhimu maishani mwake: "Angeweza kufundisha katika seminari au kushikilia nafasi kubwa katika Jimbo au Jimbo kuu," alisema Padre Tom McCarthy Muagostinian,  rafiki wa muda mrefu. "Baada ya kusoma muda wote huo ili kupata Shahada ya Uzamivu katika Sheria ya Kanisa, hatimaye alikwenda wapi? Kwa maskini... Kwa maskini, wanaohitaji mahubiri ya Yesu."

Prevost durante gli anni di missione in Perù

Prevost wakati wa miaka ya utume wake nchini Perù

Katika Huduma kwa Wengine

Chaguo pia lilitokana na masomo yake katika Mafundisho Jamii ya Kanisa, Somo ambalo lilimvutia kila wakati, kama alivyoeleza akikumbuka Sr Dianne Bergant, mtawa mchangamfu aliyemfundisha Papa wa baadaye katika Chuo, (CTU,). "Mara nyingi nilisikia kwamba alikuwa mvulana mcha Mungu sana aliyecheza kama Padre. Mimi pia nilikuwa msichana mcha Mungu sana na nilicheza kama Padre. Sio kawaida kwa watoto waliolelewa kidini kutaka kuwa kitu fulani Kanisani. Kinachoshangaza kumhusu ni jinsi alivyotumia kile alichopewa na Mungu, kwa asili, jinsi alivyokitumia, maamuzi aliyofanya. Hakuinuliwa juu ya kiburi, bali alijiweka katika huduma kwa wengine. Hii ilimfanya awe wa kipekee."

Historia, simulizi ambazo hazikuwahi kusimuliwa, mahojiano, na picha kutoka miaka ya Papa  Leo XIV,  nchini Marekani zote zimo katika makala ya "Leo kutoka Chicago," uzalishaji wa ke ni wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano iliyotangazwa  kuanzia tarehe 10 Novemba  kwenye Radio Vatican - Vatican News.

Lro From Chicago

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here

11 Novemba 2025, 09:15