Kardinali  Edoardo Menichelli aliaga dunia tarehe 20 Oktoba 2025. Kardinali Edoardo Menichelli aliaga dunia tarehe 20 Oktoba 2025. 

Rambi rambi za Papa kwa kifo cha Kard.Menichelli: Alitumikia Kanisa na Vatican kwa kujitolea

Papa Leo XIV anamfafanua Kardinali Menichelli Askofu Mkuu Mstaafu wa Ancona -Osima kuwa Mchungaji mwenye bidii wakati wa uhai wake,aliyeaga dunia tarehe 20 Oktoba 2025 akiwa na umri wa miaka 86.

Vatican News

Papa Leo XIV ametuma salamu za rambi rambi katika telegram aliyomtumia Askofu Mkuu Angelo Spina wa Jimbo Kuu Katoliki la Ancona – Osimo, “baada ya kupata habari za kifo cha Kardinali Edoardo Menichelli,” Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu hilo, ambaye aliundwa ukardinali na Papa Francisko kunako mwaka 2015, kilichotokea tarehe 20 Oktoba 2025 akiwa na miaka 86.  Baba Mtakatifu Leo XIV anaelezea “rambi rambi kwa msiba huo uliowakumba Jumuiya ya kikanisa na ile ya Chieti – Vasto ambapo alitoa huduma yake ya kichungaji kwa bidii, kama ilivyo pia Jimbo Kuu Camerino – Mtakatifu Severino Marche mahali ambapo alikuwa kuhani mkarimu.”

Baba Mtakatifu Leo XIV aliandika kuwa, “Katika kukumbuka kaka yetu mpendwa ambaye alihudumia Kanisa na Kiti kitakatifu kwa kujitolea, ninainua sala kwa Bwana, ili kwa maombezi ya Bikira Maria, ampokee katika Yerusalemu ya Mbingu “ na kwa kuhitimisha Baba Mtakatifu aanabainisha: “kwa moyo wote ninawatumia baraka ya kitume kwa familia, wale ambao kwa upendo walimuhudumia na wote wanaoshiriki katika ibada ya mazishi.”

Papa atuma rambi rambi

 

 

 

 

22 Oktoba 2025, 10:34